Mradi wa bomba la gesi asili toka Tanzania kwenda Kenya

Siyo swala la kuwa Mwafrika au la, ni swala la kiuchumi, haya mambo ndiyo yaliyotufikisha hapa, kuwekeza 1 bilion USD kwa nchi kama Tanzania ni pesa nyingi sana, na Kenya hakuna uchumi wa kuhalisha huo uwekezaji.
Ni trillion ngapi kwa pesa ya Tanzania?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Unangaalia horizon ya muda gani?

Lakini sio pesa nyingi Kama unavyofikiria it's just 2.3trillion sh.
 
Hivi hizi gas mihan, taifa, manjis ziko kwenye form ipi? Zinatokea mtwara? Naogopa kusema kuwa tuna gas lkn hatuiztumii kumbe tunazo za orexy, mihan, lake gas, manjis, taifa gas etc

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Unangaalia horizon ya muda gani?

Lakini sio pesa nyingi Kama unavyofikiria it's just 2.3trillion sh.

Ni nyingi sana kwa ukubwa wa Uchumi wa Tanzania, ukitaka kujua 1 bilion USD ni kiasi fikiria hili, Mgodi mzima wa Buzwagi thamani yake ilikuwa ni Milioni 300 USD, lkn Serikali ilitafuta muwekezaji kwa kuwa pamoja na mambo mengine haikuwa na hizo fedha, hivyo ina maana kwa 1 bilioni USD tuna uwezo wa kuwa na Migodi 2 kama Buzwagi na kubakia chenji, Migodi ambayo tungeimiliki kwa 100% na siyo kupata 3%, sasa kwa nini tutumiie 1 billion USD kujenga Bomba la mafuta kwenda Kenya ambapo hata haitolipa?
 
Hivi we mkikuyu ni mtz au nyang'au? Ha ha ha

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kama tunajenga miradi ya trillion 6 na 7 SGR na Umeme, 2.3 ni hela ya mboga tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kama tunajenga miradi ya trillion 6 na 7 SGR na Umeme, 2.3 ni hela ya mboga tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app

Nafikiri labda hatuko page moja na tunaongelea vitu 2 tofauti, sisemi kwmba hatuna uwezo wa kupata 1 billion USD bali huo mradi kwa maoni yangu haulipi kwa fedha zote hizo, nina uhakika 1 bilion USD kama tunazo hapa Tanzania tunaweza kufanyia mambo mengi na yenye kuleta faida kubwa kuliko hilo bomba.
 
Soma vizuri nimesema haina faida beyond Nairobi, lakini Mombasa to Nairobi inasaidia ndio sababu nikasema umuhimu wa Mombasa to Nairobi super high way haupo tena kutokana na kuwepo hiyo reli
Nafurahi kuona kwamba uko objective. Yaani kama kitu kina manufaa naona huogopi kusema. Hio ni poa. Ndio Sgr ina mapungufu mengi ila pia ina manufaa yake. Endelea kusimama na ukweli.
 
Twende kwa mfano

Matumizi ya mwezi gasi ya kupikia ni mtungi wa kg 15, sawa na 53,000/-.

Tuchukue 1/4 ya watu milion 50 wa kemya wanatumia au watatumia gas kwa matumizi ya nyumbani. Ni sawa na kaya 12,500,000 zitumie gas kupikia.

12,500,000*53,000=662,500,000,000/-

Zidisha kwa mwaka yaani 12 month's
=7,950,000,000,000/-

Sijasoma hesabu. Lkn iko hivyo iwapo nishati nyingine zitapigwa marufuku

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hayo yangefanyika hapa nyumbani kwanza na kuwa success story ndiyo tungeanzia hapo na hayo Mahesabu yako, kumbuka Gesi kuifikisha Majumbani ni lazima Miundo mbinu iwepo pia, sasa ni nani ataijenga hiyo Miundo mbinu huko Kenya? Ni Kaya kwanza ngapi hapa nyumbani zinatumia Gesi ya Tanzania kwa matumizi ya kila siku? Kaya nyingi zilizonizunguka zinatumia gesi ya Mitungi ambayo inaagizwa kutoka nje, kwanza sijawahi kukutana Mtanzania ambaye anatumia Gesi ya Tanzania nyumbani kwake.
 
Nimeuliza hili swali kuwa hizi mihan, manjis, lake gas, orexy zinatokana na gas yetu? Sijapata jibu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hizi gas mihan, taifa, manjis ziko kwenye form ipi? Zinatokea mtwara? Naogopa kusema kuwa tuna gas lkn hatuiztumii kumbe tunazo za orexy, mihan, lake gas, manjis, taifa gas etc

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kaka gesi yoyote iliyopo ndani ya mtungi ni "Liquid form", yaani imekuwa "Compressed tayari. Hapa Africa hakuna kiwanda hata kimoja kinachofanya hivyo, hizo gesi zote zinatoka Uarabuni na mashariki ya kati.

Kama kiwanda kitajengwa mtwara kama tunavyotegemea huenda kikawa ndio cha kwanza Africa, hiyo haina maana kwamba gasi za kwenye mitungi zitapungua bei kwasababu kiwanda kipo Tanzania.

Chukulia mfano wa maji ya kunywa, chupa moja ya maji ya Lita moja ni Tsh 500, Lakini ndoo moja ya maji ya Lita 20 kwenye kiosk cha serikali ni Tsh 50. Kwahiyo mkombozi wa wananchi ni pipe za Vodacom gesi majumbani sio gesi za kwenye mitungi, hicho kiwanda ni kwa ajili ya biashara.
 
Du bro kuwa serious,

Bomba la gas kutoka Mtwara Hadi Dar ni Dola 600 million, na tunatumia only 11%.

SGR Dar Moro ni zaidi ya hiyo hela usiwaze kimasikini hivyo
 
Siyo, zinaagizwa kutoka nje,hao ni wasambazaji tu, ni kama tu waagizaji wa Windhoek au budweiser bia, ingekuwa ni ya kwetu tungekuwa mbali sana, ...
Basi sawa, inaweza isisaidie kama bado gas yetu wenyewe haitusaidii.

Kwa hiyo mkuu unataka kusema gas iliyozuiwa kuuzwa kenya kipindi kile ni ya wasambazaji tu wa Tanzania siyo gas ya Tanzania?

Kwa hiyo Tanzania tunaweza uwakala kuliko Kenya hadi sisi kuwasambazia hadi wao tena gas toka Tanzania kuwa nafuu kuliko inayosambazwa Kenya?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Du bro kuwa serious,

Bomba la gas kutoka Mtwara Hadi Dar ni Dola 600 million, na tunatumia only 11%.

SGR Dar Moro ni zaidi ya hiyo hela usiwaze kimasikini hivyo

Sasa nani anapaswa kuwa serious hapo? Wewe mwenyewe umesema tunatumia tu 11% ina maana siyo success story, sasa sababu ni nini? Kwani nini tukawekeza 1 billion US dollars nyingine kama huu uliopo haufikii hata 20% ya matumizi yake?
 
Ah wasinge pelekewa ilo bomba la gesi maana ni washindan wetu na wanajifanya wajanja sanaaa.

Kuna siku nilimsikia Mqnager wa TCAA akielezea swala la radar zile akasema majamaa yalipeleka proposal ya radar zao zimulike mpaka tz (kumne waki muoika radar ktk eneo la Tz fee wana chukua wao jumla jumla ) ss TCAA wakawa wahi. Hawa wange achwa waendelee watumie mkaa na kuni mpaka wakome
 
Ngumu kumesa mzee. Sasa hii gas ya hawa makonde waliokataa haitoki Mtwara, imesaidia nini hadi sasa?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo mazito. Dola bilion moja hiyo na usheee​

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…