MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Ukisoma ramani ya kwanza ya Belt-Road Initiative utaona kwamba njia ni Pakistani hadi Lamu na siyo Bagamoyo. Hivyo ina maana Uchina alikuwa na mpango wa kujenga Mega-Port Lamu na siyo Bagamoyo, lakini Jakaya Kikwete akafanya yake.Man, kwenye hili la bandari unatakiwa ukajipange upya manake maelezo yako yana mapungufu kadhaa!!!
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba, kupitia China's Belt & Road Initiative, Mchina alijipanga kuwekeza kwenye miundombinu sehemu kadhaa duniani. Hili nalifahamu vizuri kwa sababu nilikuwa mbeba mikoba wa Beberu moja la Kimarekani wakati wa kufanya research, na moja ya case study ni Bandari ya Bagamoyo!!!
Katika kufikia hilo, Mchina akawa ameigawa dunia kwa mafungu... kule Ulaya akawekeza pesa ya kutosha kwenye Bandari ya Piraeus nchini Greece!!!
Kama alivyo beberu langu lile la Kimarekani linavyopinga hii miradi including mradi wa Bagamoyo, Mabeberu ya Ulaya yakaanza kumwekea figisu figisu Mchina kwenye Bandari ya Piraeus! Kuna wakati EU, huku Italy wakiwa ndi viherehere zaidi, wakaanza kusema kwamba China inaitumia Bandari ya Piraues kufanya biashara haramu!!
Cha ajabu, miezi kadhaa baadae, Italy ile ile ikaingia mkataba wa kibiashara na bandari ile ile!! Na bandari ile ile ambayo walikuwa wanaisemanga, leo hii imeingia kwenye Top 10 of largest terminal ports in Europe wakati uendelezaji wala hujafika ukingoni!!
Hilo ni la Ulaya! Mchina huyo huyo akataka kwenda kumchezea sharubu Marekani kwa kutaka container terminal ya South California! Hadi mara ya mwisho nafuatilia, Senate likaanza kutoa povu hawataki Mchina achukue terminal pale South Port!!
Hilo ni la Marekani!!
Tukija Africa sasa, Mchina anafahamu fika kwamba Africa ni emerging market.Strategy yake ikawa kuigawa Afrika kwa blocks! Kwenye Horn of Africa, akawekeza Djibouti ili hatimae mizigo yake itakayoenda ukanda wa Horn of Africa ipitie Djbouti!
Afrika Mashariki tukawa na competition kati ya Kenya na Tanzania huku Kenya akimkaribisha Mchina ajenge Lamu!!! Kenya walitoa incentives kibao lakini Mchina akachomoa na kuchagua Bagamoyo!
Unlike Djibouti na sehemu zingine Africa, Mchina alitaka kuifanya Bagamoyo iwe ndo central unit! I wish ungeiona ile plan, ambayo in the long run, makao makuu ya mkoa wa pwani yangehamishwa kutoka Kibaha to Bagamoyo!!
Ili kuifanya Bagamoyo kuwa Central Unit kwa kufuata mfumo ule ule wa Shenzhen Uchina, ikapangwa kujengwa not just a port but a megaport! Pamoja na hii megaport, pia na industrial complex pamoja na railway network to connect Bagamoyo na nchi zingine za ukanda wa maziwa makuu pamoja na kusini... Malawi, and Zambia in particular!!
Awamu ya 4 ya nne watu wamekula posho na kusafiri hadi Shenzhen kujifunza jinsi Shenzhen ilivyogeuzwa kuwa a fishing village like Bagamoyo!!
So, what was the idea?! Mega ships kutoka China zingekuwa zinafaulisha mzigo Bagamoyo na mzigo huo kuchukuliwa na meli za kawaida na kusambazwa sehemu zingine za Africa, na mali zingine zingetumia reli kwenda landlocked countries.
Pale Industrial Complex kungetokea mambo mawili!! Hivi sasa Uchina labor cost inapanda kila uchao! Kutokana na hilo, kulikuwa na uwezekano mkubwa Mchina akaifanya Bagamoyo Free Economic zone kama sehemu ya kuzalisha baadhi ya bidhaa zake za kulisha Afrika na maeneo mengine!
Kutokea Bagamoyo, bidhaa hizo zingesafirishwa kwa meli na zingine kwa reli kwenda landlocked countries!!!
Sasa unadai kwamba Kenya hatapata mizigo... man, unajidanganya!!! Salama yetu ni Mchina kurudi Bagamoyo vinginevyo, ile plan ya Bagamoyo anaweza kuihamishia Lamu ambako Kenyatta tangia mwanzo alisema msipojenga, tutajenga wewe!!!
Yule Beberu wangu kwavile sawa na mabeberu wenzake wanaipinga hii miradi ya Uchina, Bagamoyo Port included, moja ya hoja yake ilikuwa eti Bagamoyo Port will be too big for Tanzania's Economy, na kwahiyo Bandari ya Dar es salaam inatosha sana!!
Nilipomuuliza ikiwa na umaskini wetu wote huu pamoja na majirani zetu bado wakati mwingine Bandari ya Dar es salaam huwa inaelemewa! What if uchumi wa Tanzania na majirani zake ukipanda angalau kwa mara mbili tu hasa tukizingatia hata ukipanda mara mbili bado tutakuwa maskini!!
Wanasemaga hivi, One man's poison is another man's meat: Sisi tumegoma, Wakenya washachangamkia dili mapema. Sasa sijui tumlaumu nani ???