Nimemsikia waziri Kamwele sijui nani akiongea leo kuwa eti Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam unaoendelea utaiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kupokea meli zenye upana mkubwa hadi mita 260 tofauti na sasa ambapo inapokea max mita 200.
Huo unaweza kuwa ukweli na uongo pia.
Bandari ya Dar es Salaam ina berth (gati) 7, na sasa wameongeza moja maalum kwa meli za magari, Itakuwa jumla 8.
Berth no. 1-7 zote zina upana wa wastani wa 190 mita.
Kitachotokea ni kuwa, inapofika meli kubwa, let's say ya 260 mita, meli itafunga kwenye berth mbili kwa wakati mmoja (yaani itatumia mita 190 za Beth moja na ku overlap kwenye berth ya jirani by 80 mita.), hivyo, kuua berth moja haifanyi kazi maana itabakia na upana mdogo usiowezesha meli nyingine kufunga)
Kwa hali ya kuruhusu meli zenye upana mrefu kufunga, bandari imejikuta inahudumia meli wastani wa 4 tu kwa wakati, na kusabanisha msongamano mkubwa sana wa meli kusubiri muda mrefu nje
Kitu kitakachosaidia ktk upanuzi huu, ni kina cha berth (draft) ambapo ilikuwa 8.7m na sasa imeenda hadi 14 mita.
All on all, kwa kitengo cha serikali kuua soko huria kwa kutaka kufanya kazi zote za shipping agent serikali wenyewe, clearing and forwarding agency, bandari hii itabakia kuhudumia mizigo ya ndani tu, maana hakutakuwa na usbindani, na ikumbukwe kuwa private shipping agent zinachangia kiasi kikubwa kutafuta kazi huko nje