Mradi wa TADB yanufaisha Vijana Mwanza kwa fursa ya ufugaji wa kisasa wa samaki kwa vizimba

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi zinatekeleza mradi wa Uvuvi unaohusisha miradi miwili yenye thamani ya TZS 25.1Bln ikihusisha mikopo ya boti za kisasa zenye thamani ya TZS 2.6 Bln na ufugaji samaki kwa njia ya vizimba vyenye thamani ya TZS 12Bln katika mikoa mitano inayozungukwa na Ziwa Victoria

Hii inahusisha mikoa ya Mwanza, Geita Kagera, Simiyu na Mara ambapo makundi mbalimbali yamefikiwa ikiwa ni pamoja na Vikundi (CBOS), Vyama vya Uvuvi (FICOS), Makampuni na Watu Binafsi
Mradi wa ufugaji samaki unahusisha jumla ya vikundi vya wanufaika 120 ikiwa na jumla ya vizimba 507 vyenye thamani ya TZS 12 Bln na jumla ya wanufaika katika mradi ikiwa 3122

Aidha wanufaika wa mradi waligawanywa katika awamu mbili za utekelezaji, hii ni kutokana na sababu za kiuchumi ili kupishanisha nyakati za uvunaji kuepukana na changamoto ya masoko pindi wanapofikia hatua ya uvunaji

Katika awamu ya kwanza mradi umevifikia vikundi 50 vya wanufaika kwa kugawa vizimba 222 ikiwa na jumla ya wanufaika 1,213, wanawake 295 na vijana 903. Katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi inayoendelea tunatarajia kuvifikia vikundi 70 vya wanufaika ambapo vizimba 285 ikiwa na wanufaika 1,909, wanawake 571 na vijana 1,332

Matokeo ya mradi huu ni kama yafuatayo;

Mradi umetengeneza ajira kwa vijana katika tasnia ya uvuvi na kuongeza pato la samaki kwa mikoa inayozungukwa na Ziwa Victoria

Kwa wanufaika wa awamu ya kwanza wameweza kutengeza faida katika uvunaji mpaka kufikia tani 389.8 za samaki ambao kwa asilimia kubwa yameuzwa ndani ya mkoa

Wanufaika wameweza kulipa mikopo yao kwa asilimia 59.93% kwa rejesho la kwanza na huku matarajio yakiwa ni kufanya vizuri Zaidi katika mizunguko inayofata

1758097765417.png
 
🤣🤣h

apo Chakula cha hao samaki ni imported na hivyo vizimba made in Makoroboi Street -Mwanza🤣🤣 vizimba vina standard zake ili Upepo,Mawimbi, Jua visiwape stress Samaki waliomo ndani yake! Alafu sijui kama hawa samaki wameguzwa kuwa madume hili yakue haraka kwa muda mfupi! Hii pia ni sarakasi ingine ziwani😭 Ee Mungu Baba tusaidie
 
Attachments

  • 20250927_170646.jpg
    20250927_170646.jpg
    165.2 KB · Views: 29
Back
Top Bottom