Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?

kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?

Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu

Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!

Kuwa na uwingi wa miradi haina maana kwamba umasikini ndiyo basi tena, Isipokuwa ni kuwa miradi yenye tija

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
Tuanzie hapa kwanza ni mkataba upi ambao umeshawekwa hadharani kwa nchi hii?ndio maana tunasikia mengi na tumuamini nani?watu wanapopigania uwazi kwenye serikali mnawaita wanatumwa na mabeberu, leo yakiwakuta ndio tena mnawaona wa maana!!wewe hata mbunge wako hajui mkataba unasemaje, na yeye anasikia kama mkulima wa kijijini tu
 
Mkuu watanzania baadhi ni mazwazwa kujifanya kuhoji baadhi ya vitu wakati huo huo Kuna vitu Kama hivyo vimefanywa walikuwa kimya
 
Tanzania hakuna bandari kuna vichochoro, ili bandari ya Dar iwe bandari itakubidi uihamishe kigamboni yote na uichimbe iwe bahari... na ile kurasini yote ndio iwe container terminal...
 
Najiuliza kwanini Magufuli pamoja na kuwapenda kwake wachina na kuwaita marafiki wa kweli lakini bado aliukataa huu mradi wao, nadhani hapa lipo la kutafakari, tusiende kishabiki tu.
Nyie makamanda mnaoimba pambio na kupiga makofi kila siku kwa lengo kumkomoa Hayati JPM ndio mtabeba lawama zote endapo mama ataingizwa chaka.
 
Mmmh! Unavyoandika tu inaonesha uko chini ya kiwango. Watu kulala njaa tena! Hiyo bandari ndo mkombozi? Foolish!
Haujui kama itatoa ajira? Nyie ndio sample ya watu waKenya wanachukua kutujudge kutokana na ujinga wenu
 
Kukataa mradi wa bagamoyo ilikua na lengo baya kwa mtangulizi wa jpm pia kwanini hilo hulioni unaona tu la mama kutaka majadiliano ili hali mwendazake aliukataa.
Mshale kwa nguruwe..........
Alianza kuukata lowasa na chadema ya Zaman kwenye kampen
 
Yaani ni swala na maslahi binafsi. Ndo maana watu wengi wanakimbilia kwenye siasa kwa sababu kuna maslahi bnafsi. Mwisho wa siku siasa inaonekana ya watu wajanja wajanja na maslahi binafsi.
 
Kwanini ile proposal ya kwanza isiwekwe hadharani tusisomee wenyewe? JPM atleast alipoint out vipengele vya kipigaji kusema ni kichaa pekee angeweza kukubali. Waliokuwa wanamshauri JPM wapo wapi? Mama kawatupa nje?

Mama Samia sijui anakuwa guided na nani? Hii ni hatari kwa usalama wa Nchi

Usalama wa Nchi unakuwa hatarini kiuchumi au kiulinzi? Maana kama Ni kiuchumi bado kuna makampuni kibao ya kichina yako hapo nchini Kama ni kiulinzi miundombinu mingi ya jeshi imejengwa na wachina, achia mbali mafunzo mbalimbali yanayotolewa na wachina kwa jeshi letu.
 
Nimejipanga kuwa mpiga kampeni wa Upinzani, na hili ni halali yangu kwa sababu katiba hainizuii kuhama Chama!!

Kwa tunakokwenda, ni Dhahili sasa CCM wamepigwa upofu ili tupate ukombozi mwingine

Kuendelea kupuuza misingi bora ya aliyotuonyesha kidogo JPM hayati kwa kujali na kutetea maslahi ya nchi yetu pia kulinda kwa gharama zote rasilimali zetu, huu ni upofu kwa CCM ya sasa

JPM hakuwa na misingi yoyote, bali alikuwa kiongozi muongo, muovu na dhalimu. Na kwa taarifa yako kwenye upinzani hakuna mtu anataka wanafiki wa aina yako. Na Mkitaka kujua hakuna mtu ana muda na nyie wazalendo uchwara, anzisheni chama chenu muone kama mtapata uungwaji wowote mkono.
 
Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?

kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?

Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu

Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!

Kuwa na uwingi wa miradi haina maana kwamba umasikini ndiyo basi tena, Isipokuwa ni kuwa miradi yenye tija

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
Katika mikataba ya uwekezaji au biashara kati ya mataifa masikini na mataifa yaliyoendelea au baina ya makampuni ya kimataifa na mataifa masikini ni muhimu sana kuwa makini na rasimu ya kwanza ya mikataba, ukichemka hapo umekwisha uko mbeleni hakuna tena linaloweza kubadilishwa. Hata ukitafuta mbia mwingine atakuja na rasimu hiyo hiyo ya mwanzo, maana imekwisha kuwa ndiyo Blue Print ya mradi huo. Na wenye masiko wasikie 📻
 
Naona kama rais mwanamke amepata akili kuliko wa-tz wote! Hii ndo hali ya kawaida kwa viongozi wa kiafrika. Wakipata madaraka tu, wanaamini wana akili kuliko wengine wote, hata ktk hali ya rais wetu anayefahamu wazi ana urais wa urithi.

Rais anaelekea kujifanya kuwa ni rais wa mageuzi ktk kila kitu, hata mambo ambayo yana mifano mibovu kwa nchi zingine. Badala ya kuanzisha miradi na mipango mizuri ya kwake, yeye amekuwa ni mtu wa kufufua yaliyokataliwa na taifa hili. Tunakubali bandari, mkataba ni upi?
Taifa halijakataa mradi sema mwendazake
 
Sawa mkuu, utambue kibiashara inauwa bandari zetu zote ambazo tunazitegemea kama sehemu ya kitegsuchumi wa nchi yetu?

Embu jiilize, Kutoka Bandari ya Dar hadi Mbegani Bagamoyo ni kama kilomita 68 tu hivi,

lakini pia kama ni lazima tuwe na bandari hiyo, kwa nini kusiwepo na uwekezaji ambao unatoa faida kwa nchi, Kama yale aliyosemaJPM na Lowassa ni ya kweli, basi taifa letu iko siku Mungu atalitaka na ataona aliwapa watu wasiojielewa na hawana faida

Lowassa na JPM walikuwa ni matapeli wa kisiasa. Mnamtaja Lowassa mkitegemea kwakuwa alipokelewa na Mbowe, basi mtapata uungwaji mkono na wapinzani. Mkitutajia hayo matapeli ya kisiasa ndio mnatuchafua kinoma.
 
Tuingie kwenye majadiliano na wawekezaji kwa kina km tulivyofanya kwenye madini. Timu ile bado ipo ipewe tu hadidu za rejea za mradi wa Bagamoyo kukwepa upigaji

Ndo inavyotakiwa iwe, kuwe na team ya kupitia mkataba na uwekwe wazi kwa wananchi kwa sababu nchi hii si viongozi pekee.
 
Hapo alikuwa chadema,! Wakati huo wewe ulikuwa bado unanyonya

Lowassa hakuwa cdm na wala hatakaa awe cdm, yeye alimuhonga Mbowe na genge lake ili agombee urais. Lile zee lilikuwa tapeli tu la kisiasa.
 
Back
Top Bottom