Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Ongezeko la kukosa uzalendo lipo sasa na wajinga CCM ndiyo kwanza wamezidi, hiyo mikataba kwani si ingeweza kurekebishwa haraka kama kweli siyo kusaka 10% wakagoma kutoa, miradi yote ya CCM siyo mawazo ya watanzania ndiyo maana haina uzalendo na imejaa 10% za wajanja wachache, hivi visingizio vyako hapa havina mashiko watanzania wa sasa siyo wajinga wanajua sinema zote za CCM wanafahamu hakuna mzalendo huko kila mmoja yupo kwa masilahi yake binafsi ingawa sasa CCM ipo hata kwa masilahi ya Kenya, Tambua kuwa huo mradi magufuli hautaki na kama angeutaka hataka angekaa chini na Wachina na hao waarabu wangerekebisha mikataba na kuwekana sawa mradi uanze mara moja.
Hawa mashujaa wa keyboard ni mzigo. Hivi kwa akili zako za mtandaoni unadhani watu hawajaenda nyuzi 360 na kuona madhara hayo.

Hivi mnadhani nchi inaendeshwa kwa porojo zetu?
 
Jamaa yangu hakuna namna unaweza kutanua ile Bandari ya Dar es salaam kufikia viwango vya bandari kubwa zinazozungumziwa.. Kulia Kigamboni na kushoto Posta katikati ni njia, hakuna namna unaweza kuzuia sand deposit pale na kila siku utakuwa unachimba kina tu kuongeza kina.. Kana inawezekana ibomolewe kigamboni au Posta pawe open sea na sio mlango na hii ni moja ya sababu iliyofanya wale jamaa wakaacha bandari zote wakaitaka Bagamoyo.. Bandari zote za Tanzania zina mlango wakuingilia port maji kupwa na maji kujaa huondoa maji kabisa na kujaza mchanga mara kwa mara na kwa muda fulani itakulazimu kuchimba kuongeza kina..
Ni kweli unalosema kuhusu udogo wa nafasi ya upanuzi hata mkurugenzi wa TPA (D. Kakoko) alishaliongelea hili. Ni kwamba ilitakiwa lile eneo lote mpaka mtoni Kijichi litengwe kwaajili ya bandari na Kakoko alisema kuwaondoa watu itagharimu fedha nyingi za kulipa fidia. Ila hili la kuhusu machanga kurudi wakati wa jioni hilo linaweza kudhibitiwa kwa kuweka "surge barrier'.
Lingine pale ni storage na miundo mbinu ya kuingi na kutoka bandarini hasa kwa heavy loads, ukileta heavy loads nyingi lazima kuwe na foleni kubwa sana maeneo mengi ya Dar hasa njia zinazolink na bandari, Huwa likishuka NYK pale na kuanza kushusha magari lazima uone msongomano wa hatari pale.. Storage bado ndogo sana kwa meli kubwa tatu za kontena 10000 kushusha mzigo pale hapo bado roro kubwa hazijashuka na kuanza kupakua..
Hili la storage teyari wanalifanyia kazi kwa kujenga bandari kavu huko pwani, mizigo ikishushwa itakuwa inapelekwa huko haraka na reli ili kuacha nafasi.
Kuendelea kuijenga Dar es salaam port ni kupoteza fedha tu, ni eneo ambalo tayari sio rafiki labda tuamua DAR ES SALAAM PORT IWE NI KWA RORO TU, MTWARA PORT IWE NI KONTENA PORT, NA TANGA PORT IWE FOR TANKERS.
Hili pia wahusika teyari wanalifanyia kazi, bandari ya Mtwara inapanuliwa ili iweze ku beba mikoa ya kusini na nchi jirani, Tanga vivyo hivyo inafanyiwa ukarabati. Barabara ya kwenda Mbaba bay nayo inatengenezwa ili mizigo kutoka bandari ya Mtwara iende moja kwa moja kupitia barabara hiyo pia baadae wanampango wa kujenga reli.
 
Ongezeko la kukosa uzalendo lipo sasa na wajinga CCM ndiyo kwanza wamezidi, hiyo mikataba kwani si ingeweza kurekebishwa haraka kama kweli siyo kusaka 10% wakagoma kutoa, miradi yote ya CCM siyo mawazo ya watanzania ndiyo maana haina uzalendo na imejaa 10% za wajanja wachache, hivi visingizio vyako hapa havina mashiko watanzania wa sasa siyo wajinga wanajua sinema zote za CCM wanafahamu hakuna mzalendo huko kila mmoja yupo kwa masilahi yake binafsi ingawa sasa CCM ipo hata kwa masilahi ya Kenya, Tambua kuwa huo mradi magufuli hautaki na kama angeutaka hataka angekaa chini na Wachina na hao waarabu wangerekebisha mikataba na kuwekana sawa mradi uanze mara moja.

ZZK kasema haikuwa maktaba bali yalikuw amazungumzo ya hawali, so wangeweza bado kuzungumza na kukubaliana na ndipo mkata usainiwe,
 
Kwakweli Zitto amewandika mazito ila tu sio mtu wakuaminika... lazima kuna kitu nyuma sio kwa maandalizi ya maandishi hayo, Zitto asingekua mnafiki angekua the best presidential material wa nchi hi, anaupeo mwingi
Zitto shida yake ni hiyo. Amepoteza kila adimu kwenye maisha, trust. Nani anayemuamini? Nyuma ya kila anachofanya ana sababu zake nyingi binafsi kuliko yale anayosema.
Very interesting indeed!
 
Watu wanaotumia muda mwingi kuwaza namna ya kuhujumu upinzani mambo kama haya watayaweza wapi?

Eti hii ndio serikali iliyojaa madokta na maprofesa!!!
 
Nimesoma bandiko lako Zitto, lakini umeshindwa kumuelewa Rais Magufuli.

Ni kwamba Mh Magufuli hajakataa maradi wa bandari ya Bagamoyo. Alichokikataa Magufuli ni mkataba haujakaa kwa maslahi ya watanzania. Umekaa kwa maslahi ya wanaoujenga. Kitu ambacho hata sisi watanzania tunamuunga mkono kama mkataba umekaa kiunyonyaji hauna maslahi kwetu kuna haja gani kuendelea nao?

Mradi gani huo ambao serikali haitapata kodi, mradi gani huo ambao kama nchi haturuhusiwi kuendeleza au kujenga bandari nyingine yoyote kwa karne nzima hivi tumelogwa au?

Hapana tuendeleze tu bandari yetu ya Dar, Tanga na nyinginezo taratibu kwa maslahi yetu, badala ya kuwa na miradi feki isiyo na tija kwa nchi.

Huu ni ukoloni kama ukoloni mwingine tu, kama tutauza nchi kirahisi hivi. Kwa hili tumuunge mkono Rais Magufuli kwa maslahi ya nchi yetu. Huu ukoloni mamboleo tuukatae, chochote ambacho hakina maslahi kwetu tukatae.., hivyo hivyo watatuelewa tu.

Mambo ya kuuza rasilimali zetu tunajikuta tu watumwa hapana, hatutaki ya Zambia hapa..

Zitto kwa hii hoja yako itakushushia heshima na malengo yako ya mbeleni. Washauri wenye huo mradi uwe kwa maslahi ya wote. Kama haipo win win hiyo siyo biashara tena ni unyonyaji.
Unazungumzia mkataba gani ambao ulikuwa umeingiwa?
 
Namuelewa Zito Kabwe, ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza, lakini mimi namuona kama mwanasiasa asiyeaminika! Hubadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika
 
Ni kweli unalosema kuhusu udogo wa nafasi ya upanuzi hata mkurugenzi wa TPA (D. Kakoko) alishaliongelea hili. Ni kwamba ilitakiwa lile eneo lote mpaka mtoni Kijichi litengwe kwaajili ya bandari na Kakoko alisema kuwaondoa watu itagharimu fedha nyingi za kulipa fidia. Ila hili la kuhusu machanga kurudi wakati wa jioni hilo linaweza kudhibitiwa kwa kuweka "surge barrier'.

Mkuu huoni hapo tayari kuna limitations tayari na gharama kubwa kuifanya bandari kuweza kupokea hizo meli kubwa, Congestion ya meli bado tutashindwa kuiondoa baadala yake tutakuwa tumeipunguza hasa pale itakapofikia point ya kuwa na flow kubwa ya meli (japo siamini kama hiyo flow kubwa itakuwepo wakati bado production yetu ni very low). "surge barrier" bado ni issue kwa maana ya gharama na sina uhakika kama itawork kulingana na eneo lenyewe.

Kama waziri ameshakubari pale ni pafinyu baadala ya kutupa hela kwanini tusiangalie option nyingine, Hizo gharama za yote hayo na mengine uliyoonyesha kwanini tusikae na mchina mezani tukashare cost?? na masharti yakapungua na ujenzi ukawa na shareholder watatu GOVT, CHINESE NA ARABS with our 30%shares na tukaweka hela kabisa na sio free shares, Dar es salaam port ikawa just as backup port lakini pia ikatumiwa na fishing trawler's
Hili la storage teyari wanalifanyia kazi kwa kujenga bandari kavu huko pwani, mizigo ikishushwa itakuwa inapelekwa huko haraka na reli ili kuacha nafasi.

Point yangu ni ile ile, haya magharama yote yangechanganywa tukawa na hela yakutosha tutakaa na Mchina tukawa na shares zetu hata 30% na ARABS na CHINESE wakagawana hiyo 75% na masharti yakapungua na hiyo package yao ikaja kama ilivyo huku sisi tukineemeka kwenye kodi, ajira kwa watu wetu, miji kujengeka na kutanuka, bado tuna gawio kwenye 30% shares na multiplying effect itaenda mbali zaidi mikoa na mikoa na Tanzania inaweza kuwa Hub ya chinese business East africa na hizi land locked zote.


Hili pia wahusika teyari wanalifanyia kazi, bandari ya Mtwara inapanuliwa ili iweze ku beba mikoa ya kusini na nchi jirani, Tanga vivyo hivyo inafanyiwa ukarabati. Barabara ya kwenda Mbaba bay nayo inatengenezwa ili mizigo kutoka bandari ya Mtwara iende moja kwa moja kupitia barabara hiyo pia baadae wanampango wa kujenga reli.
[/QUOTE]


Tanga na Mtwara bado linazungumzika kupitia pointi zangu za juu na ukiangalia fikra za hawa wawekezeaji, Kwenye makubaliano ya Bagamoyo port tunaweza kuwabana wakaturuhusu tukasafirisha Korosho,Makaa ya mawe na graphite kupitia Mtwara port, lakini tukiweka reli ile old gauge kuconnect Mtwara na Songea na reli ya Tazara Ili zile shunting za meli ndogo kutoka Bagamoyo zitakuwa zinapeleka mizigo pale kwa ajili ya Songea na Nyanda za juu hata Malawi.

Tukitumia hizi fursa vizuri na kuchanga karata zetu vizuri tukizingatia kuboresha maisha ya watu wetu tunaweza kupiga hatua kwa haraka sana.
 
haya ngoja tusikilize na upande mwengine ila ile safari ya Kenyata kule Chato hata mimi naanza kuamini Jiwe anatumika na Kenya
Nalog off
 
Moshi wa Ruangwa umeisha? maana sidhani hao wamiliki wa huo moshi watakubali afike 2035 huku Bashite kipindi hicho ni waziri mkuu
Hahaha mkuu una stress sana na Magu
 
Kwanini Serikali isiifanye Kigamboni kuwa mji wa Bandari na Viwanda kwa kupanua Bandari ya Dar es Salaam tukaachana na hizi kelele za Bagamoyo?
 
MH. ZITO KABWE, hongera sana kwa ufafanuzi wako japo usiwe na wivu kwa sababu Kenya inazidi kutusua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kuna siku nilisema kwamba Kenya ni nchi yenye rasilimali chache ila inaoongozwa na watu wenye akili kubwa sana. Natumai kupitia huu uzi wako umewathibitishia watanzania kwamba Kenya iko mbele ya Tanzania kwa kila kitu i.e mentally, economically, politically and socially.
 
Bado don't see any new substance. It's just an obvious stuff.
 
MH. ZITO KABWE, hongera sana kwa ufafanuzi wako japo usiwe na wivu kwa sababu Kenya inazidi kutusua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kuna siku nilisema kwamba Kenya ni nchi yenye rasilimali chache ila inaoongozwa na watu wenye akili kubwa sana. Natumai kupitia huu uzi wako umewathibitishia watanzania kwamba Kenya iko mbele ya Tanzania kwa kila kitu i.e mentally, economically, politically and socially.

Do you know what is behind the LAPSSET contract? Kenyans have no clear picture of how much the project will cost and how long it will take to fund the project.
 
Hawa mashujaa wa keyboard ni mzigo. Hivi kwa akili zako za mtandaoni unadhani watu hawajaenda nyuzi 360 na kuona madhara hayo.

Hivi mnadhani nchi inaendeshwa kwa porojo zetu?
Wewe na wenzako porojo zenu zimeleta maendeleo yapi? Miaka 50 Nchi haina maendeleo wewe shujaa wa keyboard Mbona humwambii magufuli kuwa nyerere alinunua Ndege 14 na hazikuleta maendeleo? Tanzania ni Nchi yenye rasilimali nyingi kuliko mataifa kibao Duniani lakini chini ya CCM imekuwa Nchi masikini wa kutupwa, hutukupaswa kuhubiri flyover sasa ni vitu vilitakiwa viwepo Nchini siku nyingi lakini kwa kuwa CCM ni chukua chako mapema na CCM ni ile ile endeleeni kuitafuna Nchi mpaka mwisho wa Dunia.
 
MH. ZITO KABWE, hongera sana kwa ufafanuzi wako japo usiwe na wivu kwa sababu Kenya inazidi kutusua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kuna siku nilisema kwamba Kenya ni nchi yenye rasilimali chache ila inaoongozwa na watu wenye akili kubwa sana. Natumai kupitia huu uzi wako umewathibitishia watanzania kwamba Kenya iko mbele ya Tanzania kwa kila kitu i.e mentally, economically, politically and socially.

Wakenya ni wajanja hata Bandari Mombasa kutoa mzigo ni jengo moja tu kila kitu kimepangiliwa vizuri siyo lazima kuwa na wakala wakati wa kutoa mzigo wako.

Lakini Bandari ya Dsm hawana mpangilio kuna usumbufu mwingi mara hakuna Network ndiyo maana wageni hawaitaki Bandari ya Dsm, mabasi vyombo vya usafiri ni 24 hrs wana viwanda vingi, Serikali inaheshimu mahakama na vyama vya upinzani kuna utendaji mzuri kimfumo kwa ujumla
 
Kwanini Serikali isiifanye Kigamboni kuwa mji wa Bandari na Viwanda kwa kupanua Bandari ya Dar es Salaam tukaachana na hizi kelele za Bagamoyo?

Kile kichochoro cha huko feri ndiyo Tatizo na kukipanua kile ni gharama kubwa sana ni sawa na kujenga Bandari ingine mpya kubwa
 
Dah hapa ndo naamini watanzania tuna minyoo kichwani.

1. Hivi wachina wajenge afu wasilipe kodi hata cent lakini wawe huru kufanya biashara.
2. Wakae kwenye ardhi yetu miaka 99
3. Haturuhusiwi kuendeleza bandari yeyote zilizopo
4. Wasimamie wao for the whole period kweli. Ndugu zangu hawa hawa


Wanapinga miradi kama
1. Stiglers gorge
2. Reli
3. Ndege
I ambayo hii unakwenda kwa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.
Sijui watanzania tunataka nini


Sisi hatukuwa tayari kupata uhuru au tunatakiwa kutawaliwa kidikteta for while hadi hadi tupate akili
Nasubiri Bandari Kubwa ya Lamu izuie Bandari Ndogo za Dar na Mombasa: Namna Maarifa Madogo Yanavyoiua Bandari ya Bagamoyo na Kuifaidisha Kenya

Kumekuwa na mijadala mikali kuhusu Mradi wa Eneo la Kiuchumi la Bagamoyo. Mjadala huo wenye malumbano ya kurushiana shutuma umekuwa mjadala mbovu sana kwenye jambo nyeti la kiuchumi Kama vile Mradi wa Bagamoyo SEZ. Wanaounga mkono wanaona fursa za maendeleo katika Mradi, wanaopinga wakiona hasara nchi itapata. Wanaopinga wanawashutumu wanaounga mkono kuwa wanataka kuuza Nchi.

Kundi la wanaopinga linaongozwa na Rais John Magufuli, Spika wa Bunge ndg. Ndugai mwanzoni alikuwa kinara wa kuunga mkono Mradi kwa hoja nzito zenye nguvu. Lakini baadaye alisalimu amri kwa hoja dhaifu sana na hivyo kujisalimisha kwa Rais Magufuli kwenye hoja nyepesi zilizojaa woga na zisizo na tafakuri yenye mwono mpana wa Uchumi wa Jiografia.

Sasa inadhihirika kuwa Rais Magufuli anatumika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi ya Jamhuri ya Kenya. Nitafafanua.

Kila nchi ina picha kubwa katika mambo inayotaka kuwa (a grand vision). Picha hiyo kubwa inapaswa kuzingatia mazingira ya nchi husika (context) na namna ya kuyatumia mazingira hayo kufikia hiyo picha kubwa. Tanzania na Kenya ni nchi ndugu ndani ya familia ya Afrika Mashariki. Nchi hizi pia ni Nchi shindani kiuchumi. Ni nchi pekee za Afrika Mashariki ambazo zote zina pwani ya Bahari (access to the sea). Lakini Tanzania ina Pwani ndefu zaidi kuliko Kenya na hivyo kuipa fursa kubwa zaidi.

Nchi zote mbili zinapakana na nchi ambazo hazina pwani. Kenya inapakana na Ethiopia, Sudani Kusini na Uganda. Tanzania inapakana na Uganda, Malawi, Zambia, Kongo DRC, Burundi na Rwanda. Tanzania ina fursa zaidi kuliko Kenya kutokana kupakana na Nchi nyingi zaidi. Kenya kwa muda mrefu imekuwa ikishika biashara ya nchi inazopakana nazo na isizopakana nazo pia. Tanzania imekuwa ikisuasua kufaidika na nafasi yake kijiografia katika kushika biashara ya eneo hili la maziwa makuu. Miji inayoongoza ushindani wa Biashara wa nchi hizi ndugu ni Mombasa na Dar es Salaam. Ni miji ya Bandari, yote ikitawaliwa na Sultan wa Zanzibar wakati fulani na baadaye wababe wa Vita za Dunia Uingereza na Ujerumani kugawana miji hiyo - Mombasa kwa Waingereza na Dar es Salaam kwa Wajerumani.

Hata hivyo Bandari zote hizi 2 zimekuwa ni Bandari za mizigo inayopita (transit goods) kwa kuwa vina vyake ni vidogo hivyo kuweza kupokea Meli ndogo tu. Meli kubwa kutoka China hufika Singapore na kupakua mizigo kuweka kwenye Meli ndogo zinazokuja kutia nanga Mombasa au Dar es Salaam. Meli kubwa kutoka Ulaya hushusha mizigo kwa Meli ndogo huko Bandari ya Salalah, Oman. Ili kuwezesha Meli kubwa kufika Pwani ya Afrika Mashariki, Nchi ndugu za Kenya na Tanzania zikaanza kuwaza na kuwazua miradi ya kufanya ili kuwa Kituo Kikubwa cha Biashara ya Bahari Eneo la Afrika Mashariki (transshipment hub). Mzozo wa kimkakati ulianzia hapo katika ya Nchi rafiki Kenya na Tanzania.

Jamhuri ya Kenya ilitumia diplomasia ya Hali ya Juu kuunganisha Nchi za Rwanda, Uganda, Ethiopia na Sudan ya Kusini kwenye Mradi wa picha kubwa wa Bandari ya Lamu. Ikazaliwa kinachoitwa ‘Northern Corridor’. Tanzania ikatengwa katika Afrika Mashariki (EAC) kikaanzishwa kitu kinaitwa ‘Coalition of the Willing’. Kenya wakazindua kwa fujo Mradi wa Bandari ya Lamu ili kuwa Bandari ya Meli kubwa za Afrika Mashariki. Marais wa nchi zote za coalition of the willing za EAC na nje ya EAC walikusanyika huko Lamu kuanzisha Mradi huo.

Uongozi wa Awamu ya Nne wa Tanzania chini ya Rais Jakaya M Kikwete nao wakaamua kutumia mtaji mkubwa wa diplomasia aliouacha Mwalimu Nyerere kujibu mapigo. Mapigo ya Lamu ni Bagamoyo. Rais Kikwete akafanikiwa kuwashawishi Rais Xi Jinping wa China na Sultan Qabos Bin Said wa Oman kuisadia Tanzania katika mpambano wa kuishika Bahari ya Hindi. China na Oman wakakubali kuanzisha Mradi mkubwa wa kituo cha Meli katika Afrika na Eneo Huru la Uchumi pale Bagamoyo. Mradi wenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 10.

Rais Jakaya Kikwete alifanya kosa analolijutia, naamini, mpaka sasa. Aliondoka madarakani bila kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi. Makosa haya yanaigharimu Nchi sasa kwani ushindi wa kuimiliki na kuitawala Biashara ya Bahari ya Hindi upande wa Magharibi umekwenda Kenya bila hata risasi moja kurushwa. Mradi wa Bagamoyo umehujumiwa. Umekufa.

Baada ya Utawala wa Awamu ya Tano kuingia madarakani waliokuwa ‘coalition of the willing’ wakajisogeza karibu. Rwanda ikatangaza kuegemea Central Corridor. Tanzania ikabadili mpango wake wa Kujenga Reli kutoka Dar es Salaam kupitia Uvinza mpaka Musongati nchini Burundi na sasa ikaamua kuielekeza reli Isaka kwenda Rwanda. Badala ya Uvinza kuwa Kituo cha Biashara na Mizigo kwa Nchi za Maziwa Makuu, Sasa itakuwa Kigali, Rwanda.

Rwanda tayari imefungua Kigali Logistics Platform na Bandari huru ya Masaka (Kigali) yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 35. Bandari hiyo itaendeshwa na Kampuni kubwa duniani ya kuendesha Bandari iitwayo Dubai World. Kwa mkakati huu Rwanda itabeba mzigo wote kutoka DRC na kuhudumiwa kupitia Kigali, na hivyo Uvinza (Kigoma) kujifia kwa kukosa Biashara. Tanzania imepoteza kwa Rwanda.

Kenya kwa upande wake ilianza vibaya mahusiano yake na Tanzania ya utawala mpya. Katika hali ya kuweka maslahi ya nchi yao mbele wanasiasa wa Kenya waliamua kuungana katika kile kinachoitwa ‘handshake’, na ndugu Raila Amolo Odinga akapewa rasmi kazi ya kuhakikisha anasimamia hiyo diplomasia ya Kenya inafanikiwa. Propaganda kali dhidi ya Bagamoyo zikaanza na safari za Raila kuja kuonana na Magufuli zikawa nyingi pengine wakikutana Chato na pengine kwa Siri.

Baadhi ya watendaji wakanyweshwa sumu za ubovu wa mkataba wa Mradi wa Bagamoyo (ambapo hapakuwepo na Mkataba). Serikali ya Awamu ya Tano ikatamka rasmi kuwa hawataki Mradi ule kwa sababu za kitoto kabisa, kwani walitumia nyaraka za majadiliano na Mwekezaji. Spika wa Bunge alipoinua sauti yake akanyamazishwa. Vyombo vya Habari vikalishwa sumu na Mradi ukanuka. Msemaji wa Mradi wa Bagamoyo siku zote ni Wizara ya Viwanda na Biashara, lakini ghafla Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) ndio ikawa ndio Msemaji badala ya Wizara. Na baadhi ya Watendaji wa Serikali wenye mwono wa mbali walipotoa mawazo yao wakaondolewa kwenye nafasi zao.

Baada ya mradi wa Bagamoyo kuuawa, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akapewa tuzo na nchi yake kwa kuifanya Kenya kuwa mtawala wa Bahari ya Hindi, tuzo ya ‘Maritime Champion of the Indian Ocean’. Na Rais Kenyatta akawa rafiki ya karibu ya Rais Magufuli. Nchi yetu ikiwa imepoteza miaka minne sasa bila kutekeleza mradi wa Bagamoyo.

Ujenzi wa Bandari yenye kina kirefu ya Lamu sasa kuzinduliwa rasmi Novemba, 2019. Sasa Lamu itapokea Meli kubwa za 4th Generation kama vile Suezmax, Neo-Panamax na Chinamax. Mizigo kutoka Meli kubwa itashushwa Lamu na kupakiwa kwenye Meli ndogo kuja Bandari ya Dar es Salaam na kwenda Bandari nyengine za Afrika kama Beira na Durban. Hii ndio kazi ilikuwa ifanywe na Bandari ya Bagamoyo - Mradi ambao umehujumiwa. Pia Kenya wameamua kuchukua mpango mzima wa Bagamoyo na kuutekeleza Lamu kwa kuanzisha Eneo Maalumu la Uchumi. Hapo kabla ilikuwa iwe Lamu Port Pekee.

Watawala wetu wameonyesha uwezo mdogo sana wa kung’amua mambo na kujikuta kuwa sehemu ya Hujuma kwa Nchi yetu. Faida ya kijiografia ya nchi yetu ambayo Mungu alitupa tumeipoteza. Baadhi ya watu wanashangilia ujinga huu wa kiuchumi ambao tumeufanya bila kujua. Shida kubwa ya watu wenye mamlaka ya Dola katika nchi yetu hawasomi kujiongezea MAARIFA ili kuepuka hujuma dhidi ya nchi yetu, hujuma ambazo zitaathiri vizazi na vizazi.

Tumepoteza fursa ya nchi kwa sababu za kitoto, zisizo na maana na za kipropaganda tu. Kuendesha bandari miaka 99 mara tunataka miaka 33 haiwezi kuwa sababu kwa mtu mwenye akili timamu wakati Mradi ni Joint Venture na Serikali ni mbia mwenye hisa zinazotokana na ardhi yake. Kuna mwekezaji atabeba ardhi ya Tanzania kuipeleka China au Oman? Eti Bagamoyo itaua Bandari ya Dar es Salaam, kwa hiyo Ujenzi wa Bandari ya Lamu utaua Bandari ya Mombasa? Nasubiri kuona Bandari ya Dar ikifa kwa sababu ya ujenzi wa Bandari ya Lamu.

Biashara ya Bandari ya Bagamoyo ingekuwa kwa Meli kubwa kuleta mizigo na Meli ndogo kuja kubeba kupeleka Bandari za Afrika nzima kazi ambayo haifanywi na Dar es Salaam na wala haitaweza kufanywa kwa sababu Eneo la Bandari ya Dar ni dogo. Kazi ambayo sasa itafanywa na Bandari ya Lamu.

Hujuma hii kwa Jamhuri ya Muungano haipaswi kupita bila kulipiwa. Rais Magufuli na Serikali yake wanapaswa kulipa gharama ya hujuma hii kwa Nchi yetu. Wasipolipia watakuja Viongozi wengine kuhujumu nchi yetu kama hawa. Wakiadhibiwa itakuwa somo kwa wengine. Kwa uelewa mpana kuhusu Uchumi wa Bahari soma Gazeti la The East African la October 26 - November 1, 2019:
Inside Kenya’s plan to rule EA Coast.



Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

Mbunge - Kigoma Mjini

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo

Oktoba 28, 2019
 
Back
Top Bottom