Wapendwa wana JF, heshima kwenu, pia poleni na pilika za maisha.
Back to the topic;
Mwenzenu nimechoshwa na kazi ya kuishi kwa kutegemea mshahara. Nataka kuwa mjasiria mali hasa katika ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
NB: Naomba mniambie zile nyasi za kulishia ngo'ombe wa maziwa ndani (Zero grazing) zile ambazo huwa zinapandwa na kuvunwa -ZINAITWAJE? NAWEZA KUZIPATA WAPI (MBEGU ZA HIZO NYASI) ili nizioteshe mwenyewe huku niliko..maana kununua sitoweza.
Nataka kuanza na ng'ombe watatu wa maziwa approx. kila ngo'mbe anipe lita 12 za maziwa kwa siku = Lita 36....je kwa mlio wazoefu na ufugaji hii hesabu yangu yaweza kutimia au nime-over estimate?
Natangulisha shukrani wadau.