Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Ni maigizo yanaendelea. Mafisadi wengine "kuhukumiwa" ni mwaka 2020.
 
Mwisho tutasikia wameanza kupewa fedha za kujikimu,dah hii nchi ya kikuda sana.
 
Ushauri gani sasa au namna ya kupiga pesa kimya kimya?
 
Safi sana. Ni ujinga kumtumia watu wazoefu kama hawa kufagia wakati wanaweza kuchangia vingine...
basi tuwatoe magerezani wazoefu wote wabaki.. wabaki wasio na uzoefu ndio wawe wanafungwa humo magerezani
 
Hahahah eti mahakama ya mafisadi, hukumu ni umehukumiwa na Mahakama kwa kifungu namba ziro ziro mkwaju,kumi kumi mkwaju Ukafanye kazi ya Consultancy Kooooooot!

Tunataniana aiseee!
 
Dah... its only happening in Bongo.... Jamani hawa si ni wezi wakubwa na hatari now wanapewa kushika mafile ya wagonjwa? au ni mtego maana mwizi ni mwizi tu na haachi... tutasikia wamekwapua kitu hapo...
 
Hapo kufagia hakupo tena watakuwa washauri na watalipwa maskini Tanzania
 
Kama wana kosa la matumizi mabaya ya ofisi watatoaje ushauri kwenye ofisi za watu. Kama mnawaamini si muwaachie huru. Nchi hii cjui imerogwa na nani.

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ambao wanatumikia kifungo cha nje pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam, wamepewa kazi nyingine ya kusaidia kuongeza ufanisi ofisini. Mawaziri hao wa zamani sasa wamepangiwa kazi ya kutoa ushauri elekezi wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na masuala ya bajeti. View attachment 324057

Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi - Dar24
 
Kwa hali hii sitashangaa Mahakama ya mafisadi itakuja na gereza lake litakuwa na Wi-Fi swimming pool na sehemu za kufanyia michezo mbali mbali na mzoezi bar kiwanja cha ndege massage room na vitu vyote na litajengwa karibu na ufukwe wa bahari
kama lile gereza la Escobar kule Colombia
 
Back
Top Bottom