Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Kwa hali hii sitashangaa Mahakama ya mafisadi itakuja na gereza lake litakuwa na Wi-Fi swimming pool na sehemu za kufanyia michezo mbali mbali na mzoezi bar kiwanja cha ndege massage room na vitu vyote na litajengwa karibu na ufukwe wa bahari
Narcos
 
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ambao wanatumikia kifungo cha nje pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam, wamepewa kazi nyingine ya kusaidia kuongeza ufanisi ofisini. Mawaziri hao wa zamani sasa wamepangiwa kazi ya kutoa ushauri elekezi wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na masuala ya bajeti. View attachment 324057

Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi - Dar24
sasa hii adhabu imeongezwa na mahakama au uongozi wa hospitali una mamlaka hayo ? hii nchi inatia aibu sasa .
 
Hahahahaha!

Hii nchi bana! Naona Mkapa sasa anaendesha nchi kupitia kijana wake Magufuli!

Sasa hawa wezi wamegeuka ma consultants...?
Mambo yasiyowezekana duniani kote Tanzania yanawezekana.
 
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ambao wanatumikia kifungo cha nje pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam, wamepewa kazi nyingine ya kusaidia kuongeza ufanisi ofisini. Mawaziri hao wa zamani sasa wamepangiwa kazi ya kutoa ushauri elekezi wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na masuala ya bajeti. View attachment 324057

Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi - Dar24
Hiyo nayo adhabu???
 
Kweli hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu aiseeee[emoji15] [emoji15]
 
utasikia wiki ijayo wamepewa kazi nyingine ya kuwa mabalozi nchi za nje.
 
[emoji15] [emoji15] that's magumashi[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Safi sana. Ni ujinga kumtumia watu wazoefu kama hawa kufagia wakati wanaweza kuchangia vingine...
Ni kweli,wana uzoefu wa kuitia serikali mabilioni ya pesa,uzoefu wa kuwadhihaki masikini,watanzania watakula majani lkn ndege tutanunua
 
Back
Top Bottom