Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Wewe umejikita kumshambulia Zitto, hushambulii hoja alizoleta hapa na kuzinyoosha tuone palipopinda.

Kiufupi ni kwamba unatafuta njia ya kumnyamazisha, hata kama hutambui kwamba unafanya yaleyale yanayofanywa na serikali ya kuwanyamazisha wasiokubaliana na mambo yanayofanyika huko.

Kwako pengine unaona kila lifanywalo huko, au taarifa yoyote itolewayo huko haistahili kuhojiwa. Tumekuwa na makundi ya watu hawa sasa - wanaohoji chochote kitokacho serikalini, au kukubali chochote kisemwacho kutoka serikalini. Juhudi kubwa zinafanyika kuwaziba midomo hawa wanaohoji. Na hii ndio kazi unayoifanya hapa.
 
Amesema soma gazeti la East Africa la October 26 na November 1st
 

Anapenda kujimwambafy au siyo!
 
Zitto ni kinara wa "STATE CAPTURE"

AMetumika na akina ACACIA, akatumika na akina SCBHK -STANDARD CHARTERED BANK HONGKONG na sasa WACHINA WA BANDARI YA BAGAMOYO (ambao ndio haohao wa mradi wa makaa ya mawe mchuchuma na liganga)

"Mr. STATE CAPTURE "
Hayo yako baki nayo wewe mwenyewe endelea kukariri huko kwako, lakini wengine sie tunaangalia Bagamoyo hatutaki kufanya kazi kwa hizo history zako, umekula pesa za kenya umeshiba mpaka huna hata Aibu
 
Hakusamehe bali wazungu wamempa kitu kidogo chini ya uvungu kazuga kusamehe, wanakula peke yao huku wakihubiri uzalendo hakuna na Noah wala nini, hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
Mradi wa Bagamoyo una faida kubwa kuliko miradi yote ya magufuli kaamua kuacha huo mradi kwa kuhofia kufunika miradi yake yote
 
@="Lord denning,
Washauri wa Magufuli wanachojua kumshauri ni kudhoofisha vyama vya upinzani pekee mengine hawajui kitu.

Mombasa wapo Mbali hata mfumo wao wa kutoa mizigo kukabidhi kwa wahusika upo vizuri na kwa haraka ni tofauti na mfumo wa Bandari ya Dar es salam ambao ni wa hovyo hovyo na usumbufu mwingi sana.
 
Kuna wakati inakuwa vigumu sana kwa hoja za Mh Zitto kueleweka, au ndio kusema anatafuta umaarufu wa bei rahisi kwa kudonoa hoja kubwa. Mradi wa Bagamoyo ni sawasawa na alichosema mwalimu, "mtu mwenye akili anakwambia kitu cha kijinga, halafu anasubiri kuona mwenye akili akubali huo ujinga, na yeye achekelee" . Sasa Zitto naamini ni mtu mwenye akili anayetaka kukubali ujinga.

Mh. please make yourself familiar with issues before commenting on them, some of us do have respect on you. You need to dig deep and understand how messy the Lamu deal is, and how smart was Serikali ya Tanzania in refusing to eat matango pori. Kuna wakati tutakuwa tunakosea na tutakuwa tunauza nchi yetu kwa kupata umaarufu wa kijinga kwa sababu za siasa. Wakenya watalia sana na miradi yao hiyo wanayoita mikubwa.
 
Serikali iseme uongo kwa mradi mkubwa kama ili ipate faida gani?

Mradi kama ungekuwa mzuri kihivyo ungeisaidia Tanzania, Serikali kupata a lot credit and goodwill and money.

Kwahiyo unafikiri wote ni wajinga walioko serikalini?
Kwani wote serikalini ndiyo wamekataa Bandari ya Bagamoyo? wengi wanaitaka Bandari hiyo lakini mmoja tu magufuli haitaki mpaka China wakae nae chini kama kampuni za madini ashibe kwanza ndipo mengine yafuate
 
Zito haangalii masilahi binafsi kwani pesa bilion 56 zilizolipwa fidia kule Bagamoyo ni pesa za walipa kodi na hizo pesa zikipotea bure anayeumia ni Mtanzania mlipa kodi, kama ni masilahi binafsi atakuwa nayo magufuli anayeithamini Bandari ya Lamu kenya mpaka akagawa Tausi kwa Rais kenyata, hili la Bandari ya Bagamoyo Zitto Kabwe yupo sahihi watanzania walio na Upeo wanamuelewa vizuri lakini watetezi wa CCM watukuza Zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM lazima watampiga hata bila kuwa na Hoja za msingi.
 
Serikali iseme uongo kwa mradi mkubwa kama ili ipate faida gani?

Mradi kama ungekuwa mzuri kihivyo ungeisaidia Tanzania, Serikali kupata a lot credit and goodwill and money.

Kwahiyo unafikiri wote ni wajinga walioko serikalini?
Walivyosema makinikia iliyokuwapo kwenye kontena 270 pale bandarini dhahabu yake inaweza kujaa kwenye lori la tani 7 walikuwa na maana gani?!

Waliposema Acacia tunawadai Trillion 425 walikuwa na maana gani?

Profesa Mruma na timu yake walipotoa takwimu zilizoashiria Tanzania ndie mzalishaji mkubwa wa dhahabu Afrika na tupo kwenye Top 3 duniani walikuwa na maana gani?

Magu aliposema ana ushahidi kwamba polisi waliokuwa wanasindikiza dhahabu ya wizi walikula rushwa ya mamilioni lakini miezi 6 baadae akatangaza wale polisi waachiwe huru na warudishwe kazini mara moja alikuwa na maana gani?!

Kabudi aliposema Azory Gwanda disappeared and died, na baadae akasema amenukuliwa vibaya alikuwa na maana gani?!

Wanapotangaza kwamba tunajenga miradi mikubwa kwa pesa za ndani huku deni la taifa likiendelea kupaa wana maana gani?!
 
Kama hujui kinachoongelewa bora ukanyamaza kuliko kuandika viroja! Eti faida baada ya miaka 99... dah! Yaani nyie watu ndo maana mnadanganywa kirahisi sana kwa sababu hata mambo madogo yanawashinda!
Sasa tutabishana na serikali? Wao ndo wapo kwenye majadiliano na wajitetea kwa vipengele ivyo vya miaka 99, na bandari za dar tanga, mtwara tusizitumie
 
Atuwezi kurudia makosa ya mkapa
 
Dah mjadala mtamu kweli, sisi huku pembeni tunasoma kimya kimya tunapanua uelewa
 
Dah mjadala mtamu kweli, sisi huku pembeni tunasoma kimya kimya tunapanua uelewa
Mjue pia kuwa mradi wa Bandari ya Bagamoyo wao wapo tayari kwa majadiliana ingawa kwa kuwa Bandari ya Lamu kenya wamemteka magufuli kimawazo ni vigumu awakubalie wachina na yupo tayari kupoteza bilion 56 zilizolipwa kama fidia kwa wananchi wahame kupisha ujenzi hana uchungu na hiyo pesa ya walipa kodi.
 
Man, jisikie aibu bhana... yaani unataka kutoa kongole hadi kwa hili!!!Though I don't know you physically but I still do know you're not this low!!

Kwamba eti mimi ni nyumbu mfuata mkumbo... thubutu! More often than not, huwa naandika kwa kutumia my own judgement!! Ni vile tu mimi ni mvivu kuanzisha threads! Ripoti ya Mruma kwa mfano, hiki ndicho niliandika:-
Utaona nilii-doubt Ripoti ya Mruma wakati hata Acacia wenyewe hawaja-comment chochote! Acacia wakaja kuongea kile kile kama ambacho niliongea ama siku moja au siku mbili baadae.... halafu useme nafuata mkumbo!!!
 
@="Bongolander,
Wewe unawezaje kujua umuhimu wa huo mradi? Hiyo mifano ya maneno ya Mwalimu Nyerere haina mashiko wala uhusiano kwani huo mradi siyo maneno ya kijinga ni kitu muhimu katika maendeleo.

Msipende kutoa mifano ya maneno ya Mwalimu Nyerere kwa vitu ambavyo havina uhusiano na maneno yake, hakuna cha matango pori wala nini na Kenya hawatalia na hiyo miradi mikubwa wataendelea kupiga hatua huku vilaza wa CCM mkiwa busy kumshauri Magufuli ujinga na Nchi inazidi kurudi nyuma kimaendeleo.

Miaka 50 sasa chini ya CCM Taifa halina maendeleo kwa kuwakumbatia watu wenye mawazo mufirisi kama nyie, acheni wenye kupenda maendeleo wafanye kazi hiyo mikataba ya wachina ni kukaa chini mezani ikachambuliwa vizuri na Tanzania kuja na hoja zake wanakubaliana kwa faida ya pande zote mradi unaanza haraka tupige hatua tuachane na watu kama nyie msio na huruma na zile bilion 56 walizolipwa fidia kupisha ujenzi wa Bandari huko Bagamoyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…