Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mtapata tabu sana
Mshamba kweli wewe wengi wenye fikra ya mapinduzi nchi ukiona maisha yao utalia wanavyo-enjoy mkuu ila wanajitambua na kuona jinsi watanzania mnavyopigwa changa la macho na chichiem, wamewageuza matoi[emoji23][emoji23]
 
Heshima kwenu wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, huenda akatumbuliwa kutokana na kuwa kikwazo katika Ujenzi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station.

Inasemekana January Makamba kaunda tume ya Wataalam wa kuchunguza athari zinazoweza kutokea iwapo Mradi huo Utajengwa.

Inadaiwa Sababu alizozitoa Kwa jicho la kitaalam ni kwamba wanatumiwa na Watu wasiopenda Mradi huu Ujengwe.

Leo katika uzinduzi wa Daraja la Mfugale, rais Magufuli amesikika akilalamikia wataalam ambao walifanya utafiti huo wa mradi wa umeme na akasema atashangaa hao wataalam wakiendelea kukaa ofisini. Amewatuhumu kwamba wanatumiwa ili Watanzania wanyonge wasitumie umeme wa bei rahisi waendelee kutumia umeme wa mafuata ambayo ni ghari.

Amedai wataalam wa mazingira walikuja na sababu za hovyo kabisa kwamba kila mtu atazishangaa. Kwamba mtu anatakiwa akajisaidie KM 20 kutoka kwenye mradi, Udongo utakaotumika unatakiwa uwe unapimwa, Gari ikiharibika haitakiwi itengenezewe kwenye mradi, mchicha kutoka maneo yale hautakiwi kwamba vitaharibu uoto wa asili.

Kadai maji yale yanatoka huko Mbeya na vinyesi na wanyama wamefia humo. Akashangaa hao wataalam ambao sio wazalendo wanatoka wapi?.

Rais kasema Mradi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station lazima ujengwe.
View attachment 879376
STIEGLER’S gorge inapatikana katika hifadhi ya Selous (SGR) yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 ambayo ilipitishwa kuwa moja ya Sehemu yenye URITHI WA DUNIA mwaka 1982. Katika moja ya tafiti zilizofanyika huko nyuma miaka ya 1960s na baadae miaka ya 1980s ulitanabaisha uwezekano wa kujengwa bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme 2100MW kwa kutumia Maji kutoka katika bonde la mto Rufiji.

Baadae umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali yahusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira, zilifanya utafiti wa kubaini kama kuna athari zozote za kiokolojia na za kimazingira zingeweza kutokea iwapo mradi huo wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye takribani kilometa za mraba 12,000 utatekelezwa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.

JE, MADHARA HAYO NI YAPI YATAKAYOTOKANA NA UJENZI WA MRADI HUO?

Madhara nitayaeleza kwa kifupi kama yalivyoelezwa katika Ripoti ya WWF kama ifuatavyo;

1) Ikolojia katika hifadhi ya Selous na bonde la mto Rufiji utaathiriwa. Zaidi ya viumbe hai 200,000 watakuwa kwenye hatari.

2) Shughuli za kijamii na kiuchumi zitaathiriwa sana hasa maeneo ya Mkondo wa chini(downstream) wa bonde hilo la mto Rufiji. Mmomonyoko wa ardhi, ukosefu wa rutuba na hatari ya kuzorota kwa bandari kwa sababu zile sediments(masalia) yote ambayo yalitakiwa kufika kwenye downstream yatabakia kwenye hilo Bwawa kubwa litakalojengwa.


3) Ujangili kuongezeka maradufu zaidi ilivyo sasa katika hifadhi ya Selous, ambayo itaiweka hifadhi hiyo katika hali mbaya mnoo. Mpaka sasa hifadhi hiyo iliyo na hadhi ya URITHI WA DUNIA imetajwa kuwa katika moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na ujangili. Hivyo serikali iliweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo, lakini ujuo wa hili bwawa utakizana na jitiahada hizo za kuirudisha Hifadhi ya Selous kurudi katika ubora wake.

Pia katika Ripoti ya 2017 iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uasilia la WWF(World Wide Fund for Nature), baada ya kufanya utafiti wao walipendekeza mradi huo usitishwe kutoka na madhara yatakayo tokea baadae.

Bwana la umeme linatarajiwa kujengwa lina ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama tofauti.

Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, limesema kuwa linaitaka serikali kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo hilo ili kuhakikisha madhara yote yanabainika kabla ya mipango yoyote ya mradi huo kuanza.

JE, HAKUNA MBADALA WA KUZALISHA 2100MW ILI KUIOKOA HIFADHI HIYO?

Nchi yetu imejaaliwa nishati nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kupata Megawati 2100 na zaidi.

1)Tunaweza kuzalisha umeme wa maji kutoka bonde la Mto Rufiji mbali na bwawa la stiegler’s gorge

2) Tuna gesi ya kutosha, na uzuri pia kuna miradi ambayo ipo kwenye PSMP(mpango wa kuongeza umeme katika gridi ya taifa) shida ni kuwa tunataka vya haraka haraka haraka ambavyo vitatugharimu hapo baadae. Tatizo gesi sio tegemeo tena kwa upande mwingine.Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums

3) Kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Geothermal katika bonde la Rift valley, kwa kuwa wenzetu Kenya ambao wamepitiwa bonde hilo wanafurahia uwepo wa geothermal kwao.

4) Tuna Makaa ya mawe tunaweza kutumia kuzalisha umeme.

5) Pia kuna utafiti uliofanyika unaeleza kuwa tuna uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia Upepo katika mikoa ya katikati ya TZ (singida, Dodoma)

MAAMUZI YA KISIASA

Mwaka Jana, Juni 2017 Rais Magufuli alitoa kauli ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bwawa hilo la STIEGLER’S GORGE na kupuuza tafiti zilizofanywa zinazoonesha athari za kimazingira za mradi huo. Badala ya kutumia nishati mbadala zilizopo.

Lakini kupitia taasisi zetu za ndani yaani RUBADA(Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji) na NEMC wote wametoa baraka zao za mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la STIEGLER’S gorge kwa ajili ya uzalishaji umeme uendelee.

Faida ya Stiegler’s Gorge ni nishati ya umeme. Kama ambavyo Rais Dk. John Magufuli amekuwa na shauku ya kutengeneza bwawa la maji kwenye bonde hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 ikitumia zaidi ya Dola 2 bilioni (zaidi ya TSh4.5 trilioni)

Kusudio hilo si geni, bali ni mwendelezo wa kutimiza dhamira ambayo aliiweka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, takribani miongo minne iliyopita. Mwali Nyerere alikuwa na wazo la kujenga bwawa la umeme katika eneo hilo ili kusaidia nchi kupata umeme wa kutosha.

Kwa udadisi wa juu juu uliofanywa unaonyesha kuwa, chimbuko la wazo la kuwa na mradi wa Stiegler’s Gorge lilipata nguvu zaidi mwaka 1975, wakati Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alipoyapambanua mawazo yake juu ya umuhimu ya kuwa na mradi mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme katika bonde hilo.

Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huo ulipata vikwazo vingi, hususan vya uharibifu wa mazingira, ambavyo viliibuka kila panapokaribia utekelezaji wa mradi huo, tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza mpaka hivi sasa Rais Dk. Magufuli ameazimia kuutekeleza.

umeme unaozalishwa na TANESCO kwa sasa ni takribani megawati 1517.47 huku matumizi yakiwa ni takribani ni megawati 900.

Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous - JamiiForums

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge - JamiiForums
Naunga mkono kujengwa mradi huu kwa sababu zifuatazo:
1:bila umeme wa bei rahisi uchumi wetu hauwezi kukua kwani baada ya miaka 15 hutaona gari ya petroli tena nyingi zitakuwa za umeme,kwa kuwa mkwere kauza gesi hivi sasa tanesco wanauziwa bei ya soko na hivyo bado umeme utakuwa ghali.
2:ukisema mazingira yataharibika ukweli ni kuwa uzalishaji wote mkubwa wa umeme una madhara na mazingira uwe wa nyuklia au makaa ya mawe ukiangali huu wa bwawa ndiyo wenye madhara madogo kuliko hayo mengine,tukiangalia ukweli madhara ya kwanza tunatakiwa kupima ni kwa binadamu kwanza.
3.hao wanaotuma ngo kupiga kelele wangejali mazingira kwanza wao kwa kuzima mitambo inayo athiri watu wao kabla ya kutuingilia,unafiki wa marekani ni mkubwa kwanini wasisimamishe kuchimba mafuta wao,wakati mfumo wa uchimbaji wao unachafua mazingira na inasababisha tetemeko katika baadhi ya miji, hayo maji yanarudishwa ardhini imethibitishwa inaingiliana na mfumo wa maji safi na bado wanachimba na kurudisha maji ardhini baada ya kuchuja mafuta.
4:sielewi lini mtu mweupe akataka mwafrika awe na maendeleo ya kujitegemea,watu wanaosifiwa ni wale viongozi waliouza nchi kama hao wawili waliopita,wameuza kilakitu leo kodi yetu asilimia 60 zinalipa madeni na rasilimali imeisha,hao ndiyo viongozi bora kwa watu weupe.
 
Ww umebakia na wivu kwa makonda, dah! Jamaa ww noma sana
Lazima watu wawe na wivu naye maana sio kwa double standard anayopewa, kakwepa kodi kasamehewa, kavamia kituo cha clouds kachekewa tu sasa wewe muige uone cha moto....
 
Wapumbavu tu ninyi,huyo waziri alikuwa wapi?Katibu mkuu wa wizara alikuwa wapi?Mtajibeba wenyewe
Awamu hii Wataalamu muliozoea kuandika ripoti Potoshi kwa mawaziri Na makatibu wakuu ,wakuu wa taasisi,wakurugenzi nk mjiandae mtakiona cha mtema Kuni.Ukishauri chochote ujue mwisho wa siku ndio utadakwa kikiwa koko.Hao waliotoa huo Ushauri Raisi Magufuli usicheke nao ni ngedere hao ukicheka utakuta shamba lote wamemaliza wahindi.
 
Ukiona hivyo, ujue KICHAA hamshirikishi VP kwenye maamz mengi ya uendeshaji wa masuala ya Taifa

Environment docket inasimamiwa na VP

Sasa kuwananga Wataalam ni KUMNANGA VP
Acheni ujinga, unataka amshirikishe katika nini? Yaani aache Cabinet ambayo VP naye ni mjumbe akae pembeni kuchukua ushauri wa Mzanzibar?
Huyo VP kama ndiye anahusika na Makamba basi nao ni vilaza tu wanaojidai wanalinda mazingira wakati ni nil. Sidhani kama VP anahusika maana itakuwa kituko, Rais anamtuma kila siku nje ya Nchi anapiga bingo, hawezi kujiuliza mwenyewe na kumuacha JPM atuongoze anavyoona inafaa? Hawezi kumshukuru Rais kumtuma nje wakati mtaalamu wa mambo hayo FM yupo na huko ndiko kwao zaidi?
 
Awamu hii Wataalamu muliozoea kuandika ripoti Potoshi kwa mawaziri Na makatibu wakuu ,wakuu wa taasisi,wakurugenzi nk mjiandae mtakiona cha mtema Kuni.Ukishauri chochote ujue mwisho wa siku ndio utadakwa kikiwa koko.Hao waliotoa huo Ushauri Raisi Magufuli usicheke nao ni ngedere hao ukicheka utakuta shamba lote wamemaliza wahindi.
Ndio hao hao wanaccm,msitake kupumbaza watu
 
umesahau utafiti wa twaweza ulisema wanaoisapoti ccm ni wasiosoma? ndio maana wasomi/wataalamu wote wanahusishwa na chadema
Hata JPM kasoma,inamaana naye anahusishwa na Chadema
 
Kina nani? Watanzania?
Kwani nani wengine? Na wakiambiwa hivyo huwa wanapiga vigelegele balaa! Pombe anawaambia "kweli mtapata tabu sana" na wao wanashangilia "Ndiyoooooooooo! Sema baba sema baba tuko nyuma yako" pombe anatikisa kichwa,anajua kumbe haya majitu bado mapimbi!
 
Jamani nani mwenye historia ya huu miradi na kwa nini Nyerere aliuacha???

Alinyimwa pesa ya kujenga kutoka Benki ya Dunia na hakuwa na uwezo wa ndani kipindi hicho. Ndiyo akajenga Mtera na Kidatu.
 
Mbuga ya selous na nchi ya rwanda zinalingana. Randa watuheshimu kupita kiasi.
Yaani nchi yao huku kwetu tunafugia wanyama.
 
umesahau utafiti wa twaweza ulisema wanaoisapoti ccm ni wasiosoma? ndio maana wasomi/wataalamu wote wanahusishwa na chadema
Mimi nimesoma napinga choo kujengwa kilomita kumi kisa kinaharibu mazingira .Viko vyoo visivyoharibu mazingira kibao. Wataalamu waliotoa huo Ushauri wa kupinga vyoo visijengwe eneo la mradi ni Chadema wapinga mradi wanaotumia usomi kupinga mradi kwa ripoti koko iliyoandaliwa na Chadema na kutiwa sahihi ,kuhakikisha mamlaka husika na kusomwa na hao Wataalamu koko kwa niaba ya Chadema
 
Waacheni wavutane tu sisi watumiaji wa umeme tupo tayari kupokea maelekezo yoyote kuhusu umeme huo
 
Nyerere alikosa pesa za kujenga bwawa.Wakati huo IMF ilikuwa mwiba.Hata wale Scandinavia waliotaka kutusaidia walipewa friendly warning na Marekani.
Jamani nani mwenye historia ya huu miradi na kwa nini Nyerere aliuacha???
 
Mimi nimesoma napinga choo kujengwa kilomita kumi kisa kinaharibu mazingira .Viko vyoo visivyoharibu mazingira kibao. Wataalamu waliotoa huo Ushauri wa kupinga vyoo visijengwe eneo la mradi ni Chadema wapinga mradi wanaotumia usomi kupinga mradi kwa ripoti koko iliyoandaliwa na Chadema na kutiwa sahihi ,kuhakikisha mamlaka husika na kusomwa na hao Wataalamu koko kwa niaba ya Chadema
Ndio maana tunasema serikali/ccm haina wataalamu hadi inakodi wataalamu toka chadema wawafanyie kazi
 
Tafiti za wazungu naziamini sana, ugunduzi mkubwa na wakushangaza dunia hii umetokana na tafiti za wazungu. Umeshawahi fikiria sayansi ya tiba na ugunduzi wake au kompyuta na ufanyaji kazi wake wa maajabu. Utafiti wa mzungu unaweza kukupa matokeo ya miaka 200 ijayo. Utafiti wetu unalenga miaka ijayo ya uchaguzi.
 
Hongera kwa Mhe Rais kwa msimamo wake. Kuna chanzo kingine chenye uwezo wa kuzalishaza kama 500 MW nakifanyia utafiti nikiwa tayari nitaituma ripoti kwa KM- nishati na madini
 
Back
Top Bottom