Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Hata mie nilishangaa sana pale nilipoambiwa siruhusiwi kumuua nyoka, siruhusiwi kumwaga diseli kidogo kwenye udongo pale gereji na eti siruhusiwi kukata mti unaotaka kuharibu nyumba yangu mpaka niombe ruhusa...lakini ukweli environmental impact assessment inaenda mbali zaidi ya tulivyozoea mtaani
point
 
Hii ni mission impossible its all bout UNESCO sio January wala jiwe hapo....
 
Mradi utajengwa inyeshe mvua liwake jua
Kumega asilimia tano ya hifadhi kwa ajili ya watanzania milioni 55 hakuna ubaya
 
Jamani , tuliambiwa tutatumia umeme wa gesi ya m
Mtwara, tena tukaaminishwa utakuwa was bei rahisi Sana.
Imekuja kuwaje Tena. ??
Kwani gesi imeisha tunarudi kwenye maji Tena ????
 
Huyo jamaa akishaamua hakuna wa kupinga ajenge tu hiyo sitigilaz goji maana si anafungu lake hapo la 50%?
Ni mjanja sana ukimsikiliza unaweza kudhani anajali wananchi lakini uko pale pale, viongozi wa kiafrika ni mafisadi, hiyo miradi na mikopo wanayochukua ni kwa ajili ya manufaa yao, as long as mikopo italipwa na wananchi kwa kodi na rasilimali zao wao hawana habari.
Hiyo miradi yote wamejipigia 20% 10% na wanaendelea. Ndio maana anaoanna yeye angalau apatiemo hako ka stigler's huku wanyonge wakichekelea kuwa anawasaidia.
 
Ni mjanja sana ukimsikiliza unaweza kudhani anajali wananchi lakini uko pale pale, viongozi wa kiafrika ni mafisadi, hiyo miradi na mikopo wanayochukua ni kwa ajili ya manufaa yao, as long as mikopo italipwa na wananchi kwa kodi na rasilimali zao wao hawana habari.
Hiyo miradi yote wamejipigia 20% 10% na wanaendelea. Ndio maana anaoanna yeye angalau apatiemo hako ka stigler's huku wanyonge wakichekelea kuwa anawasaidia.
Kabisa Mkuu miradi yote hiyo wanaishupalia kwa ajili ya manufaa yao ya kupiga ma 50%,huyu jamaa hapigi 10% ni 50% sasa we angalia dirimulaina bei halisi ni below 98m terrible teen lakini sie tumepigwa usd 200m,check MV dar-es-salaam tumenunua bil 8 halafu bovu wakati bakhresa kanunua ya kisasa latest nzuri kuliko MV dsm kwa bilioni 4.
 
Kabisa Mkuu miradi yote hiyo wanaishupalia kwa ajili ya manufaa yao ya kupiga ma 50%,huyu jamaa hapigi 10% ni 50% sasa we angalia dirimulaina bei halisi ni below 98m terrible teen lakini sie tumepigwa usd 200m,check MV dar-es-salaam tumenunua bil 8 halafu bovu wakati bakhresa kanunua ya kisasa latest nzuri kuliko MV dsm kwa bilioni 4.
Viongozi wa kiafrika ni shida na hizo Stigieler's ni hivyo hivyo, cha juu ndicho anaangalia mambo ya mazingiea mtajuana wenyewe
 
Kuna kitu jiwe hakisemi au anapotosha:
1. Kuna ukataji wa miti karibia ukubwa wa jiji la dar. Dar ina sq Km 1393, sasa hapo ni miti inakatwa ukubwa huo bila uoga. Kama mnakata miti hiyo je sisi wanainchi ndo tutaiacha.

2. Jana kwenye habari ITV maji ya mto wami yamepungua sana mpaka mto sehemu kubwa imebakia ni mchanga vipi mamba, viboko na wanyawa wategemeao maji kuishi. Hamjalifikiria hili

3. Maji yanapopungua kuna magonjwa yanayosababishwa na uhaba wa maji eg anthrax

4. Kama kuna mamlaka ya maji basi inabidi watumie dawa nyingi kutibu maji nayo ni hasara kwasabu itatubidi tulipe zaidi kufidia

5. Kuna swala la mmomonyoko

6. Kuna swala la uharibifu mazingira eg. kuna watu zaidi ya 3000 kuishi kule porini hilo nalo ni janga.

7. Kuna mengi nashauri tuachana na mpango huo
Mradi haujaanza . Maji yamepungua kwa sababu gani? Je lile wazo tu la kujenga limesababisha na kuwa kama wazo limepunguza maji ina maana yataisha kanisa ukijengwa? Mmomonyoko wa ardhi kwa vipi? Na idadi ya watu3000 sawa je ni lini tutaanza miradi mikubwa isiyoathiri mazingira?
 
before hamjafanikiwa angalieni kwanza impact za hilo swala
kumbuka SIYO wewe unayehitaji kuishi hata samaki na viumbe wa ardhin nao wanastahiki ya kuishi.
pia naomba niongeze SIKU zote msipende kuchanganya siasa na taaluma.
sipingi ujenz wa mradi hapana lakini.je ujenz huo utaweza kwenda sawia na ecology+,mfumo wa bonde la pale?????
SITAKI yajitokeze ya kihansi
Hii ndio bora mtoto wa kenge apone ila mtoto wa binadamu afe kwa kisingizio cha mazingira. Kuna nchi itaendelea bila kuharibu mazingira?
 
Hata suala la Tanzania ya viwanda ni vita ya kibepari.. Mabepari hawawezi kukubali ufanye Jambo litakalovuruga maslahi Yao.

Inawezekana kuna Athari za kimazingira, ni vyema tukajiandaa kufanya restorations na sio kuogopa kufanya mradi kabisa.

Namuunga mkono Mr. President kwenye hili.
 
Viongozi wa kiafrika ni shida na hizo Stigieler's ni hivyo hivyo, cha juu ndicho anaangalia mambo ya mazingiea mtajuana wenyewe
Hawa jamaa wanauzi sana wanatapakanya fedha wakati wananchi miundombinu mibovu,sehemu nyingi DSM hazina umeme vipi kuhusu NAMINYWILI huko? Vipi KUHUSU NYAMISATI NA NAMTUMBO? VIPI KUHUSU NANJILINJI NA NAMAPANYA? VIPI KUHUS NANGURUWE HALI ZAO Zipoje ikiwa DSM barabara MBOVU? Mistigilaz na midirimulaina ni WIZI na UFISADI tu wa 50% kupigwa tu.
 
Naunga mkono mradi ujengwe, hili la wazungu kutufanyia utafiti sikubaliani nalo maana sisi hatujaenda kuwafanyia utafiti kwao.

Ifike mahali kama hatuwaombi pesa ya kujenga hilo bwawa tuwe huru kujiamulia mambo yetu.

Kwenye historia tulisoma mambo ya akina Karl Peters, hawa watu bado wanaishi. Hawa watu kama ilivyokuwa kwa akina Mkwawa, sasa hivi saizi yao ni Magufuli
Una uhakika hiyo pesa ni ya ndani ? subiri uishe itakuwa yaleyale ya gesi ya mtwara
 
Magufuli namkubali sana kwenye utendaji. Jamaa ana maono makubwa sana na ya kimaendeleo kwa taifa hili. Tatizo lake moja tu, hana washauri wazuri. Wengi waliomzunguka kazi kujipendekeza tu. Rais anapiga kazi peke ake, anabuni miradi ya maendeleo peke yake. Watendaji wake wa chini hakuna wanachokifanya zaidi ya kumsifia tu. Angepata watu wabunifu, wachapa kazi kama yeye hii nchi ingepaa kiuchumi kwa muda mdupi sana.
Wachapakazi wote amewaita mafisadi
 
Watamfustruste wee.Akija kutahamaki 2025 hii hapa.Wazungu bwana.Watamzibia mapenyo ya mikopo ya kimataifa.Labda awape wachina.
 
Heshima kwenu wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, huenda akatumbuliwa kutokana na kuwa kikwazo katika Ujenzi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station.

Inasemekana January Makamba kaunda tume ya Wataalam wa kuchunguza athari zinazoweza kutokea iwapo Mradi huo Utajengwa.

Inadaiwa Sababu alizozitoa Kwa jicho la kitaalam ni kwamba wanatumiwa na Watu wasiopenda Mradi huu Ujengwe.

Leo katika uzinduzi wa Daraja la Mfugale, rais Magufuli amesikika akilalamikia wataalam ambao walifanya utafiti huo wa mradi wa umeme na akasema atashangaa hao wataalam wakiendelea kukaa ofisini. Amewatuhumu kwamba wanatumiwa ili Watanzania wanyonge wasitumie umeme wa bei rahisi waendelee kutumia umeme wa mafuata ambayo ni ghari.

Amedai wataalam wa mazingira walikuja na sababu za hovyo kabisa kwamba kila mtu atazishangaa. Kwamba mtu anatakiwa akajisaidie KM 10 kutoka kwenye mradi, Udongo utakaotumika unatakiwa uwe unapimwa, Gari ikiharibika haitakiwi itengenezewe kwenye mradi, mchicha kutoka maneo yale hautakiwi kwamba vitaharibu uoto wa asili.

Kadai maji yale yanatoka huko Mbeya na vinyesi na wanyama wamefia humo. Akashangaa hao wataalam ambao sio wazalendo wanatoka wapi?.

Rais kasema Mradi wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station lazima ujengwe.
View attachment 879376
STIEGLER’S gorge inapatikana katika hifadhi ya Selous (SGR) yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 ambayo ilipitishwa kuwa moja ya Sehemu yenye URITHI WA DUNIA mwaka 1982. Katika moja ya tafiti zilizofanyika huko nyuma miaka ya 1960s na baadae miaka ya 1980s ulitanabaisha uwezekano wa kujengwa bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme 2100MW kwa kutumia Maji kutoka katika bonde la mto Rufiji.

Baadae umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali yahusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira, zilifanya utafiti wa kubaini kama kuna athari zozote za kiokolojia na za kimazingira zingeweza kutokea iwapo mradi huo wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye takribani kilometa za mraba 12,000 utatekelezwa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake ya IUCN(Shirika la uhifadhi wa uasilia) na UNESCO zilipendekeza kusitishwa kwa mradi huo baada ya kubaini madhara makubwa kwa wanyama na binadamu waishio katika bonde hilo la mto Rufiji.

JE, MADHARA HAYO NI YAPI YATAKAYOTOKANA NA UJENZI WA MRADI HUO?

Madhara nitayaeleza kwa kifupi kama yalivyoelezwa katika Ripoti ya WWF kama ifuatavyo;

1) Ikolojia katika hifadhi ya Selous na bonde la mto Rufiji utaathiriwa. Zaidi ya viumbe hai 200,000 watakuwa kwenye hatari.

2) Shughuli za kijamii na kiuchumi zitaathiriwa sana hasa maeneo ya Mkondo wa chini(downstream) wa bonde hilo la mto Rufiji. Mmomonyoko wa ardhi, ukosefu wa rutuba na hatari ya kuzorota kwa bandari kwa sababu zile sediments(masalia) yote ambayo yalitakiwa kufika kwenye downstream yatabakia kwenye hilo Bwawa kubwa litakalojengwa.


3) Ujangili kuongezeka maradufu zaidi ilivyo sasa katika hifadhi ya Selous, ambayo itaiweka hifadhi hiyo katika hali mbaya mnoo. Mpaka sasa hifadhi hiyo iliyo na hadhi ya URITHI WA DUNIA imetajwa kuwa katika moja ya maeneo yaliyo kwenye hatari kutokana na ujangili. Hivyo serikali iliweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo, lakini ujuo wa hili bwawa utakizana na jitiahada hizo za kuirudisha Hifadhi ya Selous kurudi katika ubora wake.

Pia katika Ripoti ya 2017 iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Uasilia la WWF(World Wide Fund for Nature), baada ya kufanya utafiti wao walipendekeza mradi huo usitishwe kutoka na madhara yatakayo tokea baadae.

Bwana la umeme linatarajiwa kujengwa lina ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama tofauti.

Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, limesema kuwa linaitaka serikali kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo hilo ili kuhakikisha madhara yote yanabainika kabla ya mipango yoyote ya mradi huo kuanza.

JE, HAKUNA MBADALA WA KUZALISHA 2100MW ILI KUIOKOA HIFADHI HIYO?

Nchi yetu imejaaliwa nishati nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kupata Megawati 2100 na zaidi.

1)Tunaweza kuzalisha umeme wa maji kutoka bonde la Mto Rufiji mbali na bwawa la stiegler’s gorge

2) Tuna gesi ya kutosha, na uzuri pia kuna miradi ambayo ipo kwenye PSMP(mpango wa kuongeza umeme katika gridi ya taifa) shida ni kuwa tunataka vya haraka haraka haraka ambavyo vitatugharimu hapo baadae. Tatizo gesi sio tegemeo tena kwa upande mwingine.Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums

3) Kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Geothermal katika bonde la Rift valley, kwa kuwa wenzetu Kenya ambao wamepitiwa bonde hilo wanafurahia uwepo wa geothermal kwao.

4) Tuna Makaa ya mawe tunaweza kutumia kuzalisha umeme.

5) Pia kuna utafiti uliofanyika unaeleza kuwa tuna uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia Upepo katika mikoa ya katikati ya TZ (singida, Dodoma)

MAAMUZI YA KISIASA

Mwaka Jana, Juni 2017 Rais Magufuli alitoa kauli ya kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bwawa hilo la STIEGLER’S GORGE na kupuuza tafiti zilizofanywa zinazoonesha athari za kimazingira za mradi huo. Badala ya kutumia nishati mbadala zilizopo.

Lakini kupitia taasisi zetu za ndani yaani RUBADA(Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji) na NEMC wote wametoa baraka zao za mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la STIEGLER’S gorge kwa ajili ya uzalishaji umeme uendelee.

Faida ya Stiegler’s Gorge ni nishati ya umeme. Kama ambavyo Rais Dk. John Magufuli amekuwa na shauku ya kutengeneza bwawa la maji kwenye bonde hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 ikitumia zaidi ya Dola 2 bilioni (zaidi ya TSh4.5 trilioni)

Kusudio hilo si geni, bali ni mwendelezo wa kutimiza dhamira ambayo aliiweka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, takribani miongo minne iliyopita. Mwali Nyerere alikuwa na wazo la kujenga bwawa la umeme katika eneo hilo ili kusaidia nchi kupata umeme wa kutosha.

Kwa udadisi wa juu juu uliofanywa unaonyesha kuwa, chimbuko la wazo la kuwa na mradi wa Stiegler’s Gorge lilipata nguvu zaidi mwaka 1975, wakati Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alipoyapambanua mawazo yake juu ya umuhimu ya kuwa na mradi mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme katika bonde hilo.

Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huo ulipata vikwazo vingi, hususan vya uharibifu wa mazingira, ambavyo viliibuka kila panapokaribia utekelezaji wa mradi huo, tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza mpaka hivi sasa Rais Dk. Magufuli ameazimia kuutekeleza.

umeme unaozalishwa na TANESCO kwa sasa ni takribani megawati 1517.47 huku matumizi yakiwa ni takribani ni megawati 900.

Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous - JamiiForums

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge - JamiiForums
https://www.jamiiforums.com/threads...ha-mradi-wa-umeme-wa-stieglers-gorge.1443916/
Kwetu wanataka kuhifadhi wanyama kwao wamejenga majiji, hata hatujui wanyama wa asili wa kwao, kwao binadamu first, kwetu mnyama first, Magufuli songa mbele hayo mambo ya wanyama baadae.
 
Uyu January alikuwa anatafutwa ila naona yeye hajui;kuna visa kafanya hapo nyuma kwamfano mvutano wa wapi ijengwe ofisi ya halmashauri Bumbuli,sakata la vibari vya mazingira kiwanda cha betri Kibaha na sasa Rufiji.Namamshauri ajiuzuru mwenyewe bila shuruti.
Akijiuzulu wasiojulikana wanae
 
Back
Top Bottom