Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Katika hili anastahili kukosolewa, katika dunia ya leo utafiti ni kitu mhimu. Huwezi kipinga ripoti ya utafiti bure bure tu.
Mimi nitakubali utafiti uliofanywa na waafrika kama Kenya,Somalia,Sudan Angola n.k sio hao white skin guys. Hata nyumbu waishe mbona kwao hakuna na wanaishi?
 

Awamu hii hili neno 'uzalendo' linatumika vibaya sana.

Tuombe uzima,kuna watu humu watabadili ID zao ili kula vyema matapishi yao.
 
Mimi ninachojua ni kwamba miaka kama mi 5 nyuma tuliaminishwa kwamba umeme wa gas utakuwa ni suluhisho la matatizo yote ya umeme nchini tena kwa bei nafuu..
Lakini mpaka sasa sijui hio gas imeenda wapi na kama huo umeme ulishaanza kuzalishwa au bado..

Na hii project mpya sina imani kama itakuwa tofauti na ile imani waliyotupa ya gas asilia
 
KWANINI WAZUNGU WAKATI WANTAKA URANIUMU MATAIFA YALIKUBALI ENEO KUMEGWA LAKINI KWENYE SISI KUZALISHA UMEME IMEKUWA SHIDA

Hapo ndio nnapokubaliana na Magu. Hawa watu wana ajenda zao. This world is not fair
 
Atumbuliwe tu ikibidi kama atakuwa yupo upande wa kukwamisha maendeleo ya nchi kwa maslahi yake binafsi au kwa kutumika bila kujua.
Maendeleo yanapokuja na athari nazo zingalimo ila inaangaliwa faida zaidi iko wapi. Nyumba za watu ngapi zinabomolewa kupisha maendeleo ya barabara au reli? Penye maslahi ya taifa tuweke siasa pembeni tujenge Taifa.
 
Twende baba Ngosha! Kwani hawa si ndiyo wanaongoza kuzalisha hewa ya ukaa! mbona viwanda vyao hawafungi? nasi tuende mbele hakuna kuangalia nyuma.
 
Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.
UNESCO walichukua hatua gani kulinda Urithi wa Dunia wa Palamilya huko Syria...hakuna...sana sana walikaa kimya kama hawaoni kinachofanywa na wahuni wale waliokuwa wanasadikiwa kusaidiwa na nchi za magharibi. Watuache...hizi UN organs wakati mwengine zinatumiwa vibaya kuhujumu maedeleo ya nchi changa! Tuwe makini.
 
Magu mambo kwa hili nakuomba ubadilishe njia vipo vyanzo ambavyo havi hitaji mbwembwe fuata ushauri wa heche na dk lisu
 
Gesi tayari ina mikataba tata isiyo na manufaa ya kutosha kwetu. Kumbuka tushaambiwa gesi mabepari washaichukua. Magufuli anafanya kitu sahihi mkii
Magufuli namkubali sana kwenye utendaji. Jamaa ana maono makubwa sana na ya kimaendeleo kwa taifa hili. Tatizo lake moja tu, hana washauri wazuri. Wengi waliomzunguka kazi kujipendekeza tu. Rais anapiga kazi peke ake, anabuni miradi ya maendeleo peke yake. Watendaji wake wa chini hakuna wanachokifanya zaidi ya kumsifia tu. Angepata watu wabunifu, wachapa kazi kama yeye hii nchi ingepaa kiuchumi kwa muda mdupi sana.
 
Amtumbue tuu ili angalo JANUARY AONDOKANE na nuksi ya kuwa kwenye cabinet la kichaa kabisa maana yeye. Hafanani na huyo kichaa... January baba you deserve more not this
 
Mimi huwa sielewi nchi kama Tanzania kusema kuna uharibifu wa mazingira kwenye miradi mikubwa, unakuta tunakomaa na mikataba ya kimataifa kuhusu mazingira kiasi kwamba hapa Tanzania tunaharibu mazingira hadi dunia inatuangalia, kwa ufupi tunapoteza muda na kujichelewa wenyewe, Huwezi ukajenga stieglers gorge moja ukaniambia environmental impacts,nchi kama china watasemaje? ambao hata kuiona tu nyota kwao ni ndoto, ufaransa anga lao ni chafu kwa sababu ya viwanda vingi vinatoa moshi muda wote, leo Tanzania anga letu ni bule sky na haliwezi kuwa affected by one gorge, ndio maana utashangaa baadhi ya mataifa yakifika Africa hupiga picha hadi Rain bow/Nyota wakati wa usiku mmewahi kujiuliza kwa nini? jibu ni kuwa wao walichagua maendeleo ya viwanda/umeme wa uhakika kwa ajri ya wananchi wetu huku mataifa yale yale yanakuja na sera za environmental effects kwa wajinga waafrica,na sisi tulivyo kweli tunapoteza muda kujadili mambo kama hayo ,hatimaye tubaki katika wimbi la umasikini miaka yote.

Kama tumezamilia kukamilisha miradi huu, tuachane na story majukwaani, tutafute pesa na mkandalasi apatikane apewe chake/down payment kazi ifanyike, mradi kama huu nchi ya kuweza kutoa msaada wa pesa ni china, Japan,korea huko, western countries ni ngumu, tuachane na kelele za mazingira, kwa nini kupoteza muda mwingi kuwafurahisha mataifa ya nje kwa ajiri ya mazingira wakati huo viwanda havina umeme, sisi wenyewe hatuna umeme?
 
Gesi tayari ina mikataba tata isiyo na manufaa ya kutosha kwetu. Kumbuka tushaambiwa gesi mabepari washaichukua. Magufuli anafanya kitu sahihi mkii
Hata yule Wa gesi alisema itatunufaisha laini patupu....huyu nae anasema hili bwawa litatunufaisha....I think it is not true
Lakini si walireview masheria ya madini na gesi au niliachwa sehemu?
Kama wwliyarekebisha kwa nn hao wanaume Wa magesi hawagusiki?
 
Kuna Wataalamu koko waliopendekeza kuwa vyoo vijengwe kilomita 10 kutoka mradi wa umeme wa Stigler gorge ulipo kwa kusema utachafua mazingira vyoo vikiwa eneo la mradi!!!!!.Mbona vyoo visivyochafua mazingira vipo .ukiwa Na mikutano au sherehe mbona watu huvileta? Hao Wataalamu koko hawajui hilo kuwa viko vyoo visivyoharibu mazingira? Hadi watoe ushauri wa kijinga kama huo? Timua wote
 
Back
Top Bottom