Mradi wa maji wa Sh585 milioni wazinduliwa na mwenge wa uhuru
MWENGE wa Uhuru umezindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Mtambo wa Kuchuja Maji Igombe–Kabangaja, jijini Mwanza, uliyojengwa kwa gharama ya Sh585 milioni, unaolenga kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo hayo.
Mradi huo umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) kwa kushirikiana na Shirika la Maji la Uholanzi Vitens Evides International (VEI) na umekamilika kwa asilimia 100.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo, Agosti 11, 2026, wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwango’nda, alieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali na wadau kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.
Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wananchi wa Kata za Bugogwa, Sangabuye, Kahama na Shibula, kwa kuwaongeza upatikanaji wa maji safi na salama, jambo litakalosaidia kuboresha afya, usafi na ustawi wa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwango’nda alisema maji ni miongoni mwa huduma muhimu zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja na kwamba uwekezaji katika miundombinu yake ni sehemu ya kuboresha mazingira ya maisha.
“Mradi huu ni mradi muhimu unaogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, kwa kuwa utaongeza upatikanaji wa majisafi na salama na hivyo kuchangia kuboresha afya na ustawi wa jamii,” alisema.
Mradi umejengwa kwa Sh585 milioni
Kwa mujibu wa taarifa ya MWAUWASA, mradi huo ulianza kutekelezwa Oktoba 1, 2024 na ulikamilika Juni 30, 2026.
Fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kuchuja maji, ununuzi na usimikaji wa tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 100,000, pamoja na pampu mbili zenye uwezo wa kusukuma maji lita 50 kwa saa.
Kazi nyingine zilizotekelezwa ni ulazaji wa bomba la milimita 200 lenye urefu wa mita 12, bomba la milimita 100 kwa ajili ya kupeleka maji kwenye tenki, pamoja na ujenzi wa choo na uzio wa eneo la mradi.
Vijana 25 wapata ajira
Mbali na kuongeza upatikanaji wa maji, mradi huo umechangia pia shughuli za kiuchumi katika eneo hilo kwa kutoa ajira za muda kwa vijana 25 wakati wa utekelezaji wake.
Msimamizi wa Miradi wa MWAUWASA, Mhandisi Nuhu Said, alisema kukamilika kwa mradi huo kumeongeza miundombinu ya maji na kutoa fursa ya wananchi kupata huduma bora zaidi.
"Alisema mradi huo pia umeweka mazingira mazuri ya kuandaa na kutekeleza miradi mingine ya kupanuwa mitandao ya maji na kuongeza maunganisho kwa wananchi". Ameeleza Mhandisi Rukia Yunge Mratibu wa mradi kutoka - VEI
MWAUWASA: Tutashirikiana na wadau
Akizungumza jijini mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA mhandisi Mashaka Sitta imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuimarisha uwekezaji kwenye miundombinu ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu.
Katika hafla hiyo, Baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa mradi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
Aidha, aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo na kuitumia kwa uangalifu ili iweze kudumu na kuendelea kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.