sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,632
- 4,737
Mkuu hatujui kama tuhuma hizo ni za kweli au hapana.kwa unafki grade one kama huu kuna kaukweli flani unakaongea na huyo mkandarazi kweli ni feki kwa ushahidi wa kumpa kazi Mchina nae kutupiga percent ya malipo bila jasho na pia yaonesha mwangalizi mkuu wa hapo yaani Waziri wa Nishati ni feki kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu alihangaika mpaka akakonda kila mradi kama hakuna upigani basi hakuna usimamizi!!Nyerere alitamani kuwa waziri wa kila kitu alipoona kachoka akamtupia kijiti Mzee Ruksa na kukimbilia Butiama kutuliza kichwa chake!!
Mradi huu ni mkubwa wenye maslahi makubwa kwa raia wote yafaa kuvunja mkataba na Watu wa Egypt na kuwapa mkataba hao wachina wanaojenga ili tupunguze costs na bureaucracy na kumuondoa mtu wa kati ili mradi uishe kwa wakati, yafaa Mkulu apewe activity plan yote ikiwa na dates za kila stage of implementation na awe kila three months anaenda mwenyewe kukagua kama reality ina reflect what is on the paper!! akikuta karatasi na reality ni tofauti hiyo ni kigezo cha kuvunja mkataba, heri nusu shari kuliko shari kamili!! huu ni mradi mkubwa wa kimkakati uliomshinda Nyerere na wengine waliomfuatia , ni mradi utakaoacha alama ya Mkulu na Chato kwa karne nyingi! Mkulu asione aibu kuwaita mawaziri na kuwakaripia na kubadilisha wasimamizi wa mradi , Nyerere aliwachekea kina Kambona akavuna mabua!!
Ila kama mchina ndio fundi mkuu wa kila kitu kwanini hakuitwa China kuwa main contractor?
Yetu macho.