KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Wewe umejikita kumshambulia Zitto, hushambulii hoja alizoleta hapa na kuzinyoosha tuone palipopinda.Shida ya wanasiasa ndio hiyo, waliowengi wanaangalia maslai binafs. Anachopigania ZZT hapa ni maslai yake binafsi. Kama nchi tulishapitia mikataba mibovu ya madini kwa sababu ya haraka na tamaa za wachache. Nahic ZZT unataka turud huko.
Kwanza najiuliza ivi muheshimu unatetea kwa maslai ya nchi au yako binafs??., au pia ivi karibuni naona Azam 2 wanarusha sana documentary ya huu mradi sasa najiuliza nani analipia airtime ya hiyo documentary? Afu ghafla kaja Zito na hoja zake. Sijui kesho atakuja nani!. Tukiacha unafiki mashart yaliyipo hayatufaidishi labda waboreshe. Ni bora kidogo tunachopata sasa kuliko kujengewa likubwa afu hatupaswi kujua nini kinapatikana
Kiufupi ni kwamba unatafuta njia ya kumnyamazisha, hata kama hutambui kwamba unafanya yaleyale yanayofanywa na serikali ya kuwanyamazisha wasiokubaliana na mambo yanayofanyika huko.
Kwako pengine unaona kila lifanywalo huko, au taarifa yoyote itolewayo huko haistahili kuhojiwa. Tumekuwa na makundi ya watu hawa sasa - wanaohoji chochote kitokacho serikalini, au kukubali chochote kisemwacho kutoka serikalini. Juhudi kubwa zinafanyika kuwaziba midomo hawa wanaohoji. Na hii ndio kazi unayoifanya hapa.