Naomba niungane na watu walioshauri vizuri, huyu mama ameshatumika vilivyo,akili yake imechoka,umri huo wa 60 yrs kinga ya mwili kwa maradhi, imeshuka, ndo maana serikali haimuhitaji tena, mama huyu anahitaji kupumzika, tena mapumziko murua yatakayofanya akili yake irelax, hiyo fedha yake ipo katika risk sana, fixed deposit ktk uchumi huu ambao thamani ya fedha sio stable sana ni shida, just imagine, ameweka fedha bank wakati dola moja ni tsh 2000 na ndani ya mwaka mmoja inakuwa tsh 3000 ina maana purchasing power imeshuka, akinunua nyumba au kujenga pia kuna risk, risk ya moto, pia turnover rate ni ndogo sana, ubishi wa wapangaji nk, kila jambo lina risk, kuna msemo nilisikia wanauchumi wanasema "Do'nt put all your eggs in one burket" hii ina maana sana, usiweke mayai yako yote katika kapu moja, kwa kuwa kapu likianguka mayai yote yatapasuka na hivyo utapoteza yote, mi nashauri achanganye achukue 40m ajenge nyumba ya kupangisha, 30million aweke fixed deposit, 10m anunue mashamba, 10 m aanze kula bata ajiweke vizuri kiafya nk mwisho nyie watt mkae mbali na hiyo hela ya mama, mtagombana, mtapata laana, tafuteni zenu, ahsanteni sana
Sent using
Jamii Forums mobile app