Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Mramba na Yona waongezewa adhabu. Sasa wapewa kazi za ofisini!

Kweli? Pamoja na "mbwembwe" zote za kupewa vifaa vya kufanyia usafi? Hii ni haki? hebu wanasheria watujuze....
 
Haina tofauti na kamishana wa TRA kubebe ndoo akiwa wanatoka mahamani na wenzie
 
Waacheni wazee wa watu, mnaacha kumshupalia Jecha na nkurunzinza wetu mnahangaika na mambo ya usafi
 
Jei chaaa na "Nkurunziza" na haya "maigizo" mengine yote mamoja! Suluhisho hapa ni Katiba iwe WAZI! Mfumo wa utumishi, utumikaji, mienendo ya makosa ya jinai na adhabu, uchaguzi, mwenendo wa utumishi wa Wabunge na yote...uwe WAZi kwenye katiba.
 
Wana jamvi wa JF, hasa mlioko Dar es Salaam, napenda kujua kama Mawaziri wa Zamani ndugu Yona na Ndugu Mramba WANAENDELEA na "adhabu" ya kufanya usafipale Hospitali ya Palestina, Sinza. Iliripotiwa kwa nguvu nyingi SANA adhabu ilipoanza. Kwa sasa KIMYA! Ama siyo habari tena?
mjomba mengine tumwachie Mungu tu , kwa kweli inachekesha sana .
 
Watanzania katiba ya ccm haitufikishi kokote hata Obama akipewa Urais wa Tanzania Kwa Katiba ya CCM in bure
 
Ujuha tumeanza siku nyingi, china adhabu tamu kwa wezi ni tuuuuuu, sisi adhabu ni maigizo.
Nani aliwaruhusu waende na ndoo? Waliambiwa na nani kuwa mahabusu hakuna ndoo ?
 
I wish wafungwa wote wangekuwa wanapata the same treatment. Halafu ndo sasa hivi tunalagaiwa na mahakama ya mafisadi! Watapewa fast track kama hawa. Vifungo virefu vya gerezani si kwa mafisadi bali malofa.
Hata mie ndicho nnachoona! Kwa nini kuwe na MATABAKA? Mwizi ni mwizi tu.. Mwizi wa viazi soko la Sombetini anakuwa na adhabu tofauti na MWIZI wa mabilioni ya Shilingi Benki Kuu!
 
Kwa hali hii sitashangaa Mahakama ya mafisadi itakuja na gereza lake litakuwa na Wi-Fi swimming pool na sehemu za kufanyia michezo mbali mbali na mzoezi bar kiwanja cha ndege massage room na vitu vyote na litajengwa karibu na ufukwe wa bahari
...Mahakama hiyo huenda ikajengwa Kilindoni, Mafia ama Mbegani, Bwagamoyo.
 
Kwa hali hii sitashangaa Mahakama ya mafisadi itakuja na gereza lake litakuwa na Wi-Fi swimming pool na sehemu za kufanyia michezo mbali mbali na mzoezi bar kiwanja cha ndege massage room na vitu vyote na litajengwa karibu na ufukwe wa bahari
umesahau na memory card
 
Back
Top Bottom