Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Ukisoma ramani ya kwanza ya Belt-Road Initiative utaona kwamba njia ni Pakistani hadi Lamu na siyo Bagamoyo. Hivyo ina maana Uchina alikuwa na mpango wa kujenga Mega-Port Lamu na siyo Bagamoyo, lakini Jakaya Kikwete akafanya yake.

Wanasemaga hivi, One man's poison is another man's meat: Sisi tumegoma, Wakenya washachangamkia dili mapema. Sasa sijui tumlaumu nani ???
 

Suala si kujenga tu bandari, bali masharti ya uwekezaji huo. Tusingekuwa makini tungeenda kama wenzetu wa Zambia na Sri Lanka walivyofikia. Walifurahia bandari, lakini kilichotokea ni majuto, hawakuweza kulipia deni na kilichotokea waChina ikabidi wachukue bandari kwa muda wa miaka 100. Yaani wachina wana maarifa kuliko wakoloni waliokutana na akina Chief Mangungo.
 
Swala la mkataba ni tata naamini hata ww hujauona na kuusoma ili kusiwe na lawama ni bora mkataba huo ukapelekwa bungeni uchambuliwe ili kila mta aelewe ni nn kilichomo kuliko kuambiwa tu ni nani kati yao yupo sahihi kutokana na mkataba? Weka mambo hadharani kila mtu achambue
 
Labor Cost ya Uchina ni ya bei ya chini duniani, lakini Afrika ndiyo chini zaidi. Wanasema Technician au Fundi Mchundo wa Tanzania, Kenya na Ethiopia mwenye kiwango kilekile na yule wa Uchina, analipwa mshahara mdogo mara kumi ya yule wa Uchina.

Gharama za uzalishaji zinaanza kumzidia Uchina maana watu wa kipato cha kati wameanza kuwa wengi. Sehemu rahisi ya kukimbilia ni Afrika ambako ndiyo kuna Cheap Labor. Sasa wahafidhina watakwambia Wachina watakimbilia Afrika ili kukwepa hilo.

Lakini wanasahau jambo la msingi kwamba idadi ya watu wa Uchina inazeeka au The Population is Aging na hivyo nguvu kazi kubwa ya vijana wa Uchina itahitajika kule kwao zaidi ya kuwaleta huku Afrika. Hapa Afrika watafanya waafrika wenyewe ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Sasa sijui kwanini huwa tunaangalia mambo ya miaka 10 au 20 mbele tu. Tunakwama wapi......???
 
Mkuu unataka kusema kwamba Lamu nayo itaivuruga bandari ya Mombasa si ndiyo ???

Hivi Chige umewahi kusikia nini kilitokea wakati reli ya TAZARA inajengwa: Unajua kampeni iliyopigwa na Marekani ili kuzuia ile kitu isijengwe ??? Basi kuna injinia mchina alikuwa ni mzee anasimulia hadi walivyopigana ngumi na wamarekani wakati wanatengeneza reli ile.
 
Kikwete hakusita kusaini bali alikuwa akisubiria upembuzi yakinifu ukamilike vizuri na ukaja kukamilika akiwa katoka ikulu na sasa aliyepo ikulu yeye kawapa Dili Bandari ya Lamu hataki meli kubwa kuja Tanzania


Huu?

 
Kwani walikataa kufanya mazungumzo upya?

Alichotaka bwana mkubwa ni yeye kuleta wawekezaji wengine ili tu achukue ujiko na si kitu kingine.
 
Bandari ya Bagamoyo haijengwi kwa mkopo kama Sri-Lanka na Zambia. Hela zote za mradi wanatoa Uchina na Oman: hapa mnaogopa nini ???
 
Hoja nzima ya ZZK inamalizwa na hoja rahisi kwamba tukiamua kuijenga bandari ya Bagamoyo hata leo kwa mkataba unaofaa kwa maslahi ya umma shida itakua wapi? Kwa position yetu kijiografia tutaiua hiyo bandari ya Lamu haraka sana
 
Zitto asitulishe matango pori. Asijifanye ana uchungu sana na nchi wakati ni mchumia tumbo. Anamjua anayemtumikia. Apeleke njaa zake huko. Bandari ya Bagamoyo tutaijenga wenyewe siku tukiamua au siku tukimpata mbia ambaye na sisi tutanufaika. Zitto siyo mchumi pekee nchi hii. Nchi hii ina wachumi wengi tena mahiri kuliko yeye na njaa zake.
 
Story ndeefu wkt lengo la thread yako ni hapa tu ulipoandika.

'Tanzania ikabadili mpango wake wa Kujenga Reli kutoka Dar es Salaam kupitia Uvinza mpaka Musongati nchini Burundi'

Reli kutopitishwa Kigoma imekua Nongwa.
Umetisha...
 
Bandari ya Bagamoyo haijengwi kwa mkopo kama Sri-Lanka na Zambia. Hela zote za mradi wanatoa Uchina na Oman: hapa mnaogopa nini ???
Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Ati fedha ni za wachina na wa omani sisi tusiogepe? Are you serious pal? Something very wrong is happening in your brain!
 
Zitto asitulishe matango pori. Asijefanye ana uchungu sana na nchi wakati ni mchimia tumbo. Anamjua anayemtumikia. Apeleke njaa zake huko. Bandari ya Bagamoyo tutaijenga wenyewe siku tukikaa sawa, lakini siyo kwa maslahi ya wache na Wachina.

Magufuli amesamehe Trilion 424 (Dola bilion 190) kwa ACACIA ambazo thamani yake ni kubwa kiasi kwamba tungeweza kujenga bandari ya bagamoyo bila kukopa wala kupata msaada wa nchi yoyote na kisha mapesa mengi tu yakabaki
 
Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Ati fedha ni za wachina na wa omani sisi tusiogepe? Are you serious pal? Something very wrong is happening in your brain!

Mkuu point ya jamaa ni hii, Mchina na Muoman wanajenga everything kwa gharama zao.. Operation na usimamizi wa kila kitu ni wao ili warejeshe gharama zao kwa hiyo 90yrs baada ya hapo wanasurrender kwetu tunaendelea wenyewe... Zambia na Sri-lanka walikopa wajenge kwa maana ya kulipa, SGR ya Kenya anaiendesha Mchina kurudisha gharama zake nafikiri pia Kenya hawakukopa..
 
Dr. Mpango waziri wa Fedha alikuwa mkuu wa Tume ya Mipango wakati wa JK; bila shaka alikuwa sehemu ya walimshauro JK asiwe "fasta" kusaini

Philip Mango hakuwa na guts kumshauri Mkwere asisaini ule mkataba; mkwere ule mradi ndio ilikuwa lala salama yake ya kuendeleza kwao hivyo asingekubali kuacha kusaini!! Hii ndio ilikuwa kati ya ile mikataba alipokuwa anasaini MOUs hata bila kusoma hivyo bila shaka ulipofika wakati wa implementation machale yalimcheza.
 
Nafikili uwekezaji kwenye umeme ni jmabo la maana sana,,Huwezi kuwa na viwanda vikubwa vya Chuma bila umeme wa Uhakika,
 
Wewe unaambiwa bandari zenye kupokea meli kubwa,sio bandari kubwa.
Ki ukweli nchi hii tuna safari ndefu mno maana vilaza walio soma wapo wengi mno,
Akina zidumu fikra za mwalimu hata kama si sahihi.
 
Mkuu sasa si bora kukopa kuliko kujitoa ufahamu namna hii? Hapa ni kama umeuza moja kwa moja. Sasa kulikuwa na mantiki gani ya kudai uhuru na kuwafukuza wakoloni wakati nao walikuwa wanajenga na kuendesha nchi yetu? Huoni Afrika Kusini ilivyojengwa? Lakini pamoja na kujengwa kote wananchi wake walikuwa hawana raha. Kwa nini tujiweke kwenye hali ngumu kama hii wakati kuna mambo mengi basic tunaweza kufanya yakanufaisha wananchi zaidi? Waje tuwekeze kwenye kilimo. Mazao yakivunwa tunagawana kulingana na makubaliano.
 
Duu, umepewa mfano wa HONGKONG, ilivyokuwa chini ya UINGEREZA kwa miaka 100, Leo imerudi CHINA na kuinufaisha China Kimaendeleo.
 
Natamani Bandari hii, ingelikuwepo Zanzibar kitambo lakini Tanganyika wakatuwekea kauzibe,
Eti nduguzetu wa damu.

Hapa ndo ninapoona kuwa CCM ni adui si wa Tanzania bara tuu bali Zanzibar pia.
Maana Inatumiwa na majirani kwa maslahi ya wengine si Tanzania.

Tumejitolea sana Majeshi yetu kuilinda serikali ya Kongo, sijui kwa maslahi ya nani? Majeneza kila mara yanarudi Nyumbani.

Msumbiji, Angola na sasa Rwanda inapaa kwa mgongo wetu na Kenya ndo hiyo.
Sijui hawa jamaa wanatuwekea Maraisi mamluki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…