Mradi wa Stieglers: Mwarabu anaharibu mradi hana utaalam wala ujuzi wa kujenga bwawa, italeta hasara kubwa kwa taifa na ubora hafifu


[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tanzania ndo nchii pekee kila mtu mjuaji na ana ujuzi wa kila kitu, mradi hata hujakamilika tayari tuhuma! upinzani kazi kwel kwel
 
Mimi sioni tatizo,sio lazima mkurugenzi wa hiyo kampuni ajue kutumia sululu katika kuchimba hilo bwawa,,atatumia subcontractor
 
Tanzania ndo nchii pekee kila mtu mjuaji na ana ujuzi wa kila kitu, mradi hata hujakamilika tayari tuhuma! upinzani kazi kwel kwel
hahaha. mkuu umenikumbusha mbali, wakati daraja la kigamboni lizinduliwa kuna watu humu walisema halina viwango na litavunjika mda wowote
 
Hiyo kampuni mbona nilisikia huko kwao ilikuwa ni kitengeneza chemba za choo na nyingine inashughulika na stetionary
 
Yeye alishauri kama wachina ndo wanafanya hiyo kazi vizuri, basi wapewe huo mradi ili wae committed na kama wakala.
Kimkataba sio Jambo jepesi hivyo, mwarabu Amepewa kandarasi ya kutengeneza bwawa,yeye ndio atajua anaajiri makampuni gani ktk vipande gani ili kumaliza kazi aliyopewa kwa ubora na kwa wakati.
 
Sijui kama taifa lini tutaacha usiri ktk kuingia mikataba mikubwa ya nchi yetu. Kukosekana kwa uwazi, tamaa ya kupata sifa binafsi kama kiki ya kisiasa, na pia tamaa ya kunufaika binafsi na kificho kutokana na fedha ya umma kwa njia za kifisadi ndizo sababu kubwa kila siku tunapigwa na wajanja.

Kabla ya utekelezaji wa miradi yote mikubwa inatotaka kuingiwa na serikali; Je! Ni kwa nini isijadiliwe kwanza bungeni ili kuweza kuzungumziwa kwa upana zaidi? Hivi ni kwa nini serikali hupenda sana kuingia mikataba kama hii kwa usiri mkubwa?

Mimi nafikiri tuelekeapo ktk uchaguzi mkuu, hapa napo panahitajika kuhojiwa na hata kupata majibu ya uhakika. Serikali imefanikiwa kuleta sheria nyingi kandamizi, matokeo yake tunakosa vyombo makini vya habari za kiitelejensia vyenye kuweza kuibua madudu ndani ya awamu hii ya tano, kwa ama kuogopa vitisho vya vyombo vya dola au hata kukabiliana na mkono wa sheria.
 
Hahaahahahhahaahahaahahahah unakuta naitwa Dr Mubarak Ni mfagizi wa kampuni nimekuja kuleta barua ya maombi kwenye huu mradi
Mkuu wengi mno ,nakambuka huko Chuo kikongwe huko Alexandria Egypt mwaka 1987 alikuwepo mwalinu mmoja kijana ana Phd mbili za Engineering kutoka UK,USA akisaka PHD ya tatu.
 
Wabongo kwa nongwa hatujambo walisema mradi utaharibu mazingira mara hakuna pesa za ujenzi sasa ujenzi unaendelea wanasema mwarabu hana uwezo ukweli ni kwamba mradi utafanikiwa na umeme utapatikana
 
Usimlaumu mwarabu, huyo alijaribu bahati yake kwenye tender ilivyotangazwa akashinda, mlaumu aliempa kazi mwarabu, huyo ndie tatizo haswa, huwezi jua huyo mwarabu alitoa nini mpaka akapewa hiyo kazi.
Kumbe basi mwaarabu ni mjanja ametumia fursa vizuri 'opportunity seeker' He is using other people's skillsets
 
Kabudi aitaja Timu ya "Taifa" ya wahandisi wa kiTanzania Stiegler's Gorge

Mhandisi Robert Kabudi msimamizi wa mkataba wa ujenzi wa JNHPP mwenye miaka 20 ya kusimamia miradi mikubwa ya ujenzi nje ya Tanzania pamoja na wahandisi wengine mahiri wazalendo wapo ktk mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji linatotegemewa kuzalisha 2115 MW wa umeme Tanzania. Mhandisi Robert anaitaja timu hiyo ya watu 21, kikosi anacho kibainisha kama timu ya kutizamwa duniani.


Timu hiyo ya wahandisi wa kiTanzania walio na ujuzikazi kwa vitendo, kuna mhandisi aliyepata kusimamia mradi wa kiwanja cha ndege cha Dubai kilichokuwa na bajeti ya zaidi ya US$ 3.5Bn. Miradi mikubwa ya Qatar, Abu Dhabi, Botswana , World Cup Africa Kusini wahandisi wake wakiTanzania wazalendo walishiriki ktk ujenzi huko ughaibuni.

Wahandisi hao chini ya kitengo cha Tanroads Engineering Consultanting Unit TECU wana kiu ya kuongeza CV zao ktk mradi huu wa Rufiji wenye bajeti kubwa kuliko iliyotumika ktk ujenzi wa Uwanja Mkubwa Mpya wa Ndege Dubai na hivyo si tu kuitambulisha Tanzania bali hata wahandisi wazalendo waTanzania kwa ulimwengu, kukitokea mradi wowote mkubwa nje ya Tanzania watapata kuitwa.
 
Kwani hiyo project bei gani?

Nachojua katika project kama hizo lazima awepo main contractors na sub hata katika ujenzi wa SGR wapo sub contractors kibao
 
Naona wengi humu mnakuja na negativity kwa kutoa taarifa. Naishia hapo sina haja ya vijembe vya kijinga na ushabiki wa kipuuzi
Itakuwa umehubiriwa kanisani leo. Nawe mbio ukaleta humu bila utafiti.
 
Utakuwa muathirika wa yule mtetezi wa ushoga aliyepo Ubelgiji
 

Wewe umesema kampa mchina 90% sasa wasiwasi wako upo wapi kama kazi hiyo bado inafanywa mchina?
Sema wapi pana mapungufu ili pafanyiwe kazi.
 
Wewe umesema kampa mchina 90% sasa wasiwasi wako upo wapi kama kazi hiyo bado inafanywa mchina?
Sema wapi pana mapungufu ili pafanyiwe kazi.
cha kuangalia ni time frame kwa kila stage na ubora wa vifaa vinavyotumiwa! lazima work plan yao iwe shared ili wafanyiwe tathmini kupitia hiyo plan!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…