Ndugu yangu
MALCOM LUMUMBA
....Long time no see!!
Kwa heshima ya ndugu
Jinga la Zamani alienialika, wacha nami niseme machache.
Hapa wacha niende moja kwa moja kwenye JNHPP ili nisiifanye post yangu kuwa ndefu maradufu..
Kwa hapa tulipofikia, hatuwezi kuendelea na yale mambo ya ku-abandon miradi mikubwa wakati tayari imeshameza mabilion ya pesa! Kwa maana nyingine, JNHPP Must Continue kwa sababu tayari pesa nyingi imeshaingia!!
Hata hivyo, wakati mradi huu unaanza binafsi niliupinga! Sikuupinga kwa sababu za kimazingira wala kwamba ni unsustainable lakini mimi ni muumini mkubwa wa Economic
Multiplier Effect na Optimal Resources Allocation.
Dhana hii ya Multplier Effect nishaieleza sana huko nyuma! Na kwavile I believe in Multiplier Effect, kama ningewekewa option ya either JNHPP or LNG Project (Gas Industry) kama source ya uzalishaji umeme, I'll ALWAYS be in favor of the Gas Industry kwa sababu huko kuna HIGHER multplier effect kulinganisha na umeme wa maji!!
There's no match between the two!
Bidhaa Kuu kutoka JNHPP ni UMEME PEKEE, and there's little (if any) to no by-products zinazoweza kuzalishwa kupitia JNHPP! Kinyume chake, Bidhaa Kuu ya LNG Project ni Gas na sio umeme lakini hapo hapo unaweza pia kupata UMEME + TAKATAKA ZINGINE!
Kumbe basi, 99% ya Multiplier Effect inayoweza kupatikana kupitia JNHPP pia inaweza kupatikana kutoka LNG Project. Kinyume chake, mengi unayoweza kupata kupitia LNG Project HUWEZI KUYAPATA kupitia JNHPP!
JNHPP itatupatia tu UMEME utakosaidia ku-boost sekta zingine za kiuchumi na labda kufanya Electricity Export but only regionally. Multiplier Effect tunayotarajia hapa inaweza kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji kwa sababu tutakuwa na umeme wa uhakika.
Hata hivyo, YOTE hayo pia unaweza kuyapata kupitia LNG Project...
Wakati hali ni hiyo kwa KNHPP, LNG Project inaweza kukupatia AT LEAST yafuatayo:-
1.
Umeme... Wakati Umeme sio Main Product from LNG Project, pale JNHPP umeme ndiyo MAIN PRODUCT itakayotokana na investment husika!
Kwa maana nyingine, faida yoyote ya kiuchumi INAYOWEZA kupatikana kwenye JNHPP Project ambayo umeme wake ndio Main Product, pia INAWEZA kupatikana, tena kwa ukubwa wa maradufu kutoka LNG Project kupitia umeme unaoweza kuzalishwa ingawaje sio Main Product!
Na kama tunasema LNG Project izalishe UMEME TU basi umeme huo unaweza kutumika kote Sub-Saharan Africa tena kwa miongo kadhaa wakati JNHPP Project haina uwezo hata ku-sustain hata uchumi kama wa South Africa!
In fact, hata Kenya ukiwaambia waachane na vyanzo VYOTE vya umeme walionao na watumie umeme kutoka JNHPP tena peke yao, bado umeme huo HUWEZI kuwatosha!!
Hapa ili nieleweke labda niseme hivi: Kwa sasa Umeme wa Gas uliopo kwenye Gridi ya Taifa ni almost 57% ya umeme WOTE huku hydropower ikichangia roughly 37%! Hata hivyo, 57% hiyo inatokana na less than 7.5 Trillion Cubic Feet of Gas ambazo ndizo zimeanza kuchimbwa kutoka Songongo, Mkoani Lindi na Madimba, mkoani Mtwara! U
Ukitoa hizo 7.5 Trillion Cubic Feet of gas ambazo zimeanza kuchimbwa, kuna almost 50 Trillion Cubic Feet of gas ambazo HAZIJAGUSWA! And remember, hiyo 57% ya umeme unaozalishwa sio unatokana na full capacity ya hizo 7.5 Trillion Cubic Feet za gas... hell no!
NInachotaka kusema ni kwamba, at full capacity, hizo 7.5 Trillion Cubic Feet zinaweza kuzalisha maradufu ya umeme utakaozalishwa na JNHPP na hapo bado zile 50 Trillion Cubic Feet HUJAZIGUSA!
2.
Gas.. Hii ndiyo MAIN PRODUCT from the LNG Project. Hapo juu tumeshaona Umeme unavyoweza kuwa another product from the LNG Project, BUT...
(a)
Gas For Export: LNG ni biashara kubwa sana duniani, na kwahiyo ni EXPORTABLE Product world-wide na sio tu regionally kama tunavyoweza kusafirisha the ONLY JNHPP Product!
Watu wanaposikia Lindi inataka kujengwa LNG Plant, akili yao wanadhani ni substitutes ya JNHPP! Kwamba, lengo ni tufanye gas processing kisha gas itumike kuzalisha umeme!
Kutokana na imani hiyo ndo maana unakuta Wafuasi wengi wa JPM wanapinga sana ule mradi kwa kile wanachodhani una lengo la kufuta JPM Legacy kwenye Bwawa la Nyerere!!!
Hapa ieleweke tu kwamba HAKUNA MJINGA ANAYEWEZA KUWEKEZA USD 30 BILLION for kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa nchi maskini kama Tanzania! Hizo almost TRILLIONS 70 zinarudi rudi vipi ikiwa main product ni umeme?!
Hiyo investment inafanyika kwa sababu almost 50 Trillion Cubic Feet of UNDEVELOPED GAS ni Huge Opportunity for Export na sio eti kuzalisha umeme ili hatimae kuua Legacy ya JPM kwenye Bwawa la Nyerere!
(b)
Gas For Domestic and Industrial Use:- Asikuambie mtu... this's a huge business opportunity!
Tuchukue mfano mdogo tu wa hii tenda ambayo ilitangazwa na TPDC...
View attachment 2113381
Kabla hata hatujaingia huko kwenye gesi yenyewe, hebu tutafakari hiyo project! Yaani tunahitaji kiwanda kitakachoweza kuzalisha vifaa vifuatavyo:-
HDPE pipes, HDPE fittings, Domestic Gas Meters and associated fittings, Commercial Gas Meters and associated fittings, and PRMS.
Na kwavile hiyo inaangukia kwenye Local Content, hiyo kazi inatakiwa kufanywa na Watanzania as per Sheria ya Mafuta na Gesi ya 2015!
Now tujiulize!!
Kama tunaamua gas infrastructure zifike hadi wilayani, hapo atakayepata tenda atalazimika kuzalisha hivyo vifaa kwa wingi gani, na angetoa ajira za moja kwa moja ngapi, indirect employment ngapi, na Wauza Mama Lishe wangeuza sahani ngapi za ubwabwa, ugali, chapati and everything else?
That's what we call: ECONOMIC MULTPLIER EFFECT! Gesi ipo LIndi na Mtwara lakini effect yake inasababisha kujengwa kwa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kujengea miundo mbinu ya usambazaji gesi! Hapo zitazalishwa aina ya ajira kama nilivyotaja hapo juu!
LNG Project inayopelekea kujengwa kiwanda tajwa hapo juu, effect yake itamkuta hadi muuza Mama Lishe, Muuza Genge, Mangi na Mpemba na maharage unga na mchele wao dukani, mkulima aliyezalisha hizo bidhaa, n.k kwa sababu pesa itakayotokana na hizo shughuli itakuwa inaenda moja kwa moja kwa wananchi na pesa hizo kuambukiza sekta zingine za kiuchumi na kijamii!
Hapo umeshazalisha tu vifaa tajwa... what next?
Hivyo vifaa vikishazalishwa ina maana itabidi iwepo kampuni nyingine/zingine za kutandaza hizo infrastructure Tanzania mzima! Kampuni hiyo nayo itatoa ajira za moja kwa moja, kwa vibarua na wauza Mama Lishe ambao pia wataambukiza sekta zingine kama nilivyotaja hapo juu!
Aidha, projects zote mbili... za kuzalisha vifaa na kusambaza miundombinu pia zitazalisha PAYE na Kodi zingine kwenda serikalini, na hatimae kuleta direct effect kwenye public services zitolewazo na serikali!
THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT in the national economy ambayo inapatikana hata kabla gesi yenyewe HUJAIGUSA!
Gesi imeshazalishwa, and ready for different uses! Je, miundo mbinu itaweza kufika kila mahali? HELL NO! This HELL NO is another business opportunity kwa sababu hatimae kutakuwa na new opportunity to Gas Vendors! Wenye uwezo watajenga Gas Fuelling Stations!
That's what we call Multiplier Effect!!
3.
Gas By-Products:-
Nimeshajaza server tayari kwahiyo hapa niongee kidogo tu ingawaje kuna mengi zaidi ya kuongea!
Mali Ghafi zinazotokana na uchakataji wa gesi zinaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali! Hapa tusiende mbali! Tayari kuna project ya USD 1.9 Billion kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea ambacho kinatarajia kutumia Gas By-Products!
Tanzania hii HAKUNA Kiwanda chenye thamani hata nusu ya hicho kiwanda!! Now tujuulize: Kiwanda kama hicho kinaweza kuzalisha direct and indirect employment to the company ngapi, Mama Lishe wangeuza kiasi gani kwa vibarua na wafanyakazi, PAYE and other taxes zingelipwa kiasi gani...
THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT!
Sio viwanda vya mbolea peke yake vinavyoweza kutumia Gas By-Products! Kuna at least 4 MORE products, including Plastic Products zinazoweza kuzalishwa kupitia Natural Gas By-Products!!!
FAIDA zote hizo nilizotaja hapo juu, HUWEZI KUZIPATA kupitia JNHPP!!
Sasa akina sisi tulikuwa tunapinga JNHPP kwa sababu tunaamini LNG Project inaweza ku-offer almost everything that can be offered by JNHPP but MANY MORE at much HIGHER VALUE than what JNHPP can offer!!!
Kwenye uchumi tunazungumzia dhana ya optimal allocation of resources!! Tunaambiwa resources, kwa muktadha huu pesa, ni SCARCE! Hivyo basi, kidogo utakachopata unatakiwa ku-allocate kule utakopata MAXIMUM RETURNS, and not just RETURNS!
LNG Project inaweza Kujenga JNHPP with our own money in less than 5 years lakini JNHPP KAMWE haiwezi kuwa na uwezo wa ku-fully finance LNG Project!! Kumbe basi, kama tunaamini Hydropower ni CHEAP source of electricity, bado tungeweza kujenga mradi huo kwa pesa zetu sisi wenyewe miaka michache tu baada ya kuanza kuzalisha gesi!
ALL IN ALL, should we expect CHEAP ELECTRICITY from JNHPP?!
Kwa maoni yangu, sioni hiyo cheap electricity inapatikana patikana vipi!!
Kwahiyo ndugu yangu Malcom, ule mpango wako wa kusambaza mashine za kusaga Tanzania mzima kwa sababu kuna umeme wa bei rahisi unakuja, man, ningekushauri pitia vizuri plans zako kwa sababu I strongly believe umeme wa bei rahisi HAUTAKUWEPO!!
WHY?
1. Mradi utatumia takribabi Sh 7 TRILLION. Hapo zijaweka riba za mabenki kwa sababu funding sources zingine zinatoka kwenye private banks!
Sasa kama tunadhani umeme utakuwa wa bei rahisi, who will pay hizo TZS 7 Trillions + Interests?! LAZIMA Watumiaji tulipe hizo gharama!!!
2. Watanzania tunadhani umeme utakaozalishwa pale ni MWINGI kweli kweli!!
Guys, kinachozalishwa pale sio kwamba Umeme Mwingi bali Umeme unazalishwa kwa ajili ya jamiii yenye Umaskini Mwingi!!
Kama nilivyosema hapo awali, Kenya ni nchi maskini tu! Lakini leo tuseme Kenya iachane na vyanzo vyote vya umeme inavyotumia hivi sasa na badala yake waanze kutumia umeme MWINGI utakazozalishwa pale JNHPP, katu Umeme huo HAUTAWATOSHA!!
Hata Tanzania kwenyewe, na umaskini wetu huu halafu tuseme tufunge vyanzo vyote vya umeme tulionao na tuanze kutumia tu Umeme MWINGI kutoka JNHPP... it'll take us less than 5 years kabla hatujaanza kuwa na uhaba wa kutisha wa umeme kwa sababu pale hakuna umeme mwingi bali tuna umaskini mwingi unaofanya less than 3000MW zionekane ni umeme mwingi!
Ninachojaribu kusema ni nini: Endapo uchumi wetu unaongeza kwa angalau 10% TU, umeme kutoka JNHPP + Available Sources HAUTAWEZA kuhimili uchumi huo ambao kimsingi na wenyewe utakuwa ni uchumi wa kimaskini tu!!!
Kwa maana nyingine, hata kabla hatujamaliza deni la TZS 7 Trillion za JNHPP basi kuna uwezekano mkubwa sana demand ya umeme nchini inaweza kuongezeka hapo mbeleni na kumeza umeme wote tulionao hivi sasa + Umeme wa JNHPP!
Demand ikiwa kubwa, watakachofanya TANESCO ni ku-DISCOURAGE Matumizi Makubwa ya Umeme! Una-discourage Matumizi Makubwa ya Umeme sio kwa kutoa elimu bubu watoazo kwenye ma-tv bali watafanya hivyo kwa kupandisha bei ya umeme ili hatimae muache matumizi holela ya umeme, kama mlivyoacha kutumia majiko ya umeme bila hata kutandikwa bakora!!
Na hapa tukumbushane kwamba, kama kweli tunaamini bei itakuwa ndogo basi ni hiyo bei ndogo ndiyo itakuwa chanzo cha kukaribisha bei kubwa! Umeme ukiwa nafuu, matumizi ya umeme yataongezeka! Watu watatupa majiko yao na pasi zao za mkaa kwa sababu umeme ni cheap!
Wafanyabiashara wataachana na mashine za kusaga zinazotumia mafuta na kuhamia mashine zinazotumia umeme kwa sababu umeme ni cheap!
Matumizi ya vifaa vya umeme yataongezeka kwa sababu umeme ni cheap!!! Huku Uswahilini ule ugomvi wa wapangaji kwamba tuwe tunazima mafriji na mafriza yetu, ugomvi huo utapungua kama sio kwisha kabisa kwa sababu umeme ni cheap, na watu watakuwa wanajiachia!!
OUTCOME?
Increased power consumption!! Njia ya kupambana na hilo? Nishasema hapo juu: discourage power consumption by increasing the price!!
IT'S SIMLE ECONOMY!
Is JNHPP White Elephant Project?
Yakitokea niliyosema hapo juu, HAIWEZI KUWA White Elephant Project lakini yasipotokea inaweza isiwe White Elephant Project lakini inaweza kuwa a STRUGGLING PROJECT!!
Tunahitaji uchumi mkubwa zaidi ili tuweze ku-consume hizo additional MW zitakazozalishwa! But don't forget, huo uchumi ukitokea itamaanisha NO MORE CHEAP ELECTRICITY kwa sababu power consumption itakuwa kubwa!!
Na isipotokea, ina maana Project Haitaweza kuzalisha pesa ya kutosha kulioa madeni yake, and hence becoming a STRUGGLING PROJECT!!
Yaani ndo ile inaitwa
Ukichimama Nchale, Ukikimbia Nchale!! Sasa chagua mwenyee udungwe nchale wakati umesima au wakati unakimbia... MAUMIVU YAPO PALE PALE!!
Ndo vile tu umeme utaingizwa Grid ya Taifa lakini kama ingekuwa unakuwa distributed kipeke yake peke yake, watu wangeukimbia huo kama wanavyolikimbia Daraja la Kigamboni!!