Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Bufa

Nikujibu hilo la elution, machinery, kemikali na maabara kwa pamoja, with respect to Chunya.

Elution kwa sasa bado ni chache (ukilinganisha na idadi ya Leaching plants ambazo ndio feeder facilities za Elution), na bado ni uwekezaji wenye tija. Lakini ni uwekezaji unaohitaji capital kubwa, na risks (kwa maoni yangu) ni chache.

Machinery na Chemicals hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa pamoja. Na kwa maoni yangu ningependekeza uanze na hii (ikikupendeza).

Maabara:
Hizi zipo chache, na mahitaji ya uchimbaji ambao ni based on informed facts (kujua kwenye sampuli kuna dhahabu kiasi gani kabla ya kufanya maamuzi) unazidi kuongezeka.
Hapa napo ni mahala pa zuri kuwekeza.

NB: Majibu yangu ni ya jumla sana, nimeacha "mashimo mengi" ya wenzangu kukosoa, kurekebisha, kuboresha n.k ili kukupatia ushauri bora na utakaokufaa wewe na wengine watakopitia uzi huu.
 
vijana tusibaki kulalamika kwa kuilaumu serikali kushindwa kutuajiri, bali tuziibue fursa


- Kote umeelezea vizuri, kwenye hicho kipengele tu ndiyo umeharibu kila kitu kwa kuwaona wengine walalamishi...
 

Asante sana mkuu, nilikua sijawahi kusikia hii nitaifanyia kazi.
 

Asante sana mkuu. Nimekupata vizuri. Nitafanyia kazi, usichoke kutupa your expertise ni darasa tosha.
 
Mkuu, kwanza hongera kwa tafiti unazofanya ili ufanye informed decision. Kama ilivyokuwa kwenye biashara yoyote ile, wapo ambao mambo yanadoda na ambao mambo yanawaendea vema.
Lakini moja ya mbinu ambazo wafanyabiashara kadhaa wanatumia ni kutengeneza "chain of dependency" kwa maana ya kwamba yeye anauza kemikali, anauza machinery na ana elution. Hivyo wale anaowauzia kemikali na mitambo ndio haohao watakua ni wateja wake kwenye elution plant wakishakuza mzigo.

Elution ni uwekezaji mkubwa hivyo unahitaji tafiti ya kutosha kabla ya ku execute, napenda unavyokusanya taarifa. Wewe ni mfano wa muwekezaji smart, keep it up.

Bufa
 

The chain of dependency is the key. Asante sana mkuu for your inputs. Nashukuru sana.
 
Million 7 upo na gram 93 uko gram moja bei gani mkuu uku Mozambique gram laki
 
Mkuu, Nasikia kuna elution zimetelekezwa kwa kukosa mzigo. Hii unaongeleaje, haiwezi kuwa changamoto hasa kwa elution mpya?
hii ni changamoto haswa hasa kama ww ni mgeni wa maeneo haya,hii imesababishwa na historia ya nyuma wakati elution zinaanza kujengwa hapa chunya,wasukuma kutoka mwanza ndo waliintroduce hii technology kwa hapa chunya so walikuwa wanawaibia sana watu kwenye kufanya processing, baadae wazawa nao wakaanza kujenga zao jambo lililosababisha elution nyingi za mwanzo na hasa za wageni kukosa wateja hivyo nyingi zinefungwa na wao kurudi kwao,so kama ww ni mgeni itakuwa kazi sana kuaminiwa haraka haraka na kupata wateja jambo la msingi ni kutengeneza connection kubwa
 

Asante mkuu nitafanyia kazi.
 
Hakika wewe umetema pointi za maana na zinazoonyesha uhalisia wa biashara tofauti na wengi wetu hupenda kusikia stori za vijiweni, maake kama faida ingekuwa kubwa sana tunavyoaminishwa basi wengi wangefanya.
Kwan wanaofanya hii biashara n wachache?
 
Mkuu, wewe ni hazina

Kuna mtu nilimuuliza kuhusu hii biashara, aliruka futi 100 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu 4 kilos umezitaja kiwepesi sana.
 
nikupe hongera nyingi kwa uthubutu na moyo wa kupambana kwa kusimamia kile unachokiamini bila kujali ugumu wa njia uliyopitia.
 
Mkuu 4 kilos umezitaja kiwepesi sana.
[emoji23][emoji23][emoji23] hayo makilo tulipiga miaka 10 iliyopita kwa marudio ya kutwanga kwa kinu. Kwahaya ya sasa unatafuta hela ya kula tu siyo kujenga magorofa. Sikutaka ligi humu kusema unatoka elution na nusu kilo mpaka kilo 2 kwa hali ya sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…