Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Umeme ni huduma muhimu sana kwa uchumi na uhai wa taifa lolote katika dunia hii ya sasa. Hivyo mbali na kupata huduma hii, lazima pia tuzingatie gharama nafuu kwa wananchi. Unadhani tukiruhusu makampuni binafsi kuzalisha, kusafirisha na kuuza umeme tunaweza kupata umeme wa gharama nafuu ??? (Kama ndiyo, naomba utusaidie kutuonesha ni kipivi itakuwa hivyo)

Nchini Marekani umeme wa Tennessee Valley Authority (TVA) ambalo ni shirika la kiserikali una gharama nafuu zaidi kuliko ule kutoka kwenye mashirika binafsi. Unadhani hili linawezekana kufanyika nchini Tanzania ???
Mwaka jana watu wengi walikufa kwa baridi jimboni Texas baada ya kutokea baridi kali, ambayo huwa inatokea kila baada ya miaka 40 - 50.

Kisa, kampuni binafsi za uzalishaji umeme zilizima mitambo kwasababu ya kuogopa hasara watakayoipata kutokana na mahitaji makubwa ya umeme kuongezeka.
 
Hatari sana, PRIVATE INTERESTS zisipoangaliwa kwa ukaribu zinaweza kuvuruga kabisa nchi....
 
Miradi kama hii haipimwi kwa financial viability. Kuna vigezo zaidi ya hivyo. Angalia kwenye nyanja za kiuchumi na kijamii. Kuna internal rate of return kubwa sana for time infinity.

CC: MALCOM LUMUMBA
Internal rate of return kutoka guugu inasemwa hivi

"Internal rate of return is a method of calculating an investment’s rate of return. The term internal refers to the fact that the calculation excludes external factors, such as the risk-free rate, inflation, the cost of capital, or financial risk. The method may be applied either ex-post or ex-ante"

Kutoka guugu hiyo utaletewa Levellised cost of energy, hii nayo ni

The levelized cost of energy (LCOE), or levelized cost of electricity, is a measure of the average net present cost of electricity generation for a generating plant over its lifetime. It is used for investment planning and to compare different methods of electricity generation on a consistent basis

====

Mkuu twende sawa, kwa ufupi, "IRR is weak and LCOE is strong", linapokuja suala la kuamua ni mradi gani wa uzalishaji wa nishati tuwekeze. Sababu kubwa, LCOE inahusisha realistic parameters nyingi zinazohusu mradi husika.

Kanuni tu za kukokotoa indexes hizi zitakupa picha ya ninachokieleza. Kama ni mradi wa nishati, kukuruka na vipimo vingine lakini usiache kutumia LCOE katika kuamua ni mradi gani unataka kuwekeza.
 
Kwa zote mbili umeme wa hydro will always rank high and be a best option against any other possible and available alternative inayojulikana kwa sasa...Unless huna comparative advantage za landscape na flows....Hakuna jinsi iwe ki ecology au ki economics umeme wa gas ukaukaribia hata kwa mbali ule wa hydro...

Tatizo la sisi ni policies zetu ambazo zina much influence kutoka kwa waliotutawala UK na mshirika wake USA ambao so far duniani zaidi ya kuwa wafanya mauaji ya kivita hawafui dafu kwa taifa lolote....Welfare zao ni mbovu na economic policies zao ndizo hasa zilizotufikisha hapa tulipo leo kwenye degradation ya hali ya juu ya mazingira.

Ni ajabu sana kwaini hatuzi abandon hizo failed economic policies zao...Sustainable development haiangalii hizo factors unazozitaja bali welfare ni kitu cha kwanza; huko kwenye nchi hizo mbili welfare ni mbovu na poverty gap ni kubwa miongoni mwa walionacho na wasionacho kuliko other EU countries ambazo nyingi zina policies zenye kuzingatia welfare zaidi i.e social benefits against private benefits. Kinara wa hizo ni Scandnavia na dunia yote inaelekea huko ni sisi tu ambao tunajidanganya yet siasa yetu ya ujamaa na kujitegemea inafanana sana na hizo EU countries nyingine including zisizo kuwepo EU but ni za Europe.

Hao ndiyo ambao wali comoditize education mpaka tukaanza kupata ma degree fake fake; hawa ndiyo vinara wa ufisadi duniani kupitia multi national companies, hao ndiyo ambao wanaojitahidi sana kushikilia mifumo ya dunia lakini pumzi zina akaribia kuwaishia...Let be watchful, economics ya projects za leo na financial analyses hazipo katika hizo investiment criteria za kizamani, tumeshaondoka huko, what is financially expensive can be very cheap and sustainable if given a low discount rate based on those extenalities unazozielezea mojawapo ikiwa social costs ambazo private firms haiziingizi kwenye cost functions zao; get your facts right nigga!
 
Let be watchful, economics ya projects za leo na financial analyses hazipo katika hizo investiment criteria za kizamani, tumeshaondoka huko, what is financially expensive can be very cheap and sustainable if given a low discount rate based on those extenalities unazozielezea mojawapo ikiwa social costs ambazo private firms haiziingizi kwenye cost functions zao; get your facts right nigga!
Asante kwa maelezo yako yote. Msingi wa hoja yako nadhani upo hapa. Hivyo, naomba ufafanue hili kwa kutumia mifano inaoendana na uhalisia ili kuipa nguvu zaidi hoja yako ya "financilly expensive is very chip based on BoT discounted rate". Pia nitafurahi ukiweka hapa investment criteria za kisasa ukiachana na kizamani nilizo bwaga kwenye uzi huu.

Natanguliza shukrani.
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA nimelisoma bandiko lako kwa umakini.

1. Nimsahihishe Stuxnet bandiko#53. Stigler's Gorge haikuanza na Mwalimu, ilikuwepo' 1936'' n

2.Siasa za Marekani ni '' complex and complicated''. Prof P. Navarro wa UCLA ame publish sana climate change. Alipochaguliwa mshauri wa Trump, Navarro akawa mpinzani wa climate change.

TVA ina vitu vingi ndani, hoja ya wanaharakati ni uharibifu wa mazingira, si unafuu wa umeme

Siasa za Marekani zinategemea masilahi. Obama alizuia Iran NUKE deal kwa mkataba.
Trump akafuta mkataba. Obama alikuwa against war. Trump alikuwa pro BB Nyahu.
Katika hali zote objective ni moja kumlinda Israel na ''maadui' au majirani kama Iran na Egypt

3. Egypt na US zina masiahi yanayolenga amani ya Israel. US wanaunga mkono Egypt ''kubomoa GERD ya Ethiopia''. Mradi wa GERD utaathiri blue Nile na mwathirika ni Egypt katika kila nyanja. Vita ya GERD inalenga hapo tu

Vita kama ya GERD mbona ilitupata Tanzania?
Kuvuta maji kutoka ziwa Victoria ilikuwa vurugu kutoka Egypt.

Kama kuna jambo la kumshukuru E.Lowassa ni jinsi alivyosimamia na kuiwekea ngumu Egypt iliyotumika mkataba wa 1929 na kutaka tuchimbe visima ili wao wapate maji ya kumwagilia.

Katika sakata la maji ya Victoria , US ilijifanya msuluhishi lakini ilikuwa upande wa Egypt
Ndicho chanzo cha kuanzishwa kwa NBI (Nile Basin Initiative)

4. China kutoa Billions hailalishi mradi. Pesa ni mkopo, mbinu ya China kupata malighafi na masoko ya Afrika. Hoja kwamba China ingalikataa kama JNHPP ni mradi mbaya haina mashiko.

5. Njia za kisayansi: Hatuna sera za kitaifa za nishati. Mpango wa gesi nishati na matumizi ya ndani umeishaje, ghafla JNHPP. Tungetumia njia za kisayansi tungefanya yote kwa mpangilio.

6. Wanharakati: Wanalaumiwa ingawa tunajua ukweli. Mtera na Kidatu yanajaa mchanga kwasababu ya shughuli za binadamu ikiwemo kuharibu vyanzo vya maji. Upatikanaji wa mvua unaathiriwa na deforestation. Tunatumia njia gani kuondoa hali hiyo isije kujirudia JNHPP?

7. Hoja ya wanaharakati ni athari katika eco-system. Nimesoma hoja za tafiti sijaona hoja mbadala zinazopinga. Ninachokiona ni hoja kutoka mtaa wa Lumumba katika lahaja za mashari na tungo.

Naamini ''Hydro power'' ni sehemu ya suluhisho la matatizo yetu na tulijadili miaka mingi hapa JF.
Ninapinga approach ya kukomoana. Tulibadilikaje usiku mmoja kutoka gesi na kwenda JNHPP?
Je, kulikuwa na mjadala wa kutosha na maandalizi ?
kilichotokea ni kama kile cha Bandari ya Bagamoyo '' knee jerk reaction'

Tuna matatizo yetu, bahati mbaya tupo katika denial. Miaka 60 tunasingizia influence za nje
 
Kwa faida ya nchi
The valuation purpose should be; to ensure projects costs and benefits are fully reflected in the process of project appraisal, addressing the balance between quantifiable and non quantifiable benefits, narrowing the scope of "pure"judgement; lakini we cannot pretend that all or even most effects can be captured in economic or financial values, providing a better indicator of economic performance, at the same time clarifying the gainers and the loosers from projects and last but not least providing more secure basis for resources policies such as polluter pays principles, or carbon market framework including taxes.

The major reasons of not relying on classical economic investiment criteria is because market fails due to presence of externalities, expounding this; people are not aware of the costs when they use environmental goods including both non renewabls like oil, coal and gas or renewables for istance water, air solar and hence no account is taken of their costs and benefits if only private i.e investiments benefits are considered without considering the social costs including pollution.

Decisions are viable not only based on financial analyeses such as IRR but IFF the development cost considers TEV i.e Total Economic Value defined as Direct Value + Indirect Value + option value + Existence Value + Bequest Value simply put this way proceed if (BC- CP- BP) > 0 and do not if < 0 meaning when the Scial values are greater than private values. TEV is therefore the total.value of the asset left as a natural environment

Hydro electricity only uses water to move the turbines which generate electricity thereafter the water is released back to its natural form to continue with its roles as it was before to provide its associated ecosystem values unlike other sources whereby ecosystems are impaired; the only cost of it is during construction (high investiment costs at the beggining) which can as well be easily mitigated because most of the things have alternatives. It is therefore a most sustainable option when compared to the available alternatives...The high investment cost is mitigated through low discounted future since its a life time investiment.
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA nimelisoma bandiko lako kwa umakini.

1. Nimsahihishe Stuxnet bandiko#53. Stigler's Gorge haikuanza na Mwalimu, ilikuwepo' 1936'' n

2.Siasa za Marekani ni '' complex and complicated''. Prof P. Navarro wa UCLA ame publish sana climate change. Alipochaguliwa mshauri wa Trump, Navarro akawa mpinzani wa climate change.

TVA ina vitu vingi ndani, hoja ya wanaharakati ni uharibifu wa mazingira, si unafuu wa umeme

Siasa za Marekani zinategemea masilahi. Obama alizuia Iran NUKE deal kwa mkataba.
Trump akafuta mkataba. Obama alikuwa against war. Trump alikuwa pro BB Nyahu.
Katika hali zote objective ni moja kumlinda Israel na ''maadui' au majirani kama Iran na Egypt

3. Egypt na US zina masiahi yanayolenga amani ya Israel. US wanaunga mkono Egypt ''kubomoa GERD ya Ethiopia''. Mradi wa GERD utaathiri blue Nile na mwathirika ni Egypt katika kila nyanja. Vita ya GERD inalenga hapo tu

Vita kama ya GERD mbona ilitupata Tanzania?
Kuvuta maji kutoka ziwa Victoria ilikuwa vurugu kutoka Egypt.

Kama kuna jambo la kumshukuru E.Lowassa ni jinsi alivyosimamia na kuiwekea ngumu Egypt iliyotumika mkataba wa 1929 na kutaka tuchimbe visima ili wao wapate maji ya kumwagilia.

Katika sakata la maji ya Victoria , US ilijifanya msuluhishi lakini ilikuwa upande wa Egypt
Ndicho chanzo cha kuanzishwa kwa NBI (Nile Basin Initiative)

4. China kutoa Billions hailalishi mradi. Pesa ni mkopo, mbinu ya China kupata malighafi na masoko ya Afrika. Hoja kwamba China ingalikataa kama JNHPP ni mradi mbaya haina mashiko.

5. Njia za kisayansi: Hatuna sera za kitaifa za nishati. Mpango wa gesi nishati na matumizi ya ndani umeishaje, ghafla JNHPP. Tungetumia njia za kisayansi tungefanya yote kwa mpangilio.

6. Wanharakati: Wanalaumiwa ingawa tunajua ukweli. Mtera na Kidatu yanajaa mchanga kwasababu ya shughuli za binadamu ikiwemo kuharibu vyanzo vya maji. Upatikanaji wa mvua unaathiriwa na deforestation. Tunatumia njia gani kuondoa hali hiyo isije kujirudia JNHPP?

7. Hoja ya wanaharakati ni athari katika eco-system. Nimesoma hoja za tafiti sijaona hoja mbadala zinazopinga. Ninachokiona ni hoja kutoka mtaa wa Lumumba katika lahaja za mashari na tungo.

Naamini ''Hydro power'' ni sehemu ya suluhisho la matatizo yetu na tulijadili miaka mingi hapa JF.
Ninapinga approach ya kukomoana. Tulibadilikaje usiku mmoja kutoka gesi na kwenda JNHPP?
Je, kulikuwa na mjadala wa kutosha na maandalizi ?
kilichotokea ni kama kile cha Bandari ya Bagamoyo '' knee jerk reaction'

Tuna matatizo yetu, bahati mbaya tupo katika denial. Miaka 60 tunasingizia influence za nje
Asante Nguruvi3 kwa sahihisho ambalo tayari nimelifanyia editing na hongera kwa kwenda deep.
 
Tumewachoka wote na wamelewa na madaraka ya kulevya hawana msimamo
 
Mkuu maelezo yako mbona yako wazi kabisa yanaeleweka…hakuhitaji rocket science kutambua hapo ni vita za kiuchumi…

Big corp wanataka kuuza mafuta na gas na mazao yao mengine….leo upunguze mpunga watakuelewa….kujitegemea ni adui mkubwa wa ubepari…

Hv mazingira vs faida itakayopatikana kwenye jamii na serikali kwa ujumla wamezipima…maana mimi ninachojua Kilimanjaro kule mito imekauka sio kwasababu ya mabwawa….watu wanakata miti misituni kutengeneza mikaa na mengineo…na bado wanawasha vibatari vya mafuta ya taa kukwepa gharama za umeme…umeme ni anasa…mtu akitaka kufungua mradi unaotumia umeme inabidi atafakari anafanyaje ili aweze kupunguza gharama ili bidhaa zake ziuzike…
Mi nakwambia chunguza tu, adui wa Afrika ni mwafrika mwenyewe, viongozi wa kiafrika wanatumika kuhujumu mataifa yao wenyewe, unlike hao wazungu ambao wana uzalendo na mataifa yao na siku zote wanafanya mambo for the next generation. Sisi huku ni very unfortunate.

Mimi hii habari ya kulaumu mabepari nshaacha, domestic enemies are the worst, mtu bila haya anahujumu taifa lake na vizazi vijavyo, hajali hatakuwepo probably in the next 20,. 30 years, kikubwa fimilia yake ifaidi, ujinga kiasi Gani huu kwa sisi watu weusi, in a long run tutakuja kuuwana sababu matatizo yatakuwa mengi maisha yatakuwa magumu ndio kitakachofuata in the next few years. Binadamu akiwa na njaa ni hatari zaidi ya Simba, ni swala la muda tu. Sababu watu watataka kuwatoa hao wanasiasa na wao wataona Kama wanahaki ya kutawala, ndio balaa litakapokuja.
 
Huu mjadala ushapitwa na wakati, mradi ushajengwa zaidi ya nusu sasa na unaendelea kujengwa mpaka ukamilike. Iwe white elephant au usiwe, haibadilishi kitu.

Sasa hivi labda tujadili namna gani wanaweza kuumaliza kwa haraka zaidi, kwa nafuu zaidi na namna gani tutamaximize manufaa huku tukitunza mazingira na maisha ya wanaotegemea mto Rufiji.

Let's think forward kuliko kurudi nyuma kila siku.
 
Kwa zote mbili umeme wa hydro will always rank high and be a best option against any other possible and available alternative inayojulikana kwa sasa...Unless huna comparative advantage za landscape na flows....Hakuna jinsi iwe ki ecology au ki economics umeme wa gas ukaukaribia hata kwa mbali ule wa hydro...

Tatizo la sisi ni policies zetu ambazo zina much influence kutoka kwa waliotutawala UK na mshirika wake USA ambao so far duniani zaidi ya kuwa wafanya mauaji ya kivita hawafui dafu kwa taifa lolote....Welfare zao ni mbovu na economic policies zao ndizo hasa zilizotufikisha hapa tulipo leo kwenye degradation ya hali ya juu ya mazingira.

Ni ajabu sana kwaini hatuzi abandon hizo failed economic policies zao...Sustainable development haiangalii hizo factors unazozitaja bali welfare ni kitu cha kwanza; huko kwenye nchi hizo mbili welfare ni mbovu na poverty gap ni kubwa miongoni mwa walionacho na wasionacho kuliko other EU countries ambazo nyingi zina policies zenye kuzingatia welfare zaidi i.e social benefits against private benefits. Kinara wa hizo ni Scandnavia na dunia yote inaelekea huko ni sisi tu ambao tunajidanganya yet siasa yetu ya ujamaa na kujitegemea inafanana sana na hizo EU countries nyingine including zisizo kuwepo EU but ni za Europe.

Hao ndiyo ambao wali comoditize education mpaka tukaanza kupata ma degree fake fake; hawa ndiyo vinara wa ufisadi duniani kupitia multi national companies, hao ndiyo ambao wanaojitahidi sana kushikilia mifumo ya dunia lakini pumzi zina akaribia kuwaishia...Let be watchful, economics ya projects za leo na financial analyses hazipo katika hizo investiment criteria za kizamani, tumeshaondoka huko, what is financially expensive can be very cheap and sustainable if given a low discount rate based on those extenalities unazozielezea mojawapo ikiwa social costs ambazo private firms haiziingizi kwenye cost functions zao; get your facts right nigga!

Asante sana kwa ufafanuzi, dunia kwa sasa inatoka kwenye unyang'anyi na kuelekea kwenye ''an all inclusive welfare of citizens''. Miaka nenda miaka rudi makampuni yalikuwa yakitengeneza faida kubwa kwa hasara ya wengi. Mfano kwenye makampuni ya uzalishaji, sikuhizi yanalazimishwa kuwa na sera za ESG. Kwa sasa hata unavyofanyiwa corporate rating wakiona you are non concerned with environment, social and governance you will score poorly.

Tukija mradi wa JNHPP una faida nyingi sana kuliko hasara (hatukatai kwamba hauna hasara. Hilo lipo kwa kila mradi). Faida ni kama ifuatavyo; 1. Climate smart project 2. Will produce power at affordable cost. 3. The water body created will be ideal for fishing, navigation, other innovated uses. 4. Tourism attraction. 5. Improved security over the area.
 
Mkuu nakusoma vizuri kabisa, hili la kuangalia Financial Viability nimelizungumzia kule juu kwenye mradi wa Tennessee Valley Authority (TVA). Mahakama ya Juu ya Marekani (The US Supreme Court) ilizungumza kama ulivyoweka bayana hapa. Nikushukuru sana ndugu yangu kwa mchango wako mzuri ?

Ubarikiwe kiongozi,
watu wengi wanashindwa kuelewa ya kwamba miradi yote ya kimkakati (strategic investments/projects) kama madaraja, barabara, viwanja vya ndege n.k. faida zake haziangaliwi kwa upande mmoja tu wa finacial viability (nasisitiza). Kuna mambo luluki ya kuangalia. Baadhi nimetaja.
 
Wazungu husema hivi "Once is an accident, Twice is a Coincidence, but Thrice is a Pattern".

Hapa namaanisha nini, duniani kote ambako miradi ya namna hii yenye lengo la kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umasikini lazima kuwepo na malalamiko.

Tena nimefuatilia kwa umakini na kufahamu kwamba malalamiko hayo ni lazima yafanane. Mbaya zaidi makundi ya wanaoleta haya malalamiko huwa ni ya watu wa aina ileile, tena huja na sababu zilezile.

Ukifuatilia kwa umakini, utatambua kwamba mfanano wa hawa watu ni mkubwa sana hadi utakubaliana na ule msemo wa kiingereza kwamba "History does not repeat itself, but people do repeat themselves".

Fanya utafiti wako binafsi, utakubaliana na nilichokiandika hapa.

Muda ni mchache, leo hii ntazungumzia nchi tatu ambazo ni Marekani, Ethiopia na Tanzania. Ambako kote katika nyakati tofauti kumekuwa na miradi mikubwa ya kuzalisha umeme wa maji ambao kwa mkono wa serikali, ambayo imelenga kuzalisha umeme wa gharama nafuu kwa wananchi huku miradi hiyo ikiendeshwa na serikali.

Hapa nazungumzia miradi ya The Tennessee valley Hydro-electric Power Projects (TVA), The Grand Ethiopian Rennaisance Dam (GERD) na Julius Nyerere Hydro- Power Project (JHPP).

Nimefuatilia kwa karibu nimeona kwenye hii miradi ya TVA, GERD na JNHPP ni lazima utakutana na majina kama WHITE-ELEPHANTS, DEBT-RIDDEN PROJECTS, UNSUSTAINABLE ENERGY SOURCE, ENVIROMENTAL HAZARDOUS, GOVERNMENT MONOPOLY, UNCOMPETITIVE SOEs na SOCIALIST EMBARKED PROJECT.

Mpaka sasa sijafahamu kwanini tokea kule Marekani, Ethiopia hadi Tanzania mambo yafanane hivi. Imetokea TVA (Once=An Accident), Imetokea GERD (Twice= A Coincidence) na Imetokea Tanzania (Thrice= A Pattern).

Pia sehemu nyinginezo yanaendelea kutoka tu, mpaka najiuliza nini hiki. Labda, huenda ni mawazo yangu hafifu tu, ambapo wazungu husema "A figment of your own imagination"

HEBU TUANGALIE MRADI WA UMEME CHINI YA TENNESSEE VALLEY AUTHORITY

Raisi Franklin Delano Roosevelt alianzisha The Tennessee Valley Authority (TVA) mwaka 1933 ili kuwezesha Marekani izalishe umeme wa bei ndogo ambao utasaidia majimbo kama saba ambayo yanazunguka lile eneo.

Lengo kubwa ni kusaidia kiuchumi ukanda ambao uliachwa nyumba kimandeleo, kutoa ajira kwa vijana na kusukuma uchumi wa viwanda eneo hilo.

Tokea mwaka 1933 mpaka sasa Marekani imefanikiwa kutengeneza mabwawa 50 ambayo yanasaidia kuzalisha umeme wa bei ndogo unaotumika kuendesha viwanda na uchumi wa majimbo karibia saba ya eneo ambalo bonde la Tennessee limepita.

Ila huwezi amini mpaka leo hii mwaka 2022, wanaharakati wa kimazingira wanapinga huu mradi kwa kusema unaleta madhara.

Wakati nasoma shule kuhusu huu mradi, tuliambiwa kwamba ulipigwa vita sana na makampuni binafsi ya umeme, wanasiasa, wanaharakati na wanasheria.

Ambapo walitumia mbinu mbalimbali kufanikisha hujuma dhidi ya huu mradi lakini hawakufanikiwa. Sababu kubwa ni kwamba raia wengi wa Marekani walikuwa ni watu wanaojielewa mno, siyo wajinga wanaopelekeshwa bila kufahamu linaloendelea (Dumbed-Down Citizenry) nchini kwao.

Upinzani haukishia kwenye uanzishwaji wa huu mradi mwaka 1933, mwaka 1936 mmoja wa wamiliki wa hisa kwenye kampuni binafsi la umeme THE ALABAMA POWER COMPANY aitwaye ASHWANDER alipeleka kesi mahakamani kuzuia serikali kuuza umeme kupitia The Tennessee Valley Authority (TVA) akisema kwamba serikali haitakiwi kabisa kuuza umeme hivyo kuna uvunjifu wa katiba ya Marekani.

Unaweza kutafuta kesi ya: Ashwander V Tennessee Valley Authority (1936)

Mahakama ya juu ya Marekani ilikataa na kusema uzalishaji huu wa umeme siyo wa faida tu, bali ulilenga kutoa huduma kwa kukuza uchumi wa eneo ambalo lilikuwa nyuma kimaendeleo na kuimarisha ulinzi wa nchi kwasababu viwanda vya silaha vilikuwepo eneo hilo.

Hivyo mabwanyeye wakapigwa chini na serikali inauza umeme kwa raia mpaka leo hii. Ikumbukwe inayofanya hivi ni serikali ya Kibeberu ya ulimwengu wa kwanza na siyo serikali ya Kijamaa ya ulimwengu wa tatu.

Wamarekani zaidi ya milioni 9 wanapata huduma ya umeme nafuu kutoka kwenye miradi 29 ya umeme wa maji kutoka Tennessee Valley Authority (TVA).

Kubwa zaidi ni kwamba huduma ya umeme kwenye majimbo hayo yanayopitiwa na bonde la Tennessee ni moja kati ya umeme wenye gharama nchini Marekani, kama siyo ndiyo wenye gharama nafuu zaidi kwenye nchi hiyo.

Kitakachoshangaza watu werevu ni kwamba PROPAGANDA CHAFU na UZANDIKI dhidi ya mradi huu hazijaisha tokea mwaka 1936. Raisi Dwight Eisenhower alishawahi kuutukana huu mradi kwa kuuita maneno kama "Ujamaa nyemelevu" (Creeping Socialism), ilhali mamilioni ya Wamarekani ni wanufaika.

Maneno kama haya hayatakiwi kabisa kutoka kwenye kinywa cha mkuu wa nchi mwenye lengo la kuwakwamua kiuchumi raia wa kawaida, kwasababu faida za mradi ni dhahiri kwa watu wote.

Lengo la Raisi Eisenhower lilikuwa siyo kupinga UJAMAA bali ni kubinafsisha (TVA), lakini akakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wazalendo wa kimarekani na mwishowe akawa mpole.

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba waliompinga ni wenzake kutoka REPUBLICAN PARTY ambao husifika kwa kuchukia UJAMAA hasa pale ambapo serikali yenyewe hufanya biashara. Nini kilipelekea Raisi na jopo la wataalamu wake kupingwa hivi ???

Sasa kubwa na baya zaidi dhidi ya mradi huu ni lile la mwaka 2013, ambapo Raisi Barrack Obama aliandaa muswada ili kubinafsisha The Tennessee Valley Authority (TVA) kwa watu binafsi.

Moja ya sababu kubwa ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ni kwamba mamlaka ya Tennessee Valley (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni mzigo kwa serikali.

Walikuwa na hoja nzito sana maana ukweli ni kwamba mamlaka hiyo (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni takribani dola za kimarekani bilioni 25.

Lakini hili halikuwa sababu ya kusema kwamba serikali ibinafsishe shirika hili la kiserikali na kuwaumiza raia wapatao milioni 9 kwa kupanda kwa gharama za umeme.

Sababu ya pili ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ili kufanikisha ubinafsishwaji wa The Tennessee Valley Authority (TVA) ni ile ambayo hata kwetu huku inatusumbua ya kutunza mazingira.

TVA mbali na miradi 29 ya umeme wa maji, imeongeza pia miradi 12 ya umeme wa makaa ya mawe, miradi 3 ya umeme wa nyuklia, miradi 15 ya umeme wa gesi na mradi 1 wa umeme wa upepo.

Inasemekana TVA inahitaji dola za kimarekani bilioni 25 ili kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababisha na huu mradi hasa kutoka kwenye vinu vya makaa ya mawe. Hivyo ili serikali isiingie kwenye hizi gharama zisizo za msingi, basi ni kheri ibinafsishe tu shirika hili.

Kuna nchi fulani hivi viongozi wake, wasomi na wafanyabiashara wanapenda kuzungumza kauli kama hizi za Raisi Barrack Obama na Dwight Eisenhower, bila shaka ndugu msomaji utakuwa unaifahamu.

Hivyo njia rahisi kwa Serikali ya Raisi Obama, kukwepa deni kubwa la TVA na gharama za marekebisho, wakaona ni bora wauze hii SOE (State Owned Enterprise).

Ila ukweli mchungu ni kwamba wangefanya hivyo ina maana gharama za umeme kwa wananchi wa Marekani zaidi ya milioni 9 ingepanda sana na wangeathiri biashara nyingi na maisha ya raia wa kawaida.

Mbali na madhaifu yake mengi, Marekani ni taifa ambalo raia wake wengi wanajielewa mno.

Wahafidhina wa chama cha REPUBLICAN hasa wawakilishi kutoka majimbo hayo, pamoja na watu binafsi walipinga kwa nguvu mswada ambao ungefanikisha ubinafsishwaji wa kiholela wa hii mamlaka ambayo lengo lake kuu ni kutoa huduma kwa raia na kuimarisha ulinzi wa nchi.

HEBU TURUDI NCHINI TANZANIA SASA, TUANGALIE TANESCO NA JNHPP

Bunge la Marekani lilichofanya ni kukataa mamalaka isiuzwe na kuiwekea ukomo wa deni, ambayo mamlaka haitakiwi kuvuka, ambapo ukomo ni dola za kimarekani bilioni 30.

Hivyo madeni hayapo tu kwenye shirika letu la TANESCO lakini hata TVA wana madeni tena yanakera. Sisemi haya kusema TANESCO inafanya vizuri, la hasha kuna mambo mengi ya ajabu yanafanyika.

Lakini naamini wakijipanga vizuri na kupunguza siasa tunaweza kufika sehemu nzuri sana. Mbona TVA wafananya vizuri na bado ni shirika la serikali ???

Jambo jingine ambalo nalisikia sana nchini Tanzania ni hilo la kusema umeme wa maji siyo endelev. Mimi siyo mtaalamu lakini naweza kufahamu wapi nadanganywa, kiukweli hili linanipa ukakasi mkubwa sana.

Mradi wa TVA umeanza mwaka 1933 na upo hadi leo hii, utasemaje kwamba umeme wa maji siyo endelevu jamani ???

Unaweza kumtukana Raisi Magufuli kwamba ni mjinga, lakini kumbuka huu mpango wa JNHPP umekuwepo tokea enzi za Mzee Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, ina maana hawa wote na wataalamu wao walikuwa ni wajinga kabisa wasitambue kwamba Hydro-Electric Power is not sustainable source of energy ??? Aidha ni kweli sisi watanzania ni watu wajinga sana pamoja na viongozi wetu, AU kuna kitu kinachoendelea nyuma ya pazia sisi raia wa kawaida hatukioni.

Jambo kubwa zaidi la kujiuliza hapa: Ni kwamba kama mradi wa TVA ambao manufaa yake yanaonekana kwa mamilioni ya wananchi wa Marekani unapigwa vita kali hivi, tena hadi na viongozi wa serikali wakiwemo maraisi, sisi huku kwetu Tanzania tusipingwe kweli ???

Mwaka jana miezi ya mwishoni nilikuwa nafuatilia wanaharakati mitandaoni, nikasikia baadhi wakisema mamilioni ya miti yamekatwa na uharibifu mkubwa wa mazingira umefanyika kwenye mradi wa JNHPP ndiyo maana mvua zimegoma Tanzania.

Lakini, wengine wanasema kwamba JNHPP ni tembo mweupe (A White Elephant Project). Majibu ya Waziri Makamba, yamakuwa yakibadilika-badilika. Lakini naamini, ukweli tutaufahamu tu.

Wanaharakati wetu wangepinga huu mradi (JNHPP) peke yake sisi tungeelewa labda na binafsi ningesema hebu tujifanyie tathmini. Lakini hakuna mradi wowote mkubwa ambao umewahi kufanyika nchini Tanzania bila kupata upinzani mkubwa:

Uwe ni mradi wa msaada, uwekezaji au mkopo. Nasema hili kwa UJASIRI WOTE, kama upo naomba nitajiwe ili nijifunze.

Ukifuatilia kinachoendelea kwa wanasiasa wetu kuna sababu nyingi sana zinazoletwa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Wengi wetu ni UJINGA, WOGA, BENDERA FUATA UPEPO lakini kubwa ni ULAJI TU wa watu wachache ambao wamevaa ngozi ya kutunza mazingira, kulinda katiba, matumizi ya mbinu za kisasa za kisayansi na kibiashara kuendesha sekta ya nishati nchini. Lakini ni hivi: UKWELI UKO KAMA MIMBA, HUWEZI KUUFICHA MILELE. Tutafamu tu...

NAMALIZIA NA ETHIOPIA, MRADI WA THE GRAND ETHIOPIAN RENNAISANCE DAM

Ingekuwa Tanzania ndiyo nchi pekee ndiyo inayopigwa vita kwa kuanzisha mradi kama huu ningesema, basi tujifanyie tathmini kidogo.

Ila hadi kule kwa ndugu zetu Ethiopia yametokea machafuko makubwa sana kupinga uanzishwaji wa The Grand Ethiopia Rennaisance Dam (GERD) ambalo litakuwa msaada mkubwa sana kwa mamilioni ya wahabeshi nchini humo.

Upinzani umekuwa mkubwa imefika kipindi kwamba Raisi wa Marekani Donald Trump akaweka bayana kabisa kwamba Misri inaweza kulipua bwana hilo" Egypt might blow up the dam".

WIKILEAKS wanasema kwamba, mradi huu ukimalika hautaisaidia Ethiopia peke yake kuzalisha umeme wa bei ndogo, bali utazalishwa umeme mwingi (Megawatts 5,250) ambao utauzwa hadi nchi jirani kama Sudan na serikali ya Sadani inafahamu hili vizuri kabisa.

Sasa ukifuatilia kwa umakini, kuna wanasiasa wakubwa ambao walisema wazi kwamba mradi wa GERD, hauna manufaa na ni tembo mweupe ( A WHITE ELEPHANT). Moja kati ya watu waliowahi kusema hivi ni Raisi Isaias Afwerki wa Eritrea.

Lakini mradi huu ukikamilika, umeme wa gharama nafuu utafika hadi nchini kwake. Watanzania tujiulize kitu hapa: Kama umeme wa maji siyo wa muda mrefu (Not Sustainable), hivi iweje serikali ya Uchina itupe zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1, ambazo ni sawa na trilioni mbili za kitanzania au zaidi kwenye mradi ?

Asasi za kiraia (NGOs) nazo haziko nyuma katika kutuonesha madhara ya mradi huu wa GERD. NGO maarufu iitwayo INTERNATIONAL RIVERS kutoka California, nchini Marekani iliandaa ripoti kubwa kabisa kuonesha madhara ya mradi huo kwenye mazingira. Wakaenda mbali zaidi na kusema kwamba bwana hili linaweza kuchangia mabadiliko ya hali ya nchi.

Ikumbukwe hawa ndugu zetu wamezungumza sana juu ya miradi ya umeme wa maji nchini Tanzania na Ethiopia.

MWISHO KABISA: MAONI YA WANAZUONI KUHUSU SIASA ZA UMEME NA MABWAWA

Kama umefuatilia siasa za Afrika kwa muda mrefu, utatambua kwamba huu mchezo haujaanza na Tanzania wala Ethiopia. Prof Mike Muller ambaye ni mhandisi kutoka chuo cha Witswatersrand Afrika Kusini, amawahi kuandika na kusema siasa za kupinga miradi mikubwa ya umeme wa maji zilianza mapema nchini Misri kipindi cha Gamal Abdi Nasser ambapo alitaka kujenga bwawa la Aswan (ASWAH HIGH DAM) ambalo lingezalisha MegaWatts 2,100.

Prof Asit K. Biswas amtaalamu wa maji na mazingira, ambaye ndiye anaongoza kwa kufanyiwa rejea za kitaalamu linapokuja suala za mazingira na maji, akishirikiana na Prof Cecilia Tortajada waliandika chapisho ambalo limesema kwamba mradi wa BWAWA LA ASWAN una madhara makubwa kwenye mazingira.

Lakini ukweli ni kwamba wataalamu mradi huo ulipokamilika mwaka 1970, ulikidhi nusu ya mahitaji ya umeme nchini Misri.

Ikimbukwe kwamba siasa za ASWAN HIGH DAM ziliwahi kupelekea Misri ivamiwe kijeshi na Uingereza, Ufaransa na Israeli. Nasser alisema alitaifisha Mfereji wa Suez kwasababu maji yake ni muhimu kwa ujenzi wa bwawa la Aswan.

Nasser aliomba msaada kwa serikali ya Raisi Eisenhower ili kujenga bwana la Aswan, lakini Eisenhower aligoma.

Raisi Kennedy alikosoa sana haya maamuzi ya kuvuruga miradi ya Afrika akisema hivi "When we abruptly abandoned the Aswan Dam in Egypt, the Russians went ahead to finance it. While we starve the Development loan Fund, the Sino-Soviet bloc has already passed us in economic assistance to selected key areas" Hili ndilo lilitokea bwawa lilijengwa na Warusi.

Maajabu barani Afrika huwa hayaishi kabisa: Kinachotushangaza wengi wetu leo hii ni kwamba Misri ambao miaka ya nyumba walionewa katika kujengwa bwawa la Aswan (ASWAN HIGH DAM), leo hii wao nao wakishirikiana na mataifa makubwa nje, wanaharakati na asasi kubwa za kiraia, wanafanya hujuma kubwa sana dhidi ya mradi wa GERD nchini Ethiopia.

NB 1: Siasa kama hizi, zilionekana pia kule nchini GHANA kipindi cha marehemu Nkhrumah ambapo alikuwa anataka kujenga bwawa la AKASOMBO (The Akasombo Dam) ili kuzalisha umeme.

Uliundwa mtandao mkubwa sana wa watu ndani na nje ya nchi ili kumzuia. Muda ni mchache sana siwezi kuzungumza kilichotokea.

NB 2: Fanya utafiti wako kuhusu miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kupitia maji (TVA, GERD, JNHPP) pia hata ASWAN HIGH DAM na AKASOMBO DAM utatambua kwamba siasa zake zinafanana.

Wahusika ni walewale, wakitumia mbinu zilezile, sema tu huja wakiwa wamevaa vingago (Masks) tofauti-tofati. Kiufupi hizi siasa zinachezwa sana kitaalamu na wengi wetu tunafuata upepo bila kufanya tafiti binafsi.

Mimi siyo mtaalamu sana wa haya mambo, hivyo naomba wale wajuvi wanisaidie zaidi kuelewa. Nitafurahi kurekebishwa na kuelekezwa pale ambapo nimepotoka na kutofahamu kinachoendelea.

CC: JokaKuu , Nguruvi3 , UmkhontoweSizwe , TUJITEGEMEE
Sasa mtu kupingana na andiko lako lazima aje na hoja zenye tafiti kama wewe na si porojo.

Always nchi hukwamishwa na maadui wa nje kupitia wananchi wenzetu hasa kupitia kichaka cha harakati. Hawa wanakuwa funded fedha nyingi kwa njia ambazo huwezi kuwapata namna wanavyo inject hizo fedha maana hutumia mbinu kubwa wakisaidiwa na taasisi zao za kifedha.

Tatizo namna Taifa lilivyoandaliwa kupigana vita ya namna hii. Hata hapa wengi wataliangalia kusiasa kuliko jicho la ziada.
 
Mbona jibu lipo wazi? Angepata wapi finances zakuujenga kama asingechukua huo wa kibiashara usio na masharti magumu zaidi ya riba?

We ukaombe pesa kwa mtu anayekugomea kujenga mradi hata kwa pesa zako? Wangempa? Mbona hii ipo so direct huhitaji hata kufikiri sana?

Mradi huu wa umeme wa maji hata riba ingekuaje kwa jinsi alivyouweka ulikuwa siyo exclusive ungeweza kujilipa na baadaye kujiendesha vizuri tu na kwa manufaa ya taifa. Hii ni kwasababu ulikuwa planed naukawa linked with other projects kama za viwanda ambavyo ulisikia kila mara akiviongelea vinajengwa na alisisitiza vijengwe pamoja na kuboresha kilimo nadhani ilikuwa ni baada ya kumaliza hizi project kubwa kubwa. Zote hizi zikichangizwa na ujengaji miundombinu ya usafiri ambazo kwa pamoja zingeipeleka production function ya nchi juu sana kwakukutoa formal employments kwa milions of youths ambao wangeinua pato la taifa through spending kupitia salaries zao ambazo ni determined na siyo probable kama wangejiajiri au kuishia kuwa street hawkers ambao kwanza wanauza vitu cheap kutoka mataifa ya nje na hasa China na ku spend kwa basic service kama nauli na hospitali tupo, ambapo dawa zinatoka nje na mafuta ya transport yanatoka nje pia iki imply hasara i.e capital flight, huku local products kama crops zikikosa soko kwakua watu hawana vipato. Besides, kupitia payee zao hao (formally employed youth) tax base ingeongezeka na kupelekea kuongeza uhakika wa mapato ya serikali badala ya kukimbizana na tozo.

Ni kwavile tu watu wanaangalia miradi kwa jicho la faida binafsi lakini taifa lolote lile ili lilete mageuzi ya haraka mambo ya msingi ni energy na infrastructure kama base then ndiyo production inayokuwa subsidized inafuatia baada ya hapo ili kujenga uwezo, kisha baada ya hapo zinakuwa released kuongeza efficiency through competition. Competition huruhusiwa baada ya frame nzima kutokea kuanzia farm gate productions, intermediaries i.e wafanya biashara na wasafirishaji kuji organize mpaka final consumption kwa maana ya market chains; ndipo basi huko mbeleni third phase, ndiyo mambo ya value addition, quality, standardization and specifications zenye linkages both vertical and lateral kuenda kwenye cluster value chains formation hufuata, hatimaye kuwa full developed economy kama za wenzetu; which means base au foundation ikiwa nzuri, kitu ambacho JPM alikuwa ndicho anakijenga, value addition and flows zake through chains and other channels .ie lateral inakuwa ni outcome ya automatic.

Kwa mtizamo wangu; Magufuli alikuwa ana maono mazuri na yenye tija kubwa kwa taifa letu, TATIZO KUBWA SANA, alitumia common sense zaidi na pengine alikosa programmers wazuri either kwakua hawapo wakutosha ama waliokuwa karibu naye walikuwa wababaishaji au alikuwa mbishi asiyependa kusikiliza, sijui sana sababu hapa na speculate tu....Pia nadhani alikosa watu ambao wanaelewa vizuri maono yake ambao wange weza kuyabeba hayo baada yake, leo tusingekuwa na shida ya kuona mwendelezo usio na confusion ndani yake...

Hata hivyo bado kama taifa tunaweza kukubali kukaa na kuelewa hayo maono na kuyapeleka ili sote tufaidike kuliko kila mara kuanza moja kila mara uongozi unapogeuka...

Thanks for a very balanced opinion.
 
Wote wanao upinga mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere ni wezi tu, wanataka tuwe na umeme wa kuunga unga ili zile kashfa za Escrow, Dowans, IPTL ziendelee kuwepo cause kuna baadhi wanafaidika nazo, hawataki umeme ambao ni sustenable; kila wakati watu wanwaza pesa za uchaguzi. Magufuli aliisha twambia hata kilicho kua kinafanyika Mtera, kumbe issue wala sio maji kua machache, maneno hayo hayo yanafanana na maneno ya aliyewahi kua waziri wa nishati na madini kwa muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 mwana George John Simbachawene, alizungumza the same thing tena bungeni, na ndio kinacho endelea hata sasa hivi. Imagine miaka 6 mfululizo utawala wa Magufuli hakukua na mgao wa umeme kabisa, Kalemani ameendelea vizuri tu hadi alivyo badirishwa, kabadirishwa tu, hata mwezi haukuisha, umeme ukaanza kua wa shida.
 
Huu mjadala ushapitwa na wakati, mradi ushajengwa zaidi ya nusu sasa na unaendelea kujengwa mpaka ukamilike. Iwe white elephant au usiwe, haibadilishi kitu.

Sasa hivi labda tujadili namna gani wanaweza kuumaliza kwa haraka zaidi, kwa nafuu zaidi na namna gani tutamaximize manufaa huku tukitunza mazingira na maisha ya wanaotegemea mto Rufiji.

Let's think forward kuliko kurudi nyuma kila siku.

Pia its sustainability.
 
Back
Top Bottom