Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Binafsi kwa maoni yangu huu mradi kikwazo kikubwa haiwezi kuwa mazingira bali ni Pesa, hivi tujiulize kama kuna nchi zina extract mafuta baharini na kuna Oil spill ambazo zina athari viumbe hai wa majini, watumia wa maji kama binadamu lakini watu wa mazingira tena mataifa makubwa yako kimya leo huu mradi wenu uwe na tatizo kweli? Gulf oil spill ilichukua zaidi ya miaka mitano, BP USA oil spill kipindi cha Obama na kadhalika, haya matukio yote lakini makampuni hayaachi kufanya research/explorations ya mafuta, sasa hivi inasemekana kuna wese Zanzibar je hamtachimba kwa sababu ya mazingira? common guys, tuone hata aibu kuzungumzia uhalibifu wa mazingira stiegler's ,focus yetu ingekuwa je tutapata pesa wapi? pia tutafaidika vipi?
 
Waache uhuni wa kutuvutia chini kwa sababu zao, mbona marekani hajari uharibifu wa mazingira kama kuzarisha hewa mpaka akajiondoa kwenye mkataba wa kyoto ili aendelee na programa zake na hakuna wa kuzungumzia tena uharibifu wake ni hatari zaidi hadi kusababisha mabadiriko ya hali ya hewa.
 
Mzee na ccm yake nchi imemshinda, ile gesi tuliyoambiwa ikichimbwa na kusafirishwa kwa bomba la Mtwara-Dar litamaliza matatizo yote ya nishati ya umeme na kuzaliwa umeme wa ziada zaidi ya MW 10,000, uko wapi sàsa?leo wanahangaika na Stiglerr's kwa MW 2100 tu.

Kweli mfa maji haachi kutapatapa.
Gas iliuzwa sasa ukichimba wenye gas yao watakushtaki, ni bora tuwaaachie miaka 50 kama wajukuu wataikuta hata kidogo nao wajirambe. chuma kimeamua tufanye ambayo haijauzwa. Umesahau ya bandari ya bagamoyo? nayo ingejengwa ilishauzwa miaka 50.
 
Huyo jamaa akishaamua hakuna wa kupinga ajenge tu hiyo sitigilaz goji maana si anafungu lake hapo la 50%?
 
Utaalamu na uzalendo ni mambo mawili tofauti,utaalamu hautakiwi kuathirika na kitu chochote. Kama una kansa na utaalamu wa Dr ukasema unahitaji kukatwa mguu, sio kwamba hakupendi, anakupa ushauri wa kitaalamu. Unaweza ukapokea au kukataa huo ushaur lakini usitukane utaalamu wake.

Siasa ndio zinaua utaalamu hapa nchini. Tanesco walisema Richmond haina uwezo, ofisi ya waziri mkuu ikaleta 'siasa'
 
....but kuna mtu akija kutoka madarakani hakuna namna itabidi tu akanyee debe hata kwa miezi 6 kama alivyofanyiwa Manji.

hakuna namna!
Si kunyea debe pekee, na kupigwa para kunamstahili, hadi mimba. Chezea UN wewe primitive wa ki hutu.
 
Uyu January alikuwa anatafutwa ila naona yeye hajui;kuna visa kafanya hapo nyuma kwamfano mvutano wa wapi ijengwe ofisi ya halmashauri Bumbuli,sakata la vibari vya mazingira kiwanda cha betri Kibaha na sasa Rufiji.Namamshauri ajiuzuru mwenyewe bila shuruti.
 
KWANINI WAZUNGU WAKATI WANTAKA URANIUMU MATAIFA YALIKUBALI ENEO KUMEGWA LAKINI KWENYE SISI KUZALISHA UMEME IMEKUWA SHIDA
Well said walahi
Na hichi kifebruary huwa kina uroho wa pesa kweli kweli walahi!
 
Uyu January alikuwa anatafutwa ila naona yeye hajui;kuna visa kafanya hapo nyuma kwamfano mvutano wa wapi ijengwe ofisi ya halmashauri Bumbuli,sakata la vibari vya mazingira kiwanda cha betri Kibaha na sasa Rufiji.Namamshauri ajiuzuru mwenyewe bila shuruti.
Umenena walahi
 
Nadhani sasa nivyema tukafanya vitu ambavyo wazungu hawataki labda itasaidia maana vitu vyote tulivyovifanya vinavyowapendeza havijatusaidia
 
Heshima kwenu wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, huenda akatumbuliwa kutokana na kuwa kikwazo katika Ujenzi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station.

Inasemekana January Makamba kaunda tume ya Wataalam wa kuchunguza athari zinazoweza kutokea iwapo Mradi huo Utajengwa.

Inadaiwa Sababu alizozitoa Kwa jicho la kitaalam ni kwamba wanatumiwa na Watu wasiopenda Mradi huu Ujengwe.

Leo katika uzinduzi wa Daraja la Mfugale, rais Magufuli amesikika akilalamikia wataalam ambao walifanya utafiti huo wa mradi wa umeme na akasema atashangaa hao wataalam wakiendelea kukaa ofisini. Amewatuhumu kwamba wanatumiwa ili Watanzania wanyonge wasitumie umeme wa bei rahisi waendelee kutumia umeme wa mafuata ambayo ni ghari.

Amedai wataalam wa mazingira walikuja na sababu za hovyo kabisa kwamba kila mtu atazishangaa. Kwamba mtu anatakiwa akajisaidie KM 20 kutoka kwenye mradi, Udongo utakaotumika unatakiwa uwe unapimwa, Gari ikiharibika haitakiwi itengenezewe kwenye mradi, mchicha kutoka maneo yale hautakiwi kwamba vitaharibu uoto wa asili.

Kadai maji yale yanatoka huko Mbeya na vinyesi na wanyama wamefia humo. Akashangaa hao wataalam ambao sio wazalendo wanatoka wapi?.

Rais kasema Mradi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station lazima ujengwe.
View attachment 879376
STIEGLER’S gorge inapatikana katika hifadhi ya Selous (SGR) yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 ambayo ilipitishwa kuwa moja ya Sehemu yenye URITHI WA DUNIA mwaka 1982. Katika moja ya tafiti zilizofanyika huko nyuma miaka ya 1960s na baadae miaka ya 1980s ulitanabaisha uwezekano wa kujengwa bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme 2100MW kwa kutumia Maji kutoka katika bonde la mto Rufiji.

Baadae umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali yahusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira, zilifanya utafiti wa kubaini kama kuna athari zozote za kiokolojia na za kimazingira zingeweza kutokea iwapo mradi huo wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye takribani kilometa za mraba 12,000 utatekelezwa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.

JE, MADHARA HAYO NI YAPI YATAKAYOTOKANA NA UJENZI WA MRADI HUO?

Madhara nitayaeleza kwa kifupi kama yalivyoelezwa katika Ripoti ya WWF kama ifuatavyo;

1) Ikolojia katika hifadhi ya Selous na bonde la mto Rufiji utaathiriwa. Zaidi ya viumbe hai 200,000 watakuwa kwenye hatari.

2) Shughuli za kijamii na kiuchumi zitaathiriwa sana hasa maeneo ya Mkondo wa chini(downstream) wa bonde hilo la mto Rufiji. Mmomonyoko wa ardhi, ukosefu wa rutuba na hatari ya kuzorota kwa bandari kwa sababu zile sediments(masalia) yote ambayo yalitakiwa kufika kwenye downstream yatabakia kwenye hilo Bwawa kubwa litakalojengwa.


3) Ujangili kuongezeka maradufu zaidi ilivyo sasa katika hifadhi ya Selous, ambayo itaiweka hifadhi hiyo katika hali mbaya mnoo. Mpaka sasa hifadhi hiyo iliyo na hadhi ya URITHI WA DUNIA imetajwa kuwa katika moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na ujangili. Hivyo serikali iliweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo, lakini ujuo wa hili bwawa utakizana na jitiahada hizo za kuirudisha Hifadhi ya Selous kurudi katika ubora wake.

Pia katika Ripoti ya 2017 iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uasilia la WWF(World Wide Fund for Nature), baada ya kufanya utafiti wao walipendekeza mradi huo usitishwe kutoka na madhara yatakayo tokea baadae.

Bwana la umeme linatarajiwa kujengwa lina ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama tofauti.

Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, limesema kuwa linaitaka serikali kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo hilo ili kuhakikisha madhara yote yanabainika kabla ya mipango yoyote ya mradi huo kuanza.

JE, HAKUNA MBADALA WA KUZALISHA 2100MW ILI KUIOKOA HIFADHI HIYO?

Nchi yetu imejaaliwa nishati nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kupata Megawati 2100 na zaidi.

1)Tunaweza kuzalisha umeme wa maji kutoka bonde la Mto Rufiji mbali na bwawa la stiegler’s gorge

2) Tuna gesi ya kutosha, na uzuri pia kuna miradi ambayo ipo kwenye PSMP(mpango wa kuongeza umeme katika gridi ya taifa) shida ni kuwa tunataka vya haraka haraka haraka ambavyo vitatugharimu hapo baadae. Tatizo gesi sio tegemeo tena kwa upande mwingine.Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums

3) Kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Geothermal katika bonde la Rift valley, kwa kuwa wenzetu Kenya ambao wamepitiwa bonde hilo wanafurahia uwepo wa geothermal kwao.

4) Tuna Makaa ya mawe tunaweza kutumia kuzalisha umeme.

5) Pia kuna utafiti uliofanyika unaeleza kuwa tuna uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia Upepo katika mikoa ya katikati ya TZ (singida, Dodoma)

MAAMUZI YA KISIASA

Mwaka Jana, Juni 2017 Rais Magufuli alitoa kauli ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bwawa hilo la STIEGLER’S GORGE na kupuuza tafiti zilizofanywa zinazoonesha athari za kimazingira za mradi huo. Badala ya kutumia nishati mbadala zilizopo.

Lakini kupitia taasisi zetu za ndani yaani RUBADA(Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji) na NEMC wote wametoa baraka zao za mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la STIEGLER’S gorge kwa ajili ya uzalishaji umeme uendelee.

Faida ya Stiegler’s Gorge ni nishati ya umeme. Kama ambavyo Rais Dk. John Magufuli amekuwa na shauku ya kutengeneza bwawa la maji kwenye bonde hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 ikitumia zaidi ya Dola 2 bilioni (zaidi ya TSh4.5 trilioni)

Kusudio hilo si geni, bali ni mwendelezo wa kutimiza dhamira ambayo aliiweka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, takribani miongo minne iliyopita. Mwali Nyerere alikuwa na wazo la kujenga bwawa la umeme katika eneo hilo ili kusaidia nchi kupata umeme wa kutosha.

Kwa udadisi wa juu juu uliofanywa unaonyesha kuwa, chimbuko la wazo la kuwa na mradi wa Stiegler’s Gorge lilipata nguvu zaidi mwaka 1975, wakati Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alipoyapambanua mawazo yake juu ya umuhimu ya kuwa na mradi mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme katika bonde hilo.

Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huo ulipata vikwazo vingi, hususan vya uharibifu wa mazingira, ambavyo viliibuka kila panapokaribia utekelezaji wa mradi huo, tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza mpaka hivi sasa Rais Dk. Magufuli ameazimia kuutekeleza.

umeme unaozalishwa na TANESCO kwa sasa ni takribani megawati 1517.47 huku matumizi yakiwa ni takribani ni megawati 900.

Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous - JamiiForums

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge - JamiiForums
Tangu lini hao wazungu wakapenda tuendelee?
 
Wewe utakuwa mzungu mweusi. Yaani wazungu waandae ripoti ya kukuinua wewe mweusi? Alafu ulivyo wa ajabu huelewi kama walikutawala na bado wanavutiwa kuendelea kukutawala kupitia viripoti vyao hivi vya kizandika, poor ideology!
 
Jamani nani mwenye historia ya huu miradi na kwa nini Nyerere aliuacha???

Ukitaka kutawala nchi yoyote kiuchumi hakikisha haina nishati ya kutosha. Wazungu walimfanyia mizengwe Nyerere kwa propapganda kuwa umeme ambao ungezalishwa kwa wakati huo ulikuwa mwingi sana kuliko mahitaji!. Sasa hivi wanakuja na ngonjera za 'utunzaji mazingira'. Lakini wakati wakati Wamarekani wanataka kuchimba maeoneo ya Selou waliwalazimisha UNESCO kusema hakuna madhara ya mazingira.
 
KWANINI WAZUNGU WAKATI WANTAKA URANIUMU MATAIFA YALIKUBALI ENEO KUMEGWA LAKINI KWENYE SISI KUZALISHA UMEME IMEKUWA SHIDA
Ila Bongo bhana mtasema mzungu kawahujumu wakati ndio hao hao mnawafuata kuwaomba pesa za kujenga hilo bwawa!! Bila kusahau hata hiyo teknolojia na mitambo mtanunua kwao

Alafi hakuna correlation kati ya madini na umeme.... Uranium is uranium maana inapatikana hapo tu ila umeme una alternative mfano gesi,upepo ambao unaweza zalishwa pengine kokote pale bila kuvamia mbuga ya wanyama

Hata hyo uranium ingekuwa kwenye hifadhi lazima watu wangepiga kelele..... Mie naunga mkono maendeleo ila tusipende kulaumu wazungu kila kitu maana hyo mikataba ya makubaliano ya kulinda ekolojia tulisaini wenyewe bila kulazimishwa na mtu
 
Back
Top Bottom