Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Tutenganishe kwanza biashara na siasa. Tatizo ni kwamba hata watendaji wakuu wa miradi kama hiyo wanateuliwa. Kibaya zaidi wanateuliwa kisiasa, ni makada ambao unakuta mara nyingi hawana sifa, wao wakishaingia maofisini ndo kuidhinisha pesa za kampeni za chama, wanajijenga wao kuja kugombea baadae badala ya kusimamia maendeleo.

Hatuwezi kwenda huku tunajiibia wenyewe, lazima tuonekane matahira tu.
 
Wakati serikali inaamua kusimamia baadhi ya bishara,kuna watu walipiga kelele mno kwamba hakuna serikali inafanya biashara duniani.

Wacha niwakumbushe,serikali haifanyi biashara ya aina yeyote bali inajenga miundombinu na kuisimamia itoe huduma na kuongeza speed ya utafutaji kukuza uchumi.

Umetoa mfano wa mwendokasi,na hasara zake,ila sijui kama unajua bado ujenzi unaendelea!!unadhani ni bahati mbaya??lengo ni huduma sio biashara.

Kesho reli ikikamilika,ni wewe utaamua ukasafirishe mitumba yako ktk train kwa masaa manne ulipe laki tano,au kwa roli masaa 12 ulipe laki 8?

Reli ya kati imetoa huduma muda mrefu sana, mpaka ilipokuja kuachwa na mabadiliko ya tech na huduma kwa ujumla,train unalipa elfu 8 unasafiri siki 2,basi unalipa elfu 24 unafasiri masaa 12.hapa uchumi wa mtanzania mwenyewe utaamua train iendelee kuishi au ife jumla.

Kuliko kuwa watu wa kulalamika kila siku kama chadema,ni heri tukawa washauri na watu wa kupiga kelee tunapohisi kuna uzembe na hujuma ktk mali za uma.
 
Tatizo aliloezea kwa mafumboni conflict of interest. Hii ndiyo inaua sekta nyingi za umma. Mkurugenzi mtendaji Sema wa tazara, Ana malori - 100 (mfano tu huo) amepata mzigo kwenda Zambia, je ataupeleka kwa malori au kwa reli? Mwingine Ana daladala 50 kila route, haya ya mwendokasi atayapa muda mwingi WA kuyashughulikia? Mwanzoniwamiaka Ile, viongozi WA umma hawakuwa na ruksa ya kushughulika na kitu nje ya kazi Ile aliyopewa. Mageuzi yaliyofanywa pale Mbeya yalileta haya tunayolalamikia Leo. HATA BABA WA TAIFA ALILISEMA NA KUOMBA AONYESHWE UBAYA WA YALE WIYOKUBALIANA KABLA YA MBEYA CONFERENCE.
 
Kwa hiyo mwendo kasi ni huduma au biashara? Ukiniambia shule za msingi ni huduma nitakuelewa, sio hayo mabasi yanayojaza abiria wanaolipa nauli mpaka mlango inakuwa shida kuufunga.
Yaani mpaka iwe bure kabisa ndo ujue ni huduma kwa jamii?
 

Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kuendesha mradi wowote kwa faida.

Siyo kweli kuwa eti sekta binafsi ndiyo inayosababisha serikali ishindwe kuendesha miradi ya biashara kwa faida. Kusema kwamba sekta binafsi inaihujumu miradi ya serikali ili sekta binafsi ipate biashara ni uwongo mkubwa:

1) TANESCO haijawahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja, inashindana na nani?

2) ATCL haijawahi kupata faida hata mwaka mmoja. Waliiondoa Fastjet kwa mizengwe. Je, sasa wanapata faida?

3) Serikali ilikiwa inamiliki viwanda vya bia kabla ya kubinafsishwa, haikuwahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja. Ilikuwa inashindana na nani wakati huo?

4) Serikali ilikuwa inamiliki kiwanda cha sigara, haikuwahi kutengeneza faida, ilikuwa inashindana na nani?

5) Serikali ilikuwa inamiliki viwanda vya zana za kilimo, kampuni ya simu na posta, na mengine mengi, lakini ilishindwa.

Serikali, kama ilivyo kwenye taasisi nyingine, imejaza watu wa ajabu, watu wenye uwezo mdogo, wanaoteuliwa kuendesha miradi hiyo wanateuliwa kwa mtazamo wa kisiasa, watu ambao uwezo na maarifa yao ni duni sana. Watu kama Sabaya, Mwigulu, Kalemani, Biteko, unategemea wanaweza kuendesha mradi wowote ukapata faida? Watu wa namna hiyo, ndiyo wamejaa kwenye taasisi za Serikali ambazo zilistahili kuongozwa na watu kwa kuangalia weledi na siyo siasa za ulimbukeni.

Nani atumie usafiri wa TAZARA, wakati ukitaka kusafirisha mizigo yako, mlolongo wa kupitia ni kama umeenda kuomba msaada. Watendaji wengi wa sekta ya umma wanachojua ni kuabudiwa, siyo time sensitive. Vivyo hivyo itakuwa kwa SGR.
 
Kuna Watu wa janja Watanzania wana hujumu hizi reli ndo maana hazifanikiwa.

Mtu ananunua magari 100, 200 ya mizigo au Abiria ni watu wenye fedha na majina makubwa wakati Mwingine wanashirikiana na watu wa Serikali anategemea kutumia barabara ya Lami hauwezi kuunga mkono reli.

Reli ikifika itaharibu biashara yake
 
Duniani kote ni nadra sana kupata serikali inayoweza kufanya biashara yoyote kwa faida. Biashara ni uwanja wa sekta binafsi, serikali iache kufanya biashara badala yake itengeneze mazingira mazuri ya biashara kufanyika na yenyewe ikusanye kodi.

Serikali ya Marekani hadi sekta nyeti kama ya Ulinzi imetoa fursa kubwa ya sekta binafsi kufanya kazi. Sekta binafsi inatengeneza silaha zote zinazotumika na jeshi la Marekani, zinazouzwa na kutolewa misaada nje ya nchi. Karibia vinu vyote vya nyuklia Marekani vinamilikiwa na makampuni binafsi, sisi bado tumebaki na mawazo ya kijima ya karne za giza ya serikali kumilik hadi ng'ombe kwenye ranchi!
 
Hata kusipokuwepo na conflict of Interest, watu walioajiriwa serikalini sio rahisi kufanya biashara kwa ufanisi kwa sababu nyingi sana.
Meneja wa masoko wa TAZARA, Meli za Serikali au ATCL watalipwa mishahara yao tu pasipo kujali kuna faida au hasara ya miaka 10 katika shirika, hali ikizidi kuwa mbaya watahamishiwa sehemu nyingine na wataendelea kulipwa kama kawaida huku mshahara wao ukipanda kila mwaka.

Meneja masoko wa Precision Air, Azam Marine au Basi la Saul utakuwa na bahati sana kama kampuni itapata hasara kwa miezi 6 mfululizo na ukaendelea "kusavaivu" ofisini.
 
Reli muhimu kuliko zote nchi hii ni reli ya TAZARA na hiyo ndiyo serikali ilapaswa ifufue miondombinu yake iwe ya kisasa na sekta binafsi ipewe fursa ya kufanya bishara ya usafiri huko.
 
Reli ya Tazara ilipingwa vikali na WB/IMF kwa sababu za nguvu kwamba was not economically viable na mbaya zaidi feasibility study haikufangika hivyo wakakataa kutoa mkopo kwa Nyerere.

Hapo sasa ikabidi mwalimu akajisalikishe kwa beberu mpya China matokeo yake reli ikajengwa ndio hadi leo hii ni hasara kwa kwenda mbele.

Jiulize kama Tazara inakula hasara na 70% za mzigo wa bandara ya Dar unakwenda Sadc region unadhani hiyo sgr ya TRC itakuaje?

Kwa miaka yote TRc inakula hasara mara wafanye wao mara walete wawekezaji lakini ni loss loss loss na zero kila wakati.Sasa subiria sgr ikamilike loss yake Atcl na Tanesco watasoma.

Hii nchi tutaendelea kula hasara na maisha magumu kwa mda wote kutokana na maamuzi yasiyo na tija hayakuzingatia weledi bali hisia za kikanda na kisiasa.

As for me muda wa kujenga sgr ulikuwa bado Sana ilitakiwa tuimarishe barabara na tusubirie Congo drc iwe na stability huku mashariki kwake na biashara yake iwe vizuri ndio Tujenge hiyo sgr .

Hakuna shirika la serikali linapata faida halipo labda mabenki ambako ina hisa,hata huo mwendokasi ni bora wafanye private sector au njia hizo ziwe za daladala tuu.Kila siku nawaambia mtu wa serikali anaepokea salary hawezi leta tija Serikalini hata siku moja,kinachofanyika private sector Ili mambo yaende ukileta Serikalini watu wataacha Kazi na wengi watafukuzwa.
 
Pamoja na hilo lakini kubwa kabisa ni kuruhusiwa viongozi Tena kule juu kabisa kujiingiza kwenye biashara, wakati huo huo TAIFA halikuwa na mwongozo wa kushughulika mambo kama haya yakitokea. Kungekuwa na sheria kuwa kama ni biashara basi a ha u director General wa TPA au TRC, fanya biashara yako.

TAIFA lilikuwa bado changa wakati huo na wakaruhusu viongozi kuwa ndumila kuwili. Je inategemewa nini. Makampuni ya biashara makubwa yalifukuzwa, elimu ya biashara ndiyo kwanza inaanza, kesho mtu Ana cheti toka cbe wakati huo au chuo cha ushirika moshi anakabidhiwa rtc mkoa au kampuni ya usafirishaji mkoa, unategemea nini.
 
Miradi ni ya mhimu ,tatizo lipo kwenye usimamizi this why miradi inaonekana ni ya hovyo
Usimamizi umefanyaje? Utasimamia nini ikiwa sgr unajenga sehemu isiyokuwa na mzigo kama njia ya Mwanza au central corridor nzima?

Tazara,mwendokasi na masoko yamewashinda ndio huko wataweza?
 
Kumbuka viongozi wote waliotembelea bwawa la Nyerere pamoja na waandishi wa habari waliwasifu wajenzi! Sasa kauli ya makamu wa Rais aliyoitoa juzi kuhusu ujenzi tuisemeje!
 

chadema ni chama kimejaa watu wa ajabu wasioitakia nchi hii jema la aina yoyote,sababu tu wamekosa nafasi ya uongozi.

bisha nikuonyeshe ni kwa namna gani watu hawa hawaitakii nchi hii aina yoyote jema.
 

kwan mwendokasi umeharibu biashara ya daladala?
 

unajua kama hujawahi fanya biashara ni rahisi sana kutoa ushauri kwa anaefanya biashara! nchi nyingi sana znategemea reli kama njia ya usafiri ila malori yapo kama kawa, hata hapa daladala zililalamika sana mwendokasi ulivokuja, hizo daladala zmekufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…