HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Kufunga CCTV hidden itabidi ufunge mwenyewe ukifunga na fundi, fundi anaweza semaHizo hidden camera watakuwa hawazioni Kwa uwazi kama hizo camera nilizokwisha kuzifunga?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kufunga CCTV hidden itabidi ufunge mwenyewe ukifunga na fundi, fundi anaweza semaHizo hidden camera watakuwa hawazioni Kwa uwazi kama hizo camera nilizokwisha kuzifunga?
Mkuu nina lengo nihamie kwenye biashara ya madini unanishauri niwekeze kwenye eneo lipi mtaji kwangu sio tatizoKaribu sana kwenye biashara ya Uchimbaji.
Ukiwa na bahati huwezi kukosa millioni millioni, muhimu Kwa miezi ya awali uwe na funds za kukuwezesha ku-run biashara walau miezi 6 hadi 12 bila kutegemea fedha ya duarani.
Asante mkuu wa elimu nzuri ya kiuchumi hususani kwa vijana, hata mimi nina mpango huo wa kujenga nyumba ya kulala wageni nimekuja kugundua hiii ni biashara inayolipa kwa haraka kuliko nyumba za kupangaMwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.
Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.
Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.
Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k
Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k
Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.
Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.
Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.
Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.
Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.
Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.
Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.
Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.
Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;
~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)
Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida
=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years
Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.
VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?
Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700
Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi
Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.
Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi
Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.
Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).
Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).
Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.
.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.
All in all Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Shukrani Mkuu 🙏Asante mkuu wa elimu nzuri ya kiuchumi hususani kwa vijana, hata mimi nina mpango huo wa kujenga nyumba ya kulala wageni nimekuja kugundua hiii ni biashara inayolipa kwa haraka kuliko nyumba za kupanga
vipi chief kuhusu vitanda umeweka vya ukubwa gani pia ulijenga jiko, chumba cha kufulia pamja na reception kubwa kwa ajili ya wateja kuweza kupumzika, kupata maji, chai pamoja na kupiga stori mbili tatu nje ya vyumbani?
Jaribu njia ya kwenda Chamazi mkuu kidogo bei zitakuwa vizuri maana uwanja wa Azam naona ni mmoja wa uwanja utaotumika, naona Tanroad wamechafua sana majengo pembezoni mwa barabara kuwa wayaondoe ikiwemo bar zote maaruf za chamazi nahisi kabla ya mwaka huo Chamazi itakuwa na njia mbilimbili ikibidi hata mwendokasi maana upana wanaotanua ni mkubwa kidogo.Shukrani Mkuu [emoji120]
Kuhusu Ukubwa wa Vitanda, nimeweka vya 5*6 na magodo ya inchi 12
Sehemu ya Chai, Reception na Kufulia zipo bila kusahau parking.
Kwa tathmini niliyoifanya, nyumba za Kupangisha hazilipi kama zilivyo za Wageni.
Kama umetia nia ya kuwekeza huku, usisite pambana uje ukamilishe ndoto yako.
Gharama za ardhi zisingekuwa kubwa DSM, ningeweka nia ya kujenga nyingine ya walau Vyumba 20 hivi.
Maana Mwaka 2027 tutakuwa na Wageni wengi sana kwaajili ya mashindano ya AFCON
Umesema sahihi MkuuJaribu njia ya kwenda Chamazi mkuu kidogo bei zitakuwa vizuri maana uwanja wa Azam naona ni mmoja wa uwanja utaotumika, naona Tanroad wamechafua sana majengo pembezoni mwa barabara kuwa wayaondoe ikiwemo bar zote maaruf za chamazi nahisi kabla ya mwaka huo Chamazi itakuwa na njia mbilimbili ikibidi hata mwendokasi maana upana wanaotanua ni mkubwa kidogo.
Karibu sana boss naimani utanipako ajira namimi nitambe mjini[emoji28]Umesema sahihi Mkuu
Na bei za viwanja njia ile haijachangamka sana kama huku City centre, hopeful ukiwa na milioni 18-25 hivi unaweza kupata Kiwanja kizuri pembezoni mwa barabara.
Naona pia hata biashara za Baa pamoja na Vyakula itakuwa hot sana kipindi hicho
Absolutely yes, Lodge inalipaMwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.
Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.
Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.
Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k
Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k
Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.
Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.
Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.
Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.
Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.
Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.
Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.
Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.
Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;
~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)
Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida
=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years
Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.
VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?
Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700
Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi
Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.
Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi
Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.
Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).
Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).
Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.
.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.
All in all Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Mkuu naomba jina la hii lodge nitakuwa Mbeya kikazi kuanzia mwezi wa 6Kuhusu breakfast nakubaliana na wewe.
Mwaka Jana nilfikia lodge Fulani Iko mbeya mitaa ya mwanjelwa kama unaelekea isanga.
Iko katikati ya mtaa lakini mazingira wamejitahidi Kuya keep up.
Vyumba safi kabisa, maji ya kutosha. Breakfast Kila siku asubuhi.
Vitanda vizuri sana.
Wahudumu Wana lugha na ushirikiano mzuri.
Ilikuwa kipindi kile wasafi festival inafanyika mbeya.
Ziko room za 20,35 na 45
Japo Mimi nililala room ya 20 nilikuwa nakula breakfast canteen kwao wale 35 hadi 45 wanapeleke hadi room yaani room service.
Nilikaa pale siku 7 ,7×20 ni 140k.
Na vyumba vilijaaa. Just imagine.
Hapa panaitwa KUOKOKA NI LAZIMA Njombe hyo 😀😀😀Kuna lodge moja njombe niliipenda sana mm nikisafiri napenda kulala lodge wanazolala wasafiri au wafanyabiashara sio wenyeji wanaokuja kufanya ngono na ulevi lodge zenye bar mzik mnene kelele nyingi sipendi, napenda nikanywe bar ya karibu na nitakapolala, ile lodge wameweka bango kubwa juu ya paa "hauruhusiwi kuingia na mwanamke asiye mke wako, pombe,kelele,sigara haziruhusiwi" nilipapenda ni pa tulivu sana mashuka mablanket masafi sana, hata majina ya vyumba ni majina ya vitabu vya biblia na panajaa sana watu wanaopenda utulivu wapo wengi.
Wanakuonea huruma ya kukufisirisi mkopaji.mkopo kwa biashara ambayo haina mwaka siwezi kopesha .Kwa sababu kuna dynqmics unakuwa hujazijua za hiyo biashara.Asante Mkuu, ila Benki zinasumbua sana kwenye kutoa Mikopo Kwa biashara mpya.
Kuna haja Wizara ya Fedha/Benki Kuu wakalegeza masharti kwenye hizo Taasisi za Kibenki
Vinginevyo ndoto za Wajasirimali wengi zinakufa
Umesema sahihi Mkuu, lakini si Kuna hati za nyumba/viwanja wangepokea kama dhamana ili walau kusaidia Wajasiriamali wanaochipukiaWanakuonea huruma ya kukufisirisi mkopaji.mkopo kwa biashara ambayo haina mwaka siwezi kopesha .Kwa sababu kuna dynqmics unakuwa hujazijua za hiyo biashara.
Kuuza dhamana siyo lengo la kwanza la mkopeshaji ;sababu kuna usumbufu wa kuiuza dhamana.Mabenk wanataka kujiridhisha na uwezo wako wa kuingiza mapato.Waone angalau mtiririko wa kipato chako cha muda mrefu kutoka kwenye hiyo biashara,ndiyo wajue watakavyo kukakata.vinginevyo uweke dhamana halafu ukope nusu ya thamani ya dhamana ya soko.ili ukishindwa wauze kirahisi.Umesema sahihi Mkuu, lakini si Kuna hati za nyumba/viwanja wangepokea kama dhamana ili walau kusaidia Wajasiriamali wanaochipukia