Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Mkapa alitoa mapendekezo ya kuachiwa watu hawa alipomtembelea Magufuli ikulu mwezi January, alijua anasimamia nini, anajua anasimamia nini na anajua atasimamia nini! Zao la Magufuli ni mpambano kati ya Kikwete na Mkapa!!
ila nikweli...jpm na jk naona kama haziivi hivi! siku ile ya kuongea na wazee wa dar nilisikilza kwa makini speech ya jpm...kuna sehemu aliwataja mwinyi...kikwete...lakini kwa mkapa akasema ...MZEE MKAPA sasa nikawa najiuliza nani mzee kati ya mwinyi na mkapa....hapa kuna jambo
 
Wote tunafahamu, mfungwa anapokua gerezani hufanya kazi za mikono kama kilimo nk; hawa jamaa mara baada ya kuhukumiwa walikua nao wanaenda site kama wafungwa wengine? Nauliza hivyo kwasababu kama kumbukumbu zangu zitakua vizuri, kabla hawa jamaa hawajakamatwa tuliona pirika pirika za usafishwaji wa gereza la KEKO na magari mapya ya wafungwa kununuliwa then hawa jamaa ndipo wakakamatwa, hope walikua na vymba vyao special na hata TV sitashangaa nikisikia kua walikua wanaangalia. Hongera Mkapa kuchezesha karata zako vizuri
 
hawa wana uelewa mkubwa sana kwenye matumizi ya madaraka na ofisi!! ndio maana wako pale. wacha wawashauri....
 
Usiogope kaka sema kwa sauti kubwa mijizi izomewe mijizi hii Yona ndio mshirika mkubwa wa mkapa kujimilikisha mgodi wa kiwira halafu MTU itakuwa na nguvu ya kupambana na mafisadi

Inauma sana ukiangalia jinsi nchi hii kuna wanaojiona ni binadamu zaidi ya wengine. Nachelea pia kwamba vita ya ufisadi mkubwa haitaweza kufanikiwa watakaoumizwa ni vifisadi vidogo. Wezi wa Kiwira na waliochukua mapesa ya EPA na Escrow (achilia waliopiga cha juu kwenye rada na ndege ya rais) hawatokaa waguswe... ama kweli CCM ni ile ile.
 
Tukisema hana ubavu wa kuwahukumu mafisadi kweli povu linawatoka,uwezo wake kucheza na watoto wa chekechea akitia mguu hata kwa vijana wangu wa shule ya msingi atakalishwa kwa hiyo sahau kabisa wenye degree zao kama joka la makengeza
 
...ile adhabu ya kufagia ilionekana inawadhalilisha hawa wazee,watu wanawashangaa mwanzo mwisho.Hivyo basi,wakaona wawatafutie "kiji adhabu" kingine kiwasukume wakati wanaendelea kutafutiwa mlango wa kutokea.!
 
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ambao wanatumikia kifungo cha nje pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam, wamepewa kazi nyingine ya kusaidia kuongeza ufanisi ofisini. Mawaziri hao wa zamani sasa wamepangiwa kazi ya kutoa ushauri elekezi wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na masuala ya bajeti. View attachment 324057

Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi - Dar24
you cant be serious..let me find the truth
 
Subirini kama hamjasikia wamepiga mihela ya hospitali
Ukishakuwa mwizi huwezi kuacha
 
Na hayo ni machache wanayojibana bana kutueleza.....ila inaonyesha yapo mengi manono kwa mabwana hawa ila raia hatuna haki ya kujuzwa.
Wasiogope wawatoe kabisa tu na kuwapa uwaziri, sisi wa Tz hatuna neno tutalalamika kichini chini siku mbili tatu tu kisha tutasahau.
 
Daah lumumba wote wamekula kona, siwaoni hapa
 
Sasa si bora hizo kazi wapewe vijana grduates wajitolee wapate experience.
 
Topic kama hiz ...lumumba huwaoni kabisa wanapitatu...ila kijarida cha ulaya kitaje jina la rais makufuli kina pwaani kwetu,ikungi,singida dodoma, utaifa kwanza ,na lizaboni, utakuta tayar washaandika ,makufuli sasa zaid ya Obama ,marekani kujifunza kwa makufuli ....utadhani wamekatwa vichwa ....
 
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ambao wanatumikia kifungo cha nje pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam, wamepewa kazi nyingine ya kusaidia kuongeza ufanisi ofisini. Mawaziri hao wa zamani sasa wamepangiwa kazi ya kutoa ushauri elekezi wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na masuala ya bajeti. View attachment 324057

Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi - Dar24
Ushauri gani wa kiutendaji wakati walifungwa kwa kushindwa kuwajibika ktk hizo hizo ofisi za serikali?
 
Hahahahaha!

Hii nchi bana! Naona Mkapa sasa anaendesha nchi kupitia kijana wake Magufuli!

Sasa hawa wezi wamegeuka ma consultants...?
Mkuu si ulimsikia akisema kuwa yupo tayari kumsaidia magu wakati wowote?ndio tayari yupo kazini kimasafa
 
Back
Top Bottom