Kuna kitu jiwe hakisemi au anapotosha:
1. Kuna ukataji wa miti karibia ukubwa wa jiji la dar. Dar ina sq Km 1393, sasa hapo ni miti inakatwa ukubwa huo bila uoga. Kama mnakata miti hiyo je sisi wanainchi ndo tutaiacha.
2. Jana kwenye habari ITV maji ya mto wami yamepungua sana mpaka mto sehemu kubwa imebakia ni mchanga vipi mamba, viboko na wanyawa wategemeao maji kuishi. Hamjalifikiria hili
3. Maji yanapopungua kuna magonjwa yanayosababishwa na uhaba wa maji eg anthrax
4. Kama kuna mamlaka ya maji basi inabidi watumie dawa nyingi kutibu maji nayo ni hasara kwasabu itatubidi tulipe zaidi kufidia
5. Kuna swala la mmomonyoko
6. Kuna swala la uharibifu mazingira eg. kuna watu zaidi ya 3000 kuishi kule porini hilo nalo ni janga.
7. Kuna mengi nashauri tuachana na mpango huo