Tufungueni macho nasi ni kitu gani hii
Airbnb ni unapangisha chumba/ nyumba kwa muda wowote kuanzia siku, wiki, mwezi, hadi miezi mitatu nk. Unafanya haya kupitia platform/ mtandao wa Airbnb.
NI hivi badala ya mfano wewe mwenye ku-advertise nyumba yako kupitia dalali, unaiweka kwenye website ya Airbnb unalipa pesa kidogo mpangaji anakutafuta pale mnakutana moja kwa moja hapo sokoni mpangaji anachagua ayatoka analipia unapata pesa zako chap.
Kiufupi inarahisisha sana mambo mfano una watoto saba unataka kwenda holiday au wewe na washkaji zako wanne mmeamua kwenda morogoro kwa siku tatu mnapangisha nyumba moja badala ya kuchukua hotel na vyumba tofauti. Kiufupi unapata huduma zote utakazopata nyumbani kama jiko, washing machine, na vingine.
Siyo kama hotel, lodge, hostel, guest ni kama unahamia nyumba nyingine kwa muda mchache kutoka nyumbani kwako sababu inatokana na wewe mwenyewe.
Sasa ukiondoka unaacha review, rate, marks ulipapenda, usalama, usafi, facilities nk. Na yeye mwenye nyumba anaacha review kuhusu wewe ni msafi, hukufanya fujo na kuvunjavunja TV, hukuacha, bangi na gongo kila chumba nk.
Hizo review ni ukiwa nazo nyingi positives (chanya) unaweza ku-kodi nyumba yako kwa urahisi. Zikiwa negatives. (hasi) nyingi kupata wateja itakuwa vigumu.
Vivyo hivyo kwa mpangaji na yeye kwenye profile yake kuna hasi na chanya. Kama hasi ni nyingi, kupata nyumba itakuwa vigumu sababu wenye nyumba wanangalia kwanza feedback historia yako kwanza kabla hawajakukubali. Umeelewa?
Rent from people in Dar es Salaam, Tanzania from £16/night. Find unique places to stay with local hosts in 191 countries. Belong anywhere with Airbnb.
www.airbnb.co.uk