Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Ila ni changamoto Kwa Wajasirimali wapya
Yeah ni kweli, ila sishauri mjasiriamali mdogo aanzishe biashara kwa mkopo tena bank,. Akifanya mistake kidogo tu anaweza ajutie na aogope kufanya tena biashara maisha yake yote.. Better mtu akajitafuta regardless atatumia mda gani ila aanze biashara kwa mtaji wake mwenyewe, mkopo uwe tu ni kama nyongeza kukuza mtaji basi
 
Yeah ni Kweli Mkuu.....ukithubutu unaweza kufa Kwa presha ya Kudaiwa 😅😅
 
Very helpful indeed mkuu. Asante kwa info za namna hii za kujenga. Nikiwa na mda kwenye huu uzi wako nitaweka practical input ya nyumba/vyumba vya kupanga.

Lodge zina return ya mda mfupi zaidi, japo running costs na maintenance nahisi zipo juu zaidi.
Shukrani Mkuu

Lodge ikiwa mpya maintenance cost zake zinakuwa Chini

Me nimejipanga kuifanyia marekebisho Kila mwisho wa mwaka.
 
Mwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.

Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.

Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.

Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k

Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k

Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.

Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.

Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.

Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.

Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.

Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.

Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.

Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.

Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;

~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)

Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida

=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years

Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.

VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?

Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700

Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi

Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.

Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi

Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.

Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).

Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).

Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.

.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.

All in Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
We jamaa umeandika research yako kisomi sana hongera mkuu, nimepata kitu hapo
 
Shukrani Mkuu

Lodge ikiwa mpya maintenance cost zake zinakuwa Chini

Me nimejipanga kuifanyia marekebisho Kila mwisho wa mwaka.
Ukifanya hivyo itakuwa up-to-date na kuzidi kuongeza mapato. Wengi wanajisahau hapo kwenye maintenance, unakuta showers hazifanyi kazi, maji ya moto mara yapo mara hayapo, hudum za Wi-Fi (optional) au huduma za dstv/azamtv zipo mara hazipo, wengi wanaanza na bed and breakfast then wanaishia kati.

All in all hongera sana, pia kwa kushare nasi kutupa changamoto za kimaendeleo.
 
Shukrani sana Mkuu
 
Shukrani Mkuu, kumbe inawezekana kusajiri biashara tofauti then ukaziweka kwenye kapu Moja?
Na sio kumbi ikikamilika tu hata wakati unaijenga unaweza ukajinga kama mali ya kampuni yako, gharama zotw za ujenzi unaziandika na zinakuwa kama gharama za kampuni na unaweza pata nafuu ya kodi kama uliziandika na kutunza risiti zote..

Mfano kama kwa mwaka mapato yako ni 30mil na ukawa na matumizi mfano ya ujezi wa kimbi na matumizi mengine ikawa 20mil hapo fedha utayotozwa kodi ni hiyo tofauti ya 30mil na 20mil = 10mil!

Pia kampuni inaweza kuwa na biashara hata 50!

Anyway mimi sio mtaalam wa kodi ila nimeongelea ujuzi kidogo nilionao!

All in all fikiria wazo la kampuni mkuu

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Shukrani sana Mkuu, nimejifunza mengi kwako.

Wazo la Kampuni ninalo ila nimeona hela nyingi zipo kwenye Starehe

Hivyo biashara zangu zitajikita huko

Wacha niendelee Kujitafuta
 
Back
Top Bottom