Man, unachanganya mambo!
Hakuna popote niliposema kwamba kiasi so and so ndo reasonable, nilichosema ni kwamba, muda unaowekwa ni kwa ajili ya ku-recover investment + operational cost, plus PROFIT! Aidha, nikasema mara nyingi BOT Schemes, mara nyingi project transfer hufanyika kuanzia miaka 30 na kuendelea!!!
Hii miaka sio kwamba watu huwa wanakurupuka tu na kusema "...tupeni miaka 30!!
That's one, two... 99 Years sio Project Transfer Time bali Land Lease Period! Kwamba, Mwekezaji alitaka land lease ya miaka 99!!
Tatu, kwamba eti nchi yetu na majirani zetu
Jana nilitaka kuandika THREAD kuwaelimisha wale wanaosema kwanini hiyo bandari tusijenge wenyewe kwa pesa zetu!!
The problem watu hawajaelimika vizuri what's behind Bagamoyo Port Project!! Target ya Mchina sio kwamba anajenga bandari kwa matumizi ya nchi za ukanda huu... la hasha!!
Hapa JF nimesema mara nyingi sana kwamba Xi Jinping alipoingia madarakani, alianzisha the so called Belt & Road Initiatives.
Mtandao wa
China Power unailezea BRI kwamba:-Kwahiyo ukisoma hapo utaona kabisa kwamba ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni tofauti na ujenzi wa TAZARA ambayo baada ya Mchina kuijenga, akasepa zake!!
Bandari ya Bagamoyo alilenga kuitumia yeye (ingawaje wengine pia ni rukhsa kuitumi) kama kituo kikuu cha usafirishaji wa bidhaa zake kwenye Ukanda huu wa Afrika!
Unlike projects zingine za BRI in Africa, ndoto ilikuwa kuifanya Bagamoyo kuwa Transshipement Port. Transshipment Port ni bandari inayopokea meli kubwa zenye mzigo, na meli zingine zinaenda kuchukua mzigo hapo!! Yaani, meli kubwa inajaza mzigo kutoka Uchina and bandari zingine za mashariki ya mbali, na kwenda kufunga gati Bagamoyo!!
Sasa mizigo yote inayoenda (say) Mombasa Port, Beira, Maputo and the like, inakuja kufuatwa hapo Bagamoyo kwa kutumia meli za kawaida. Kama ingefanikiwa, huenda ingekuwa to Singapore Port ya Ukanda wa Bahari ya Hindi kama sio Afrika kwa ujumla!
Kwa landlocked zingetumia reli, na ndio maana kwenye ile masterplan, ujenzi wa bandari unaenda sambamba na ujenzi wa reli!Hapa ndo umechanganya madesa moja kwa moja!! Miaka 99 sio ya kuwapa ku-operate bandari bali umiliki wa ardhi! Na ikumbukwe kwamba, wakati MoU inafikiwa, sheria ilikuwa inaruhusu hatimiliki ya miaka 99.
Na hata baada ya marekebisho ya sheria ya ardhi ya mwaka 2017, umiliki upo wa miaka 33 renewable, 66 renewable and 99 years! Hiyo itakuwa a new form of BOT Scheme! But that's not an issue... kama wanaweza kukuibia kwa kuwapa hiyo miaka 40, vile vile wanaweza kukuibia kwa hiyo yearly total cost recovery scheme!
Hakuna anayesema serikali ya Magu iibebe MoU ya JK kama ilivyo! No one contract is perfect! Magu anaweza kuita wanasheria nguri wote duniani wanaozingatia maslahi ya Tanzania na kupendekeza kile chenye manufaa kwetu na Wachina wakapokea bila kufanya editing!!!!
In a year or two, mkataba ule ule ambao ulionekana 100% PERFECT, utaonekana kiondolewe hiki na kiongezwe kile! Na ndio maana mwaka 2010, Sheria ya Mpya ya Madini ikalitaka Bunge liwe linafanya review kila baada ya miaka 5, na faida yake tukaiona mwaka 2017!
Na kwa upande wangu, nimeshasema mara kadhaa ni mambo gani tunatakiwa kuyazingatia na kuhakikisha yanakuwepo kwenye hiyo project! Kawa treated differently kivipi?! Hata kama hukuwa sahihi, umesema Mchina ange-operate bandari kwa miaka 99 kabla ya kuirudisha serikalini!!
Kwa uelewa wako, Dangote atarudisha Kiwanda cha Sementi cha Mtwara baada ya miaka mingapi?!
Kumbe unadhani sie wengine tunaliangalia kwa kutumia nadharia zipi?!
Tatizo la nchi hii ni pale wengine wanapotumia nadharia za kisiasa na zingine za kipumbavu hata kuzipa jina inatia kinyaa!! Ni kawaida sana kusikia watu wakisema ule mradi haufai, JK kaupeleka kule ili kupendelea nyumbani kwao!! Narudia, 33 or 99 ni masuala ya umiliki wa ardhi!! Hayo mengine tushajadili sana, na inatia uvivu kuyarudia rudia!! Na hilo ndo watu tunapigia kelele kila wakati! Nilishawahi kusema hapa kwamba back in 2016 nilikuwa mbeba mikoba wa beberu mmoja wa Kimarekani anayefanya utafiti kuhusu Belt & Road Initiative ya China, na moja ya Case Studies ikiwa ni Bandari ya Bagamoyo!!
In short, Mabeberu wa Marekani na EU wanaipinga sana hii initiative! Pale Ulaya, Mchina aliingia kwenye Bandari Piraeus Port in Greece! Fitina na propaganda zilizokuwa zinafanywa na EU pale Piraeus, Mungu mwenyewe anajua! Watu wakachochea hadi migomo ya wafanyakazi!
Leo hii tunapoongea, mafanikio ya Bandari ya Piraeus yanawaumbua!
Hili la madini bhana, wacha kwa sasa nilipe kisogo! I
Unajua mnachoshindwa kumwelewa Zitto na watetezi wa mradi mnadhani watu wanataka serikali ikubali kila kitu kinachosemwa na mwekezaji!
Hoja hapa ni kwamba, huu mradi ni muhimu mara elfu moja ya uwekezaji kwenye ndege, na kwahiyo serikali haitakiwi kufanya masihara kwenye issue muhimu kama hizi!!
Ukweli ni kwamba, na hili ndilo ambalo huwa natofautiana na Magu, huwa anaweka nguvu kubwa mno... tena kubwa mno maradufu kwa vitu ambavyo ni average na kuacha vitu ambavyo ndo kweli vingeibadilisha uchumi wa Tanzania!!!
Angalia nguvu kubwa anayotumia kwenye madini!! Kaamuru hadi ujenzi wa ukuta Mererani! But look, Capital Market Share ya Acacia haifiki hata USD 5 Billion!!
Barrick Gold na yenyewe, ambayo ndani yake ina kampuni dada takribani saba, huku zikichimba kwenye migodi mikubwa kabisa ya dhahabu kuliko hii ya Tanzania kama vile Cortez Gold Mine na Goldstrike iliyopo Nevada, USA, Market Cap yao ipo around USD 40B, huku mwaka jana wakiwa wame-record Revenue USD 7.2Billion!
Lakini huko Magu anatamani atumie hadi vifaru, lakini kwenye gas ambako uwekezaji wa processing plant tu ni USD 30 Billion... huko wala haonekani kushituka zaidi ya kutoa majibu mepesi kwamba "gas yote imeibiwa!"
Sasa ikiwa wanaoiba dhahabu isiyofika hata Sh 5 Trillion, unaunda tume za kuchunguza, na wengine kuwafukuza kazi, mbona hatuoni akifanya hivyo kwa hao walioiba au kufisadi gesi yenye thamani ya matrilioni ya pesa?!