Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Wanaume hawaaminiki na pia uwe na mpango wa kuwabadilisha kazi mara kwa mara pale ambapo wanaonesha kutokuwa waaminifu.
Au ingia gharama nunua smart lock ambazo pw utakuwa watoa wewe
Shukrani Kwa Ushauri wako Mkuu.

Hizo Smart lock, Kuna Kampuni unajua wanazalisha? Nitafurahi kupata mawasiliano yao kama hautajali
 
Hongereni Mkuu, huko maisha ni simple kumbe.

Japo maeneo ya hivyo panakuwa na Mzunguko mdogo wa hela
Watu wa huku wakivuna viazi, maharage mbao, mahindi wanahamia njombe mjini wanasema beer za mjini ni tamu wanapiga kambi pesa zikiisha wanarudi vinyunguni kuandaa mashamba, wakati wa mavuno ya viazi huku ukienda njombe hupati Chumba lodge zote zimejaa wakulima wanaenda mjini kutanua wakenya nao wanajaa mjini kununua viazi.
 
Hahaha.........kumbe kuna hela.

Nitatafuta nafasi kuja kusavei ili kuona fursa za Kiuchumi huko, hata kuwajengea baa na kuwaletea wale wadada wa Kiilaqi kama Wahudumu wao 😜
 
Asante Mkuu

Watanzania wengi sio waaminifu

Baada ya kuichezea Camera saivi analeta hela anayojisikia maana anasema Leo wamelala wateja 7 kumbe wamelala 9

Nimetengeneza mara 3 lakini baada ya muda inaharibika Tena.

Nina hakika ningekuwa nakaa mwenyewe huenda Payback period ingeshuka hadi miaka 2

Maana nahisi napoteza Mapato mengi Kwa Wizi wao Hawa Vijana
Fukuza huyo anayechezea cameraeta watu wengine wapya ,ili kusurvive kwenye hii dunia inaitaji uwe beberu kweli kweli
 
Fukuza huyo anayechezea cameraeta watu wengine wapya ,ili kusurvive kwenye hii dunia inaitaji uwe beberu kweli kweli
Umesema sahihi Mkuu.

Huyo Dogo nilimwondoa, ajabu baada ya kuanza kazi Mhudumu mwingine eti Lodge inajaa.

Hii ina implies kuwa Mhudumu wa mwanzo alikuwa anaiba hadi anapitiliza
 
Umesema sahihi Mkuu.

Huyo Dogo nilimwondoa, ajabu baada ya kuanza kazi Mhudumu mwingine eti Lodge inajaa.

Hii ina implies kuwa Mhudumu wa mwanzo alikuwa anaiba hadi anapitiliza
Ndo mana watu wanashangaa kwa nini wahindi wanaajiriwa sana na wazungu kwenye makampuni makubwa duniani?hata C.E.O Wa makampuni yote makubwa ni wahindi simply ni kwamba wahindi ni waaminifu, wachapakazi na wasimamizi wazuri wanawaza future ya kampuni kwanza kuiba baadae na wanaiba faida sio mtaji, sasa jitu jeusi kutoka kazulamimba akipata kazi anachowaza aibe apate pesa akaonge demu iPhone macho matatu .
 
Kwa kweli hapo Kama Wabongo ndiyo tunapofeli kuwaza upigaji badala ya kazi.

Hawajui Wizi wake ukibainika unampiga Chini na kumleta mfanyakazi mwingine
 
Aweke hiden camera ya kumpa live situation, kuna maza anamiliki gest nyingi kila siku anafukuza na kubadil wafanyakazi sasa nimemwelewa
Hizo hidden camera watakuwa hawazioni Kwa uwazi kama hizo camera nilizokwisha kuzifunga?
 
)Kuna camera zinakuwa ndani ya taa au uwe ubadili wafanyakazi kila muda ndo utaona pesa, gest inachangamoto sana hasa zile za showtime ndo wanapiga sana, hakikisha unapewa hesabu ya vyumba vyote kulala kila siku izo showtime ndo atajazia
 
Nitafatilia kuhusu hizo Camera, nahisi Kuna hotel Moja nililala DSM ilikuwa na Camera za namna hiyo.
 
Kwahiyo Wanawake Wana unafuu kidogo?
At least hao ukiweka hizo CCTV ni rahisi kuwadaka.

Maana wengi wao ndio vile ..... Brain.

Wanaume wengi wajanja wajanja tu.

Kuna biashara zinataka Wanawake tu kuzirun hasa gesti.

Tena tafuta wenye misambwanda weka hata wawili au watatu
 
Mwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.

Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.

Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.

Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k

Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k

Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.

Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.

Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.

Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.

Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.

Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.

Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.

Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.

Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;

~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)

Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida

=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years

Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.

VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?

Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700

Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi

Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.

Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi

Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.

Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).

Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).

Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.

.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.

All in all Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Kiwanja mil.12 tena Wilayani,duu hiyo ni noma sana.
 
Moja ya application ya shule ni hii....
Hongera sana mkuu!
Hakuna Cha shule yeyote hapo,watu layman wanafanya hiyo sana tuu.

Inatakiwa akisharejesha pesa yake ndani ya miaka hiyo 4 ,apunguze bei ya lodge walau ifike 20,000-25,000 na baada tena ya miaka 5 apunguze zaidi iwe kayo ya 10,000-15,000 hapo maintainance costs zinaanza kupanda na vitu vinaanza kuchakaa.
 
Ya kwako yenye miaka 5 ushapunguza bei? (Acha shobo, appreciate kitu kizuri mtu anafanya)
 
Back
Top Bottom