MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Uogope nini wakati wewe ndiyo mwenye ardhi ??? Bahati nzuri sana nchini Tanzania ardhi mgeni hauziwi na hata kwenye uwekezaji kupitia Joint-Venture ya kawaida au Special Purpose Vehicle anayemiliki hati ya hiyo ardhi ni Export Processing Zones Authority (EPZA) na siyo Uchina wala Oman.Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Ati fedha ni za wachina na wa omani sisi tusiogepe? Are you serious pal? Something very wrong is happening in your brain!
Wajinga tu ndiyo mliodanganywa na kuamini kwamba ardhi ya Tanzania aliuziwa mchina kwa miaka 99. Kumbe alipewa Derivative Right kama sheria ya ardhi inavyosema kuhusu uwekezaji.
Ningekuona una akili ambazo unajisifia hapa, kama ungesema kwamba baadhi ya vifungu vya mkataba virekebishwe ( ambavyo nina uhakika hujawahi hata kuvisoma wala kuviona) na siyo kuniletea porojo za kijinga kwamba watanzania tunaogopa mradi wa Bagamoyo kwasababu tu pesa ni za wachina. Miradi mingapi hapa nchini imefanywa kwa fedha za wageni ???
Halafu mbona hamuogopi kwamba Barrick anamiliki hisa asilimia 80% na sisi 16% wakati madini ni yetu na ardhi ni yetu ??? Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.