Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Gesi tayari ina mikataba tata isiyo na manufaa ya kutosha kwetu. Kumbuka tushaambiwa gesi mabepari washaichukua. Magufuli anafanya kitu sahihi mkuu
 
Kwa hili nipo na Magufuli asilimia mia moja, mambo mazuri lazima tumpongeze Rais wetu, tumkosoe kwa yake mabaya tu
Katika hili anastahili kukosolewa, katika dunia ya leo utafiti ni kitu mhimu. Huwezi kipinga ripoti ya utafiti bure bure tu.
 
hao watu wa bonde nao waliniangusha Sanaa.
nikashangaa mhifadhi MKUU analalama
katika swala la ki mazingira wapo sahihi 100%
 
Heshima kwenu wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, huenda akatumbuliwa kutokana na kuwa kikwazo katika Ujenzi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station.

Inasemekana January Makamba kaunda tume ya Wataalam wa kuchunguza athari zinazoweza kutokea iwapo Mradi huo Utajengwa.

Inadaiwa Sababu alizozitoa Kwa jicho la kitaalam ni kwamba wanatumiwa na Watu wasiopenda Mradi huu Ujengwe.

Leo katika uzinduzi wa Daraja la Mfugale, rais Magufuli amesikika akilalamikia wataalam ambao walifanya utafiti huo wa mradi wa umeme na akasema atashangaa hao wataalam wakiendelea kikaa ofisini.

Amedai wataalam wa mazingira walikuja na sababu za hovyo kabisa kwamba kila mtu atazishangaa. Kwamba mtu anatakiwa akajisaidie KM 20 kutoka kwenye mradi, Udongo utakaotumika unatakiwa uwe unapimwa, Gari ikiharibika haitakiwi itengenezewe kwenye mradi, mchicha kutoka maneo yale hautakiwi kwamba vitaharibu uoto wa asili.

Kadai maji yale yanatoka huko Mbeya na vinyesi na wanyama wamefia humo. Akashangaa hao wataama ambao sio wazalendo wanatoka wapi?.

Rais kasema Mradi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station lazima ujengwe.

STIEGLER’S gorge inapatikana katika hifadhi ya Selous (SGR) yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 ambayo ilipitishwa kuwa moja ya Sehemu yenye URITHI WA DUNIA mwaka 1982. Katika moja ya tafiti zilizofanyika huko nyuma miaka ya 1960s na baadae miaka ya 1980s ulitanabaisha uwezekano wa kujengwa bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme 2100MW kwa kutumia Maji kutoka katika bonde la mto Rufiji.

Baadae umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali yahusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira, zilifanya utafiti wa kubaini kama kuna athari zozote za kiokolojia na za kimazingira zingeweza kutokea iwapo mradi huo wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye takribani kilometa za mraba 12,000 utatekelezwa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.

JE, MADHARA HAYO NI YAPI YATAKAYOTOKANA NA UJENZI WA MRADI HUO?

Madhara nitayaeleza kwa kifupi kama yalivyoelezwa katika Ripoti ya WWF kama ifuatavyo;

1) Ikolojia katika hifadhi ya Selous na bonde la mto Rufiji utaathiriwa. Zaidi ya viumbe hai 200,000 watakuwa kwenye hatari.

2) Shughuli za kijamii na kiuchumi zitaathiriwa sana hasa maeneo ya Mkondo wa chini(downstream) wa bonde hilo la mto Rufiji. Mmomonyoko wa ardhi, ukosefu wa rutuba na hatari ya kuzorota kwa bandari kwa sababu zile sediments(masalia) yote ambayo yalitakiwa kufika kwenye downstream yatabakia kwenye hilo Bwawa kubwa litakalojengwa.

3) Ujangili kuongezeka maradufu zaidi ilivyo sasa katika hifadhi ya Selous, ambayo itaiweka hifadhi hiyo katika hali mbaya mnoo. Mpaka sasa hifadhi hiyo iliyo na hadhi ya URITHI WA DUNIA imetajwa kuwa katika moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na ujangili. Hivyo serikali iliweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo, lakini ujuo wa hili bwawa utakizana na jitiahada hizo za kuirudisha Hifadhi ya Selous kurudi katika ubora wake.

Pia katika Ripoti ya 2017 iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uasilia la WWF(World Wide Fund for Nature), baada ya kufanya utafiti wao walipendekeza mradi huo usitishwe kutoka na madhara yatakayo tokea baadae.

Bwana la umeme linatarajiwa kujengwa lina ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama tofauti.

Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, limesema kuwa linaitaka serikali kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo hilo ili kuhakikisha madhara yote yanabainika kabla ya mipango yoyote ya mradi huo kuanza.

Mradi huo unatarajiwa kugharimu dola bilioni mbili za Marekani

JE, HAKUNA MBADALA WA KUZALISHA 2100MW ILI KUIOKOA HIFADHI HIYO?

Nchi yetu imejaaliwa nishati nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kupata Megawati 2100 na zaidi.

1)Tunaweza kuzalisha umeme wa maji kutoka bonde la Mto Rufiji mbali na bwawa la stiegler’s gorge

2) Tuna gesi ya kutosha, na uzuri pia kuna miradi ambayo ipo kwenye PSMP(mpango wa kuongeza umeme katika gridi ya taifa) shida ni kuwa tunataka vya haraka haraka haraka ambavyo vitatugharimu hapo baadae. Tatizo gesi sio tegemeo tena kwa upande mwingine.Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums

3) Kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Geothermal katika bonde la Rift valley, kwa kuwa wenzetu Kenya ambao wamepitiwa bonde hilo wanafurahia uwepo wa geothermal kwao.

4) Tuna Makaa ya mawe tunaweza kutumia kuzalisha umeme.

5) Pia kuna utafiti uliofanyika unaeleza kuwa tuna uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia Upepo katika mikoa ya katikati ya TZ (singida, Dodoma)

MAAMUZI YA KISIASA

Mwaka Jana, Juni 2017 Rais Magufuli alitoa kauli ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bwawa hilo la STIEGLER’S GORGE na kupuuza tafiti zilizofanywa zinazoonesha athari za kimazingira za mradi huo. Badala ya kutumia nishati mbadala zilizopo.

Lakini kupitia taasisi zetu za ndani yaani RUBADA(Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji) na NEMC wote wametoa baraka zao za mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la STIEGLER’S gorge kwa ajili ya uzalishaji umeme uendelee.
Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous - JamiiForums

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge - JamiiForums
Mm nachouliza je wamejiridhisha maji hayata pungua na kusababisha lisifanye kazi,? Maana mabwawa ya kuzalisha umeme makubwa yapo katika mto huohuo,
 
moja ya matatzio ya watanganyika ni UJINGA.
WA KUTOYATAMBUA/KUYAKABILI MAZINGIRA YAO.
mradi Unaweza fanyika lakini je?kuna mpango mkakati wa kuitunza na kuifadhi ecology na mfumo wa pale??? nisingeprnda yale ya kihansi yajitokeze
 
Huyu February Marope haivi na Ngosha, tangu wakati ule aliporusha mtandaoni zile katuni zake zenye ujumbe wa kejeli.

Hii ni mara ya pili anashambuliwa hadharani.
IMG_20180927_131314.jpg
 
Wakuu mi naomba kuuliza hili jina Stiegler's Gorge limetoka wapi katika huu mradi hili si ni la kiingereza hili liliingiaje mpaka huko mto Rufiji?
Samahi wakuu naomba mnieleweshe.......by the way mi naomba huo mradi utekelezwe tu popote pale palipofanyika maendeleo lazima uharibifu wa maendeleo utokeee hatuwezi kuuepuka hata hao wazungu wameharibu sana mazingira wakati wanajenga miji yao nani aliwazuia wakati huo kwa nini sisi huku Africa inakuwa nongwa?
Huyu Jiwe vitu karibu vyote huwa simuungi mkono lakini katika hili niko pamoja nae iwe kuna kuharibu mazingira ama la hata ukisoma sababu zenyewe ni za kipuuzi tu......mi nasema umeme ujengwe na hakuna wa kutuzuia
 
Heshima kwenu wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, huenda akatumbuliwa kutokana na kuwa kikwazo katika Ujenzi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station.

Inasemekana January Makamba kaunda tume ya Wataalam wa kuchunguza athari zinazoweza kutokea iwapo Mradi huo Utajengwa.

Inadaiwa Sababu alizozitoa Kwa jicho la kitaalam ni kwamba wanatumiwa na Watu wasiopenda Mradi huu Ujengwe.

Leo katika uzinduzi wa Daraja la Mfugale, rais Magufuli amesikika akilalamikia wataalam ambao walifanya utafiti huo wa mradi wa umeme na akasema atashangaa hao wataalam wakiendelea kikaa ofisini.

Amedai wataalam wa mazingira walikuja na sababu za hovyo kabisa kwamba kila mtu atazishangaa. Kwamba mtu anatakiwa akajisaidie KM 20 kutoka kwenye mradi, Udongo utakaotumika unatakiwa uwe unapimwa, Gari ikiharibika haitakiwi itengenezewe kwenye mradi, mchicha kutoka maneo yale hautakiwi kwamba vitaharibu uoto wa asili.

Kadai maji yale yanatoka huko Mbeya na vinyesi na wanyama wamefia humo. Akashangaa hao wataama ambao sio wazalendo wanatoka wapi?.

Rais kasema Mradi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station lazima ujengwe.
View attachment 879376
STIEGLER’S gorge inapatikana katika hifadhi ya Selous (SGR) yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 ambayo ilipitishwa kuwa moja ya Sehemu yenye URITHI WA DUNIA mwaka 1982. Katika moja ya tafiti zilizofanyika huko nyuma miaka ya 1960s na baadae miaka ya 1980s ulitanabaisha uwezekano wa kujengwa bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme 2100MW kwa kutumia Maji kutoka katika bonde la mto Rufiji.

Baadae umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali yahusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira, zilifanya utafiti wa kubaini kama kuna athari zozote za kiokolojia na za kimazingira zingeweza kutokea iwapo mradi huo wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye takribani kilometa za mraba 12,000 utatekelezwa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.

JE, MADHARA HAYO NI YAPI YATAKAYOTOKANA NA UJENZI WA MRADI HUO?

Madhara nitayaeleza kwa kifupi kama yalivyoelezwa katika Ripoti ya WWF kama ifuatavyo;

1) Ikolojia katika hifadhi ya Selous na bonde la mto Rufiji utaathiriwa. Zaidi ya viumbe hai 200,000 watakuwa kwenye hatari.

2) Shughuli za kijamii na kiuchumi zitaathiriwa sana hasa maeneo ya Mkondo wa chini(downstream) wa bonde hilo la mto Rufiji. Mmomonyoko wa ardhi, ukosefu wa rutuba na hatari ya kuzorota kwa bandari kwa sababu zile sediments(masalia) yote ambayo yalitakiwa kufika kwenye downstream yatabakia kwenye hilo Bwawa kubwa litakalojengwa.

3) Ujangili kuongezeka maradufu zaidi ilivyo sasa katika hifadhi ya Selous, ambayo itaiweka hifadhi hiyo katika hali mbaya mnoo. Mpaka sasa hifadhi hiyo iliyo na hadhi ya URITHI WA DUNIA imetajwa kuwa katika moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na ujangili. Hivyo serikali iliweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo, lakini ujuo wa hili bwawa utakizana na jitiahada hizo za kuirudisha Hifadhi ya Selous kurudi katika ubora wake.

Pia katika Ripoti ya 2017 iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uasilia la WWF(World Wide Fund for Nature), baada ya kufanya utafiti wao walipendekeza mradi huo usitishwe kutoka na madhara yatakayo tokea baadae.

Bwana la umeme linatarajiwa kujengwa lina ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama tofauti.

Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, limesema kuwa linaitaka serikali kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo hilo ili kuhakikisha madhara yote yanabainika kabla ya mipango yoyote ya mradi huo kuanza.

Mradi huo unatarajiwa kugharimu dola bilioni mbili za Marekani

JE, HAKUNA MBADALA WA KUZALISHA 2100MW ILI KUIOKOA HIFADHI HIYO?

Nchi yetu imejaaliwa nishati nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kupata Megawati 2100 na zaidi.

1)Tunaweza kuzalisha umeme wa maji kutoka bonde la Mto Rufiji mbali na bwawa la stiegler’s gorge

2) Tuna gesi ya kutosha, na uzuri pia kuna miradi ambayo ipo kwenye PSMP(mpango wa kuongeza umeme katika gridi ya taifa) shida ni kuwa tunataka vya haraka haraka haraka ambavyo vitatugharimu hapo baadae. Tatizo gesi sio tegemeo tena kwa upande mwingine.Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums

3) Kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Geothermal katika bonde la Rift valley, kwa kuwa wenzetu Kenya ambao wamepitiwa bonde hilo wanafurahia uwepo wa geothermal kwao.

4) Tuna Makaa ya mawe tunaweza kutumia kuzalisha umeme.

5) Pia kuna utafiti uliofanyika unaeleza kuwa tuna uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia Upepo katika mikoa ya katikati ya TZ (singida, Dodoma)

MAAMUZI YA KISIASA

Mwaka Jana, Juni 2017 Rais Magufuli alitoa kauli ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bwawa hilo la STIEGLER’S GORGE na kupuuza tafiti zilizofanywa zinazoonesha athari za kimazingira za mradi huo. Badala ya kutumia nishati mbadala zilizopo.

Lakini kupitia taasisi zetu za ndani yaani RUBADA(Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji) na NEMC wote wametoa baraka zao za mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la STIEGLER’S gorge kwa ajili ya uzalishaji umeme uendelee.
Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous - JamiiForums

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge - JamiiForums
Mzee na ccm yake nchi imemshinda, ile gesi tuliyoambiwa ikichimbwa na kusafirishwa kwa bomba la Mtwara-Dar litamaliza matatizo yote ya nishati ya umeme na kuzaliwa umeme wa ziada zaidi ya MW 10,000, uko wapi sàsa?leo wanahangaika na Stiglerr's kwa MW 2100 tu.

Kweli mfa maji haachi kutapatapa.
 
Wakuu mi naomba kuuliza hili jina Stiegler's Gorge limetoka wapi katika huu mradi hili si ni la kiingereza hili liliingiaje mpaka huko mto Rufiji?
Samahi wakuu naomba mnieleweshe.......by the way mi naomba huo mradi utekelezwe tu popote pale palipofanyika maendeleo lazima uharibifu wa maendeleo utokeee hatuwezi kuuepuka hata hao wazungu wameharibu sana mazingira wakati wanajenga miji yao nani aliwazuia wakati huo kwa nini sisi huku Africa inakuwa nongwa?
Huyu Jiwe vitu karibu vyote huwa simuungi mkono lakini katika hili niko pamoja nae iwe kuna kuharibu mazingira ama la hata ukisoma sababu zenyewe ni za kipuuzi tu......mi nasema umeme ujengwe na hakuna wa kutuzuia
Mradi wa gesi umeishiwa wapi?? Kwa nini wang'ang'ane na vitu vua uharibifu wakati vitu vyenye madhara madogo tena gharama nafuu na very effective vipo??
 
Back
Top Bottom