Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

10% wanajulikana tu! unadhani ukilipwa hiyo ndiyo itakufanya uishi duniani siku zote, tunalinda rasilimali kwa ajili ya vizazi vijavyo
vizazi vijavyo ni vipi hivyo? kauli za kijinga tu na kitapeli upumbavu nchi hii shida sana kuisha. Jenga nchi imara fursa kwa wote watakaokuja wakute misingi imara na wao waendeleze. ila usilete kauli ya kijamaa na kijinga vizazi vijavyo au kizazi chako. Ukimuona mtu yoyote anajificha nyuma ya udini na utaifa ogopa sana hao. Mahitaji ya kiuchumi duniani ya leo sio kesho tech inakuwa kwa haraka leo unayoona ni rasimali kesho hata bure hakuna wa kuchukuwa watu wanaendelea wewe utabaki naweka kwa kizazi kijacho.
 
Nchi sasa itaongoza kwa mikataba laghai kupitia kwa yule kichaa aliyesemwa na JPM
 
Lowassa hakuwa cdm na wala hatakaa awe cdm, yeye alimuhonga Mbowe na genge lake ili agombee urais. Lile zee lilikuwa tapeli tu la kisiasa.
Ila Mbowe aliyewaletea chuma chakavu yeye sio tapeli? na bado mkampa uenyekiti...ndo maana nyie mkaitwa nyumbu
 
Katika utawala wote wa CCM hakuna mktaba hata mmoja uliowahi kuwekwa wazi ili tuhoji kama una maslahi kwa taifa, bahati nzuri tu wakati wa Mwalimu na Karume walijali maslahi ya watanzania.
Mikataba ya madini, gesi, mafuta, ununuzi wa ndege, SGR, uwanja wa ndege na bandari ya Bagamoyo haijawahi kuwekwa wazi au kujadiliwa hata bungeni. Na yote imegubikwa na utata. Kwa bahati mbaya JPM alishupalia sana suala la bandari wakati serikali yake imefanya hayo hayo na kudhindwa kurekebisha mikataba aliyoikuta hasa ya madini.
 
Mpaka hapo Bara watakapoelewa kuwa maendeleo ya ukanda fulani hupambaniwa kuelekea ukanda huo ndio watajua CCM kumbe ni chama cha Maslahi ya watu wa pwani!
 
Hivi mna matatizo gani lkn? Penda kufanya research ndo uje uandike hapa jukwaani. Unajitia aibu kwa huu mchango wakonwa chuki na ubinafsi hapa ujue. Acha kufata upepo. Mradi wa Bagamoyo una tija kwa Taifa. Hivi Ile chato airport haikusaidii?? Mbona mama alipoenda kigogo busisi hamkulalamika???
 
Mkuu, tunauwa vyanzo vya uchumi wetu kwa sababu tu tunataka tume huru
Hahahaaa!!! Ile comment yake imeniacha kinywa wazi....hawa ndio wapinzani wanaopigania kushika hatamu.....yeye kwa sasa hivi haya mambo sio kipaumbele chake.....kwanza tume huru....baada ya kushika madaraka wanakuja kulaumu ubovu wa mikataba......
 
BBaaDa
Hii Bandari ina maana Hayati alitudanganya?

Kwa maslahi mapana ya Taifa mikataba iwekwe wazi

Kwa nchi nzima itakua haina maana.

Labda Kwa Wizara,Wakuu wa Taasisi za Uwajibikaji nchini na Wadau wa muhimu.

Kukataa mradi wa bagamoyo ilikua na lengo baya kwa mtangulizi wa jpm pia kwanini hilo hulioni unaona tu la mama kutaka majadiliano ili hali mwendazake aliukataa.
Mshale kwa nguruwe..........
Baada ya kusikia Rais wetu kaongea na simu ya Rais wa China nikajua Kuna suprise inakuja, sasa hii ndio suprise yenyewe.
 
Kama mtu alituaminisha miradi yote ni hela za ndani na deni la Taifa ninapaa tu huyo sio wakuamini ata kidogo.
Na wengi tuliamini hivyo lakini mkopo wa Trillion 31 katika miaka mitano tu,tena tokea benki za biashara akina EXIM Bank tutawalipisha hadi vitukuu.Kumbe tumeuziwa mbuzi kwenye gunia.
Kukosekana ukweli na uwazi katika utawala ndio sababu kuu ya wananchi kudai katiba mpya ya Warioba.
 
Pale palikuwa iundwe committee team ya nchi tatu, china, oman na Tanzania naTRAwalikuwa wapewe mgao toka hiyo tume
 
Mzee akili za aina hii za kuuliza maswali intelligent ya aina hii wanayo only 1 percent ya watanzania, hata hao viongozi sidhani kama wanayo. Tena humu JF sidhani kama utapata mtu wa kukujibu haya maswali, wengi humu ni viazi, sio watu wa kusoma, kujifunza, wengi ni
mashabiki wa kisiasa, kufanya comparative analysis, hata kuona tu nchi zilizoingia migogoro sababu ya aina hii ya miradi ya kichina.

Ujinga mwingi mno sisi watu weusi. Watu waliokuwa wanapandisha twiga kwenye ndege wanauzalendo gani kwenye nchi hii? Subiri uone utumwa utakaokumba vizazi sababu ya huo mradi.
 
Wale waliomshauri Magufuli kuhusu hiyo Bandari awali hebu wajitokeze watueleweshe uozo uliopo kwenye huo mpango mzima.
 
Bora sikuzaliwa Mwafrika, japo nimekulia Afrika,.
Hawa wanastahili kutawaliwa for good
 
Madini si ndio aliwasumbua barrick gold,ndio mpaka makinikia yakazuiwa kuondoka,akafanya juhudi na kijenga ukuta?
Au mimi ndio sielewi?
Hiko kieneo cha bagamoyo kitakuwa ni koloni la wachina,hiko kipande tunauza nchi yetu.watatusumbua sana wachina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sidhani kama uko sahihi. Mikataba ya madini ilisainiwa JPM akiwa waziri na wakati huo mtaalamu wa sheria za madini (PhD) sasa hivi ni waziri na ndiyo mikataba iliyoleta mrahaba wa 3%. Na ndiyo mikataba mibovu sana ulimwenguni. Tundu Lissu alipiga kelele sana kuhusu hii mikataba ya madini ambayo kila serikali ya CCM haitaki kuipitia upya.

Kulikuwa hakuna haja ya kuunda tume au kusitisha kusafirishwa kwa makinikia, alichotakiwa kufanya JPM ni kuipitia mikataba yote UPYA NA KUIBADILISHA lakini akagwaya kama watangulizi wake. Akapeleka mswada bungeni wa kulinda raslimali za nchi, lakini cha ajabu katika muswada huo kuna kipengele kinasema "SHERIA HII HAITAHUSIKA NA MIKATABA YA AWALI". Kama unajua athari ya sheria hii, basi utajua kuwa suala ni mikataba ambayo sababu wanazojua wenyewe viongozi wetu waliridhia, wakasaini na hawataki kuitengua.

Tusilaumu wachina au mabeberu. Matatizo yako kwetu na ha viongozi wetu.8
 
Ila Mbowe aliyewaletea chuma chakavu yeye sio tapeli? na bado mkampa uenyekiti...ndo maana nyie mkaitwa nyumbu

Uenyekiti kapewa na wanachama kupitia njia ya kura, ila hiyo haipunguzi ukweli kuwa kwa kulichukua lile zee tapeli alichemsha. Unakwama wapi mama Majaliwa?
 
wewe ni mtu duni mno kifikra

Huwezi kusema vitu vya kipumbavu eti ndiyo viwe msingi wa vizazi vijavyo, Tunatumia akili kubwa tunapotazama mbele,

Sisi tunajadili uwekezaji wenye tija, wewe unakuja na mitusi utadhani ni chakula chako cha asubuhi, Jenga hoja, Narudia tena kukubali mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuzingatia manufaa ya uchumi ya nchi yetu, na bila kuondoa baadhi ya mashariti kandamizi, ni kuuwa kwa maksudi bandari zilizopo

Sasa wewe, badala ya kuja na hoja unakuja na matusi utadhani wewe ni mjusi haya bhana
 
Lowassa na JPM walikuwa ni matapeli wa kisiasa. Mnamtaja Lowassa mkitegemea kwakuwa alipokelewa na Mbowe, basi mtapata uungwaji mkono na wapinzani. Mkitutajia hayo matapeli ya kisiasa ndio mnatuchafua kinoma.
Gombea uraisi sasa wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…