Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Hiyo lodge ya ghorofa nane utaikodi na kuipangisha bila ukarabati?
 
Hiyo line yako ya mwisho kuna wengine wateja hawapendi pulukushani za kelele sasa ukishaanza kuuza Pombe, supu, chakula hiyo sasa inakua sio lodge hata mazingira wateja wanaweza kimbia wale wastaarabu. Alafu ukiweka hivo vitu inakua lodge ya wahuni shortime, uchafu. Labda aweke ki bar nje ya lodge huko ambapo mteja akiitaji chakula inakua sio mbali kukifata na kelele za watu/miziki haziingii lodge.

Maana kuna logde zingine zenye bar ni kelele sana likipigwa "IN DA CLUB" la 50 cent unaweza hisi umo ndani chumbani kitanda kina dance imagine mziki huo mpaka saa saba au nane usiku huko na unataka kulala.

Lodge wewe weka vitu vya kawaida pale reception kama miswaki, maji, dawa ya mswaki, vitu vile vitakavomvutia mteja maana ni wa kulala na kuondoka.

Ukianza kuweka sijui chakula, pombe, mziki e.t.c hiyo sio lodge ni bar wateja utakaopata ni wahuni na kukuharibia lodge yako.
 
Kuna lodge moja njombe niliipenda sana mm nikisafiri napenda kulala lodge wanazolala wasafiri au wafanyabiashara sio wenyeji wanaokuja kufanya ngono na ulevi lodge zenye bar mzik mnene kelele nyingi sipendi, napenda nikanywe bar ya karibu na nitakapolala, ile lodge wameweka bango kubwa juu ya paa "hauruhusiwi kuingia na mwanamke asiye mke wako, pombe,kelele,sigara haziruhusiwi" nilipapenda ni pa tulivu sana mashuka mablanket masafi sana, hata majina ya vyumba ni majina ya vitabu vya biblia na panajaa sana watu wanaopenda utulivu wapo wengi.
 
Uko sahihi
Pia ukiweza kuwekeza kwenye njia kuu....kwa kulenga malori
 
Bila shaka wewe ni mkristo ndio maana hauelewi hicho nilichokiandika na uzito wake pia, kwahiyo ni ngumu sana mimi na wewe kuelewana
 
Mkuu wale wa Malori wanalalaga lodge kweli? Naonaga kama wanapark na kulala seat za magari yao akijilngeza sana anataka guest za short time apinguze usingizi aendelee mbele
Hulala bei ya wastani ili wapate bafu....
 
Kabisa mkuu! Sio unaenda lodge watu wanapishana pishana sana kwenye korido.Mimi kiukweli lodge zenye bar kwa nje sio choice zangu kabisa.Nenda kale/kunywa kwingine ukirudi ni kulala tu.
Kuna moja nililala ifakara inaitwa clifton lodge ina vyumba vina majina ya wanyama, ukitaka kuna chef pale unaweka oda anakupikia chakula chochote kuna jiko lao zuri, safi hapo reception aiseeh yule chef ni fundi kwenye kukaangiza aiseeh😀
 

Attachments

  • images.jpeg
    59.8 KB · Views: 21
Hongera sana mkuu, uwekezaji mzuri pia nimejifunza kitu
 

Hongera kwa uwekezaji Mkuu.
Somo hili pia tumelichukua, Asante…
 
Pazuri asee gharama ni ngapi kwa usiku mmoja?
 
Sio purukushani hapo ndio watu wanafanya dili za maana. Hakuna mziki kabisa kuna utulivu sana ila kuna chakula, vinywaji.

Lodge ya viwango mswaki, dawa ya mswaki, taulo mpya, makobazi mapya yote unawekewa chumbani.

Mara nyingi nimona kuhusu breakfast, lodgers na wageni wao walipewa breakfast bure asubuhi.

Inaleta kuaminika. Ujue kitu cha kwanza wateja wako ni kina nani? Sio maskini wanahitaji mazingira rafiki kufanya kazi zao. Uaminifu, utulivu, huduma za viwango ndio wanacholipia.
 
Umesema sahihi, Mimi nilishauriwa pia niweke Vinywaji kwamaana beer.

Nilikataa as Kuna watu wakishalewa wataanza kupiga kelele bila kuangalia Kuna mtu amelala kesho alfajiri anawahi kikao/usafiri hivyo angehitaji utulivu.

Hizo huduma za miswaki/dawa n.k wanavipata kule vyumbani
 
Sure

Mimi pia huwa sipendi kelele hivyo na pale ofisini sijaweka hiyo biashara ya Vinywaji.

Vinywaji vinaenda sambamba na Muziki, hivyo itakuwa usumbufu Kwa mteja aliyeko ndani amejipumzisha
 
Tatizo huoni CCTV upande wako, weka na WIFI uwe waona au mtoe weka mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…