Mr Nice afunguka kuhusu utajiri wake

Mr Nice afunguka kuhusu utajiri wake

Kuna mwngine nae atakuja dai hivyo hivyo ngoja aendelee tu kuleta magari ya zamani na kudanganya kanunua kwa bethidei

Teh teh hiyo nimeipenda, hata mimi nili notice plate number nikabaki naguna!
 
Sijawahi kuona Mchaga kilaza kama huyo,,,alikua anatembea na Taksi mbili kutwa nzima moja yake nyingine ya wapambe afu anasema hajui Pesa imeishia wao? Teh teh teh teh...ndio hapo huja msemo "NINGE"

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.

Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.

“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana”

Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.

Lucas-Mkenda-aka-Mr-Nice.jpg

Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.

Majuto ni mjukuu lakini hujachelewa kaka,
jamaa alikuwa na matumizi mabaya sana pia alikuwa mgomvi mno . nakumbuka siku moja tukiwa pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere Mr nice alikuwa amerejea toka comoro akiwa na wacheza show wake alikuwa anakuja bear kwa fujo mno na kucheza hovyo alikuwa kero kwa kila mtu. lkn katika hari ya kushangaza Mr nice alichukua pombe yake ambayo ilikuwa kwenye kopo na kumwagia mzungu aliyekuwa amekaa pasipo hili wala lile.
na kisha akawa anamtolea maneno ya kijeri akisema mimi natembea dunia nzima na pesa ninayo hata huko kwenu wazungu wenzako wananitetemekea.
sawa polisi wetu wakamwita chemba na kuongea naye baada ya muda mfupi akaondoka, sasa hilo ni tukio moja la muda usiozidi dakika thelathini sasa vp kwa masaa 24, nani anajua wale polisi uliwapa bei gani?

pia kuna jamaa alitoka malawi akawa analalamika juu yako anasema kwa jinsi alivyokuwa nakupenda akaona ni bora akupe zawadi ya gari , jamaa anasema alikupa gari ambayo ilikuwa mark 11 old model nawe hukuonesha kuifurahia japo ulipokea , lakini cha kushangaza ukiwa unaimba kwenye onesho lako na huyu jamaa alikuwa mmoja wa wahudhuliaji na mulionana ukamtambua cha kushangaza ukaita pale kijana atakayeweza kuimba moja ya mashairi ya nyimbo zako na uliahidi kutoa zawadi ambayo hukuitaja , kuna kijana akajitahidi kuimba moja ya nyimbo zako na ukampa ufunguo wa ile gari aliyokupa mshaji , jamaa anasema alijisikia vibaya na kuamua kutoka nje na moyo unamuuma mpk leo kwa kitendo hicho.
inawezekana kabisa ukapata mafanikio makubwa kuliko haya ya mwanzo lkn badili tabia kaka
 
kumbeeee...bas ale jeuri yakö
 
Akili zake mbovu huyo,yeye anahisi Mungu anakuadhibu kwa kuzulumu tu.Dharau ndio zimemfikisha hapo alipo,alikuwa na dharau na kujiona mwenye hela,huyo ndio asahau,hatokuja kufika pale alipofika mwanzo.

Dimond hawezi kuja kufulia kiasi hicho,dimond ana busara na anajua kuwa kuna kesho ndio maana hana dharau za kijinga ila watu tu tu wana jaribu kumnukuu vibaya ili aonekane mbaya.

Kama unasubiri dimond afulie kama alivyo fulia huyu kilaza basi utangoja sana,Dimond amefanya investments huyu mshenzi yeye alikuwa anafanya starehe tu.
 
mr-nicee.png

Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!.
Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.
Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.

“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana”
Alimalizia star huyo kutoka Tz na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.

Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake

wasanii wa kibongo wanakosea wanadhan they can self manage!!!
 
Akuna mipango ya mungu hapo starehe zako na kutokua na mipango kumekuponza

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Majuto ni mjukuu lakini hujachelewa kaka,
jamaa alikuwa na matumizi mabaya sana pia alikuwa mgomvi mno . nakumbuka siku moja tukiwa pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere Mr nice alikuwa amerejea toka comoro akiwa na wacheza show wake alikuwa anakuja bear kwa fujo mno na kucheza hovyo alikuwa kero kwa kila mtu. lkn katika hari ya kushangaza Mr nice alichukua pombe yake ambayo ilikuwa kwenye kopo na kumwagia mzungu aliyekuwa amekaa pasipo hili wala lile.
na kisha akawa anamtolea maneno ya kijeri akisema mimi natembea dunia nzima na pesa ninayo hata huko kwenu wazungu wenzako wananitetemekea.
sawa polisi wetu wakamwita chemba na kuongea naye baada ya muda mfupi akaondoka, sasa hilo ni tukio moja la muda usiozidi dakika thelathini sasa vp kwa masaa 24, nani anajua wale polisi uliwapa bei gani?

pia kuna jamaa alitoka malawi akawa analalamika juu yako anasema kwa jinsi alivyokuwa nakupenda akaona ni bora akupe zawadi ya gari , jamaa anasema alikupa gari ambayo ilikuwa mark 11 old model nawe hukuonesha kuifurahia japo ulipokea , lakini cha kushangaza ukiwa unaimba kwenye onesho lako na huyu jamaa alikuwa mmoja wa wahudhuliaji na mulionana ukamtambua cha kushangaza ukaita pale kijana atakayeweza kuimba moja ya mashairi ya nyimbo zako na uliahidi kutoa zawadi ambayo hukuitaja , kuna kijana akajitahidi kuimba moja ya nyimbo zako na ukampa ufunguo wa ile gari aliyokupa mshaji , jamaa anasema alijisikia vibaya na kuamua kutoka nje na moyo unamuuma mpk leo kwa kitendo hicho.
inawezekana kabisa ukapata mafanikio makubwa kuliko haya ya mwanzo lkn badili tabia kaka

Aiseee kumbe jamaa alikua hivi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndo basi tena ashaharibu!

Alivuma... Uganda utasikia vitoto vya kiganda (ambao hata kiswahili hawajui) wako busy wanacheza huku wanaimba kwa furaha 'kuku kapanda baiskeli'....Alipendwa sana.
 
Suti alikuwa akinunua Uingereza na meno ya dhahabu kuchonga Dubai nakumbuka alichonga meno kwa thamani ya milioni 15 wakati ndugu zake wanalala njaa.....angalia chai jaba aka diamond alivyomjanja Mr.Nice ata kama nyumba anayo MBWA MKUBWA KABISAA

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Teh teh hiyo nimeipenda, hata mimi nili notice plate number nikabaki naguna!

Hana lolote huyo mr nice,alii to.mbea hela yote na ulimbukeni juu,bado diamond naye iko siku mtamsikia tu.
 
Laiti ningejua uja baada yakishatokea.
 
Back
Top Bottom