ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 3,586
- 3,857
Hiyo line yako ya mwisho kuna wengine wateja hawapendi pulukushani za kelele sasa ukishaanza kuuza Pombe, supu, chakula hiyo sasa inakua sio lodge hata mazingira wateja wanaweza kimbia wale wastaarabu. Alafu ukiweka hivo vitu inakua lodge ya wahuni shortime, uchafu. Labda aweke ki bar nje ya lodge huko ambapo mteja akiitaji chakula inakua sio mbali kukifata na kelele za watu/miziki haziingii lodge.
Maana kuna logde zingine zenye bar ni kelele sana likipigwa "IN DA CLUB" la 50 cent unaweza hisi umo ndani chumbani kitanda kina dance imagine mziki huo mpaka saa saba au nane usiku huko na unataka kulala.
Lodge wewe weka vitu vya kawaida pale reception kama miswaki, maji, dawa ya mswaki, vitu vile vitakavomvutia mteja maana ni wa kulala na kuondoka.
Ukianza kuweka sijui chakula, pombe, mziki e.t.c hiyo sio lodge ni bar wateja utakaopata ni wahuni na kukuharibia lodge yako.
Muhimu kujali wateja wako. Wateja wengine asubuhi wanakula breakfast, saa nne wanakutana na washikaji wanaongea kidogo wanaenda kumaliza dili huko.
Wakirudi saa tisa, kumi wanakamilisha maongezi yao. Hapo wanaweza kuomba supu, nyama choma, nk wanaachana saa kumi na mbili. Ila mziki ni hapana. Hautakiwi kabisa.