Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
 
Nimekusoma ulichoandika mpaka pale uliposema nchi yetu ina siasa nzuri, huu upofu wa makusudi unaojitia unajidanganya mwenyewe, ni kama unajitekenya na kucheka peke yako.

Kuhusu hiyo LNG mtazipata wapi $30mil zinazohitajika kwenye huo mradi?

Kwa utoto ulioandika hapa, vipi kuhusu Nyerere Dam ndio pesa imeshachezewa pale kwa hiyo iachwe ipotee?

Kama hiyo ndio akili yenu, kwanini nisiamini mnataka kuanzisha mradi mpya wa LNG ili nanyi mpate nafasi ya upigaji ili kama ikitokea msipoukamilisha kama wa Nyerere Dam muwe mmeshaiba mnachotaka?

Naona umejaza uzi wako na yanayotokea ulaya kama vile hao wazungu wanatupenda sana sisi, unajidanganya tu, kwenye maslahi hakuna taifa litakalokubali kuwa nyuma ya lingine hata kama kila siku mtaenda kwao miaka kumi mfululizo.

Tusidanganyane, sharti mradi wa Nyerere Dam ukamilike kwanza kama kweli mnataka kuokoa pesa za walipakodi masikini wa Tanzania, badala ya kujitutumua na miradi mipya ya bei ghali ambayo hamuwezi kuikamilisha wenyewe, huu ujinga wa kujiona wajanja kwasababu mnakopesheka utaangamiza vizazi vya hili taifa.
 
Hata wa gesi enzi za Kikwete walisema ukianza uzalishaji hakutakua na tatizo la umeme na nchi itapata faida za madola mengi mpaka waitu tukawa na matuamaini ya maisha mazuri.

Lakini mpaka sasa tunaugulia maumivu ya maisha magumu.

Hii ndo Tanzania ndugu.
 
Aisee kama ukisikia kukosa Busara na kutokufikiria mbali ndipo huku.

Kama kweli kilichoandikwa hapo kwamba anafikiri mgogoro wa Russia na Ukraine utamnufaisha kuuza gas (kufikiri sio kosa ila watu kujua fikra zako, hususan hizo fikra kama hazina ubinadamu basi ni kosa kubwa), Hujui kesho itakuwaje na nani..., atakuwa nani.... Alafu anajimarket kama mtaka Amani Duniani..., wakati matendo yanaonyesha ni mtafuta Fursa

Lesson from the Godfather; Never let anyone know what your are thinking
 
Kaka hakuna siri duniani
 
Huo mradi si mwendazake aliusimamisha
 
Wakati wa Kikwete hatukufikia hatua ya uzalishaji wa LNG
 
Upo sahihi kabisa...

Mwaka 2018 niliwahi kuandika haya...


mkuuwakaya,

Nitajitahidi kueleza kwa uchache sana manake kwenye issue ya gas kuna mengi sana ya kueleza!!

Mosi; FAILURE kubwa ya JPM katika issue ya kutozingaatia vipaumbele basi ni suala la gas!

Kama kweli JPM ana lengo la kuwaondolea Watanzania umaskini basi TOP PRIORITY yake ingekuwa kwenye gas na wala sio ndege na wala sio viwanda!

Angeweka priority kwenye gas... akazuia ufisadi kwenye gas; na akajenga uchumi mzuri wa gas; hayo ya ndege na viwanda yangekuja automatically tena at advanced level!

Wakati tunaenda mwaka wa 3 sasa na bado ndo kwanza kafanikiwa kupata vindege 3 kiasi cha kutokuwa threat hata kwa FastJet; endapo angejenga na uchumi wa gas angeweza kununua hata Airbus 100 kwa mpigo na kuyatisha hata mashirika makubwa kama Ethiopia Airline!

Gas ni uchumi

Gas ni viwanda

Gas ni fimbo ya diplomasia

Gas ni fimbo ya siasa za kimataifa

Kufafanunua yote hayo kunahitaji muda!

Lakini kwa ufupi tu ni kwamba; leo ukizalisha gas na kusambaza throughout East Africa... hizo nchi zote zitakuheshimu!

Zitakuheshimu kwa sababu zitafahamu uchumi wao unategemea gas ya Tanzania!!

Yule Kagame aliyekuwa anamkejeli JK ingekuwa ukimpigia kufuli koki inayopeleka gas Rwanda; siku ya pili angepanda ndege kuja Dar kusawazisha hali!

Hiyo ndiyo gas!

Hata byproducts zinazotokana na natural gas processing ni malighafi tosha ya viwanda!

I hate to say this but to be honest hata kwenye madini alikowekeza nguvu nako ni wastage of time!

Sisemi apuuze kwenye madini bali ile nguvu aliyowekeza kwenye madini ndo angewekeza kwenye gas basi impact yake ingekuwa kubwa zaidi ya mara 10!

Ngoja nikuulize swali moja:

Hivi wazungu wakigoma kununua ile Tanzanite na Gold; alternatively tutaifanyia nini?!

Swali lingine dogo: Unaweza kunitajia nchi 3 tu duniani zinazokula bata kwa kutegemea uchumi wa madini?!

Jiulize maswali sawa na hayo upande wa gas!

Panapo majaliwa; ningependa tujadili kwa mapana na marefu; with statistics and figures na subject iwe: "A Comparative Analysis of the Gas and Mining Economy"

To sum up... JPM bado hajaiangalia gas kwa jicho pana kiasi hicho! Pamoja na madhaifu yote ya JK lakini inaelekea yeye aliiangalia gas kwa jicho pana na ndio maana ilikuwa ndiyo priority yake!

Na ngoja nikutoe shaka!

Gas tunayoizungumza hapa na aliyokuwa anaisema JK na Muhongo wake sio hii iliyoanza kupita kwenye Bomba la Gas la Mtwara!

Gas yenyewe haijachimbwa bado! Ile ya kwenye bomba is just a fraction of 57 trillion cubic feet of discovered gas reserve!!

Gas yenyewe ni ile ambayo kiwanda cha kuichakata ndo kile kilitarajiwa kujengwa pale Lindi!

Mradi wa kile kiwanda peke yake ni zaidi ya Shilling Trilioni 65... narudia; sio Bilioni 65 bali TRILIONI 65... Bajeti yetu miaka 2 na chenji inabaki!

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kiwango hicho ni takribani mara 2 ya Market Cap ya Barrick Gold!

Barrick Gold ndio kampuni kubwa kuliko zote za uchimbaji dhahabu duniani!

Cortez na Goldstrikes ni among top 10 mines duniani na yote hiyo ipo USA na inamilikiwa na Barrick Gold Mines!

Chukua mapato yote (not faida) ya mgodi wa Cortez na Goldstrikes kwa miaka 10 ndipo labda unaweza kufikia hiyo Trilioni 65.

Hiyo ndiyo gas tunayoisema! Investment ya kiwanda cha kuichakata tu ni Bajeti yetu ya miaka 2!!

JPM bado hajaona ikiwa mradi kama huo unahitaji priority!

Aidha nikujuze lingine! Achana na simulizi za kwamba gas yote imechukuliwa na Wachina!

Makampuni yaliyofanya exploration ni ya Ulaya na America! They invested billions of T Shilling kufanya exploration! Aidha zote hizo ni gas and oil companies!

That said; there's no way pamoja na energy yote waliyotumia halafu gas yote wamwachie Mchina wakati wao hiyo ndiyo biashara yao ambayo wapo tayari hata ku-initiate War for the sake of their business... gas and oil business!!

Gas and oil business iliyozalisha:
Etihad Airways
Emirates
Qatar Airways

Hivi umeshawahi fika Qatar ukaona wa-Qatar wanavyoishi kama Wafalme?!

Ni nchi pekee duniani ambayo zaidi ya 80% ya population yake ni wageni! Ni wageni walioenda kutafuta na kufanya kazi huku wenyewe wakifanya kazi kifalme! All that is because of the fvcking gas and oil business ambayo JPM ni kama bado sio priority kwake!

Tungechimba ile gas wala tusingehitaji tena Stigler's Gorge!

Stigler's tungeiacha iendelee kuhifadhi uoto wetu!!

What about Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015 pamoja na ile ya Sheria ya Matumizi ya Mapato ya Mafuta na Gesi?!


Na kuna siku niliwahi kusema hapa kwamba, position ya Tanzania relative to Europe ni fursa kubwa sana kwa sababu Putin amekuwa akitumia sana fimbo ya gesi, na kwahiyo lau kama tungekuwa tumechangamka, basi ukanda huu wa Africa... yaani Tanzania and Mozambique ingekuwa ndo kimbilio la Europe ukiacha Middle East.
 
Kwa iyo unapingana na wachambuzi mahiri The African Report?

Unaonekana hata Elimu yako ni mashaka, kuna uhusiano gani kati ya LNG na Umeme au Bwawa la Nyerere?

Nani kakwambia LNG inatumia pesa za serikali?
 
Kaka hakuna siri duniani
Nani kasema ni Siri...., Kuna Tofauti kubwa kuwaza kwamba rafiki yako amefariki huenda yule kimada wake atakuwa wako...., Na kusema hadharani kwamba sasa rafiki amefariki kuna uwezekano kimada atakuwa wangu...., unaweza kumkosa hata huyo Kimada kwa kuonekana una roho ya ajabu....
 
Hivi ww upo Tanzania au nje ya Tanzania, unaambiwa hii gesi inayochibwa tanzania sio ya tanzania ni ya viongozi wachache na wawekezaji.

Taifa halina chake hapo umasikini ni wetu milele
 
Nchi hii bado ina vijana wa ovyo wengi. Naona mnaanza kujitengenezea mwanya wa kula national cake ili hali raia wanalia kwa maisha magumu. Mnataka mrudishe siasa za gas ya Mtwara zilizoacha watu wakiwa vilema na wengine kulazimika kuzikimbia familia zao.
 
Tanzania ni mbali sana kusafirisha Gesi mpaka Ulaya, Ulaya target yao ni Ukraine ambapo ni karibu gharama itakua ndogo ya usafirishaji
 
Acha kuongea nadharia, Samia alikuwa Ulaya wiki hii iliyopita, Mkuu wa Kampuni ya Shell kaongea na shirika kubwa la habari la Ulaya Reutres juzi na kasema juu ya maendeleo ya mazungumzo na serikali ya Tanzania

Wachambuzi wa nje wameona hilo na wanaliongelea wewe endelea tu kudhani ni siri
 
Na juzi juzi tu hapa nilimwambia ndugu yangu MALCOM LUMUMBA maneno haya:-

Kwahiyo nakubaliana na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…