Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
View attachment 2128208
Game of Chance.

Safi sana.

Hii ni straight forward cash.

Negotiations skills ni muhali lakini hapo hapo ndo exit ilipo!

Hongera sana MH Rais.
 
Duniani anayetumia nafasi anayopata vizuri ndo anaye survive. Amri kuu ni survival for the fittest
 
Akili ya mtu na fikra potofu ni ku-attack personality na sio hoja; Mimi nimekwambia hayo mawazo ni potofu kuliko..., hao stakeholders sita walioingia mkataba leo ndio walifanya research, na hizo research walifanya kwa hisani? Gas huko iligunduliwa lini na nani na wanaosign mkataba leo ni kina nani ?

Again rudia nilichoandika ni lazima natural resources zote zimalizwe katika kizazi chetu ?, Kwa matumizi mazuri tungeweza kuchimba baadhi na kutumia hio faida kuwekeza kwenye migodi mingine kwa stake nzuri zaidi.., Mfano Mkataba wa Diamond Botswana ni sawa na wa kwetu ? Je Dunia pia itapiga marufuku matumizi ya Diamond na Gold ?

Unajua maana ya faida ? Tunapata percent ngapi kwa huo uwekezaji ? Alafu usiamishe mjadala hapa umeongelea kwamba wacha tupate stake kidogo sababu hatukufanya research na hatuna uwezo ili tupate faida ya ajira na Kodi....

Kweli Akili ni Nywele....
Rubbish 🚮🚮

Screenshot_20220222-100231.jpg
 
Indeed I might be a fool..., but am wise enough to know that I know Nothing, which gives me opportunity to learn and understand..., unlike if I was a Much-Know Person, I might have known less than what I know Now....

And I always talk and discuss issues at hand..., not personalities and who has said what.... (even a fool might have a point sometimes and vice versa)
 
Wapo wengi ila huwezi mlinganisha Muhongo na Kalemani au Makamba...hata ukiwachanganya pamojahawafiki hata heluthi ya uelewa wa Muhongo kwenye ishu za madini na nishati mkuu...Muhongo ni level nyingine boss.
Ni sawa na kumlinganisha Danieli Chongolo na Pius Msekwa/Rashid Kawawa/Horace Kolimba/L.M. Gama/P.J. Mangula/W. Mkama/A. Kinana. Ni mbingu na ardhi.
 
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
View attachment 2128208

Tanzania hatuna gesi! Gesi yetu tulishaiuza! Hata wakija kuchimba hiyo gesi sisi tutaambulia labda Kodi! Lakini gesi Kama gesi tulishaiuza kitambo! Iliamdaliwa sheria ya gesi kwa hati ya dharula muda mfupi kabla ya kumalixika kwa Serikali ya awamu ya nne!! Kwa sheria hiyo tuliuza gesi yetu!! Na sisi ni wadowezi tu wa gesi hii inagopatikana Nchi. Ni bahati mbaya Sana!
 
Hizi ni propaganda za watu wa ulaya.
Mh. Samia sio limbukeni hivyo, wa kukubali kuyumbishwa na matakwa ya kibepari.

Propaganda za watu wa ulaya na baadhi ya mabepari wanaoizunguka CCM .

Akijichanganya, ndie atakuwa Raisi aliyopotoshika na kuyumbishwa na mabepari kuliko maraisi wengine wengi Barani Afrika.
Hizi ni jitihada hasi kwa Rasilimali za Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
Ee muumba, tupatie nguvu za kuwajua wasiotutakia mema mbeleni.
 
Back
Top Bottom