Mradi wa Stieglers: Mwarabu anaharibu mradi hana utaalam wala ujuzi wa kujenga bwawa, italeta hasara kubwa kwa taifa na ubora hafifu

Hata mimi nikipata taarifa toka juu kuwa wewe ni Mtanzania wa kwanza kwenda mwezini huku nikijua wewe ni kilaza wa Darasa la 7 sitakulaumu wewe wala kilaza mwingine aliyesambaza taarifa bali kwa kujiamini kabisa nitasema huo ni utani wa kilaza mwingine anayedanganya wananchi kwa ujinga wake anayetaka atambulike. Kuna mtu alisema Watanzania siyo wajinga ni kweli lakini wajinga kama wewe pia wapo tena wengi zaidi.
 
 
Watu mna vichwa vigumu, sasa success ya MWENDOKASI ni nini? Let us be serious!!
Watu wa Kimara Mbezi wanalalamika kila chao, wewe unasema eti nchi za nje wanakuja kujifunza huku. Labda wanakuja kuona MLIVYOFELI
 
Tujiandae na visingizio lukuki maana hilo tunaliweza sana
 
We una utaalamu kiasi gani au ndio utaalam kwenye mambo ya majungu na fitna za kiafrika?

Najua unatamani mradi ufeli ili upate cha kuongea, kwa uwezo wa Mungu mradi utaisha na nchi itanufaika sana
Wacha unafiki na akili za kichawi kwa kujifanya kuwa huo mradi ni mali ya ccm,huo mradi ni Mali ya watanzania maana unajengwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania hata kama ni za kukopa maana tutakao lipa ni wataanza woote
 
Chadema kazi mnayo,wewe unaumia na nn? Baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mmeishiwa hoja mmebaki kubwabwaja na kukosoa miradi ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM .Tulieni CCM ikamilishe miradi yake iliyowahaidi wananchi baada ya hapo ndiyo mje muhoji mafanikio yake vinginevyo pelekeni porojo zenu kwenye vikao vyenu CCM mbele kwa mbele
 
We una utaalamu kiasi gani au ndio utaalam kwenye mambo ya majungu na fitna za kiafrika?

Najua unatamani mradi ufeli ili upate cha kuongea, kwa uwezo wa Mungu mradi utaisha na nchi itanufaika sana
Chadema huyo wivu umemjaa baada ya kuona serikali ya CCM inatekeleza Ilani yake ya uchaguzi kwa vitendo.Shame on on you Chadema
 
Nasikia wanyama wamekuwa wanakimbia eneo siku hizi kwa kelele za mabomu
 
Mkuu,

Inavyoonesha wewe ni mwathirika wa uongozi uliopo hapo Bwawa la Mwalimu Nyerere

Nikuulize haya
1. Nyumba za maboksi mlizojengewa na mchina kisha kubaguliwa kwa ngozi nyeusi ambapo chumba kimoja zaidi ya watu kumi mchanganyiko na mwajiri wako yaani HR meneja !!!
2. Nyumba mbadala zilishajengwa baada ya za kwanza kuungua moto?
3. Je, mlisharuhusiwa kupika chakula wenyewe au bado marufuku hiyo ipo pale pale?
4. Wafanyakazi wasio na nyumba kambini bado wanasafirishwa kama mizigo kwenda Mloka na Kisaki huku mmeshonwa kama ng'ombe wanaotoka mikoani?
5. Nyumba za fulu suti mabati watu zaidi ya mia zilishabadilishwa na kujengwa zenye hesima ya binadamu?
6. Vipi hali ya afya na usalama wakati wa ulipuzi miamba inayowabana hadi kifo au kupoteza viungo bila ya bima?

Mwisho: Waarabu sio watenda kazi ya maana, Wachina wanafanya kazi sana usiku kucha lakini pia ni wabaguzi na hawazingatii maslahi bora ya mfanyakazi. Huwezi kuamini meneja uajiri hana uwezo wa kusimamia maadili na nidhamu kwa wafanyakazi ambao ndio wajibu wake badala yake bosi wa Kichina au Kiarabu ndiye mwamuzi, kama hakutaki ndio hivyo tena; sheria hazifuatwi ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…