Mradi wa barabara ya mwendokasi Kilwa Road

Mradi wa barabara ya mwendokasi Kilwa Road

menny terry

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
509
Reaction score
670
Wakuu!

Jana nimetembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa kipande hiki cha barabara kutokea mbagala hadi kariakoo! Hakika inapendeza sana. Asilimia kubwa imekamilika hivyo soon mradi huu utakuwa unaanza kazi!

Lakini tofauti niliyoiona ni kuwa ile awamu ya kwanza ambayo ilijengwa Na strabag kwakweli ilikuwa Na viwango vya juu sana, Strabag walifanya kazi ya kibabe sana, Kuanzia barabara yenyewe mpaka vituo vya abiria ni vyote ni vya hali ya juu sana.

Tukirudi Kwenye huu mradi ukiangalia hata vituo vya abiria japo bado havija kamilika utagundua ni vidogo sana alafu ni vyembamba sio makubwa kama yale ya phase one, Zege iliyowekwa ni ile nyembamba pia! Japo sijajua ni kampuni gani inajenga huu mradi ila kiuhalisia haujakutia phase one Kwa ubora wa hali ya juu japo pia kwakweli wamejitahidi na soon watu wa mbagala watapunguziwa tabu ya usafiri.
 
Hujamsikia Jerry Slaa, huyo mchina kashajipigia hapo
 
Huu mradi upo chini ya kiwango, barabara haijaisha inavunjwa na kujengwa upya.

Misheni,mtoni mtongani Hadi sabasaba kipati walivunja na kujenga upya Kwa sababu barabara ilianza kuharibika kabla haijatumika.

Pita pale mtoni kizinga (msikitini) utaona ushahidi wa Hilo ninachokumbia maana mapande yote ya zege walkuovunja na kujenga upya yamekuja kutupwa pale kwenye mto na yapo hata sasa.

Mbaya zaidi huyu mkandarasi mchina syno hydro ndy amepewa tena tenda ya kujenga phase iii kutoka gongo la mboto wenye km 23 wakati huu mradi wa kilwa road phase 2 wenye km 19 unaenda slow na upo chini ya kiwango.Nadikia tumeahidiwa utakamilika mwakani 2023 mwezi March.

Hadi juzi mbunge wa ukonga(sina uhakika na Jimbo) mg Jerry Slaa alilia bungeni Kwa ajili ya huo mradi unaokuja baada ya huu wa Kilwa road anailaumu serikali Kwa nn phase III apewe tena mkandarasi yuleyule wa phase II ambaye anajenga chini ya kiwango na anasuasua.
 
Kwanini.wasinge wapa wachina walio.jenga flyover ya ubungo?
Huu mradi upo chini ya kiwango, barabara haijaisha inavunjwa na kujengwa upya

Misheni,mtoni mtongani Hadi sabasaba kipati walivunja na kujenga upya Kwa sababu barabara ilianza kuharibika kabla haijatumika

Pita pale mtoni kizinga (msikitini) utaona ushahidi wa Hilo ninachokumbia maana mapande yote ya zege walkuovunja na kujenga upya yamekuja kutupwa pale kwenye mto na yapo hata sasa

Mbaya zaidi huyu mkandarasi mchina syno hydro ndy amepewa tena tenda ya kujenga phase iii kutoka gongo la mboto wenye km 23 wakati huu mradi wa kilwa road phase 2 wenye km 19 unaenda slow na upo chini ya kiwango.Nadikia tumeahidiwa utakamilika mwakani 2023 mwezi march..Hadi juzi mbunge wa ukonga(sina uhakika na Jimbo) mg Jerry slaa alilia bungeni Kwa ajili ya huo mradi unaokuja baada ya huu WA kilwa road anailaumu serikali Kwa nn phase III apewe tena mkandarasi yuleyule wa phase II ambaye anajenga chini ya kiwango na anasuasua
 
Mbongo hata kupima mgonjwa hahitaji maabara

akimuona tu anakwambia huyu alivyokonda itakuwa ana sukari, TB au Ukimwi

akishika kichwa cha Mtoto wake anakwambia anachemka ana malaria
Akikuangalia machoni mbongo anajua Jana ulikuwa Tabata Barracuda! 😂 😂

Sometimes sauti tu wala hahitaji kuona! Anatoa diagnosis! Hiyo sauti ni Corona!
 
Huu mradi upo chini ya kiwango, barabara haijaisha inavunjwa na kujengwa upya

Misheni,mtoni mtongani Hadi sabasaba kipati walivunja na kujenga upya Kwa sababu barabara ilianza kuharibika kabla haijatumika

Pita pale mtoni kizinga (msikitini) utaona ushahidi wa Hilo ninachokumbia maana mapande yote ya zege walkuovunja na kujenga upya yamekuja kutupwa pale kwenye mto na yapo hata sasa

Mbaya zaidi huyu mkandarasi mchina syno hydro ndy amepewa tena tenda ya kujenga phase iii kutoka gongo la mboto wenye km 23 wakati huu mradi wa kilwa road phase 2 wenye km 19 unaenda slow na upo chini ya kiwango.Nadikia tumeahidiwa utakamilika mwakani 2023 mwezi march..Hadi juzi mbunge wa ukonga(sina uhakika na Jimbo) mg Jerry slaa alilia bungeni Kwa ajili ya huo mradi unaokuja baada ya huu WA kilwa road anailaumu serikali Kwa nn phase III apewe tena mkandarasi yuleyule wa phase II ambaye anajenga chini ya kiwango na anasuasua
Mtoa mada inaelekea sio mkazi au mpitaji wa maeneo hayo mara mara ila kwangu mimi naona mkandarasi wa kipande cha Mbangala ni puwa zaidi kuliko wa sehemu zote makosa mengi , mradi spindi ya kobe nk
 
Huu mradi ni wakipumbavu sana. Mimi ni mmoja naye sema huko chini ya kiwango. Kipindi kile unajengwa huu wa kwanza ulikua unaona nondo na zege za kutosha. Mfano vituo na zile gema za kutenganisha barabara za mwendokasi. Ukipita ile njia unaona kabisa hapa tunaunganisha barabara na Zege pasipo ubora.

Kuna makosa yanafanyika na kama yaliyofanyika hapo mwanzo. Mfano pale mto msimbazi na kigogo chini kuja magomeni bado barabara wanaijenga chini vile vile. Ile barabara kipindi cha mvua ni maji huwa yanapita juu. Yanakua yale yale ya mkwajuni au jangwani.

Nahisi huyu mkandarasi ni wa bei ndogo na anatujengea kulingana na bajeti au utoaji pesa wetu. Kikubwa mradi ukamilike zipigwe shangilio
 
Wakuu!

Jana nimetembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa kipande hiki cha barabara kutokea mbagala hadi kariakoo! Hakika inapendeza sana. Asilimia kubwa imekamilika hivyo soon mradi huu utakuwa unaanza kazi! Lakini tofauti niliyoiona ni kuwa ile awamu ya kwanza ambayo ilijengwa Na strabag kwakweli Kwa kiwango kikubwa walijenga Kwa viwango vya juu sana. Kuanzia barabara yenyewe mpaka vituo vya abiria ni vya hali ya juu sana. Kwenye huu mradi ukiangalia hata vituo vya abiria japo bado havija kamilika utagundua ni vidogo sio makubwa kama yale ya phase one. Japo sijajua ni kampuni gani inajenga huu mradi. Otherwise kwakweli wamejitahidi na soon watu wa mbagala watapunguziwa tabu ya usafiri.

Nawasilisha.

Mchina na itazinduliwa mwisho wa mwezi.
 
Sijui kwanini Mjerumani wa Starbarg ambaye kajenga poa sana Morogoro RD hakuachwa aendelee na phase zingine badala yake kanyang'anywa na kupewa Mchina substanard
Kale kapasenti ketu kanapatikanaje mkuu!
 
Back
Top Bottom