Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Umeshauri vizuri sana Mkuu

Iwapo Mamlaka zikafanyia kazi Ushauri wako, utaleta tija sana Kwa ma-hustler wengi Nchini
 

Hongera mkuu,
Kama mzee pia ninayepambana, umenipa motisha sana.
 
Najuta kujenga Apartment ya kupangisha,ni jana tu nimetoka kugombana na wapangaji wawili ambao mmoja hajanilipa tangu mwezi April na mwingine tangu Mei kila siku sound tu!!ningejenga Lodge nisingepata usumbufu kama huu. Cha kushangaza hawa wapangaji wangu wanaonisumbua Kodi wameshawajaza wake zao mimba,najiuliza nguvu na hamu za kutomba wanazipata wapi ilihali Kodi hawalipi. Nimewapa notisi mwisho wa mwezi huu wawe wameondoka
 
Hahaha........pole Mkuu Kwa kadhia unayopitia.

Biashara ya nyumba za Kupangisha, ina adha kubwa ya baadhi ya wapangaji kushindwa kulipa Kodi zao Kwa wakati.

Mimi pia nimelazimika kubadirisha kitasa Kwa mmoja wa wapangaji wangu baada ya kushindwa kulipa Kodi yake Kwa miezi 5 sasa, bahati mbaya hata simu hapokei.

Kama utaweza jipange uwekeze kwenye biashara ya Lodge ambayo walau ina unafuu kuliko nyumba za Kupangisha
 

Pole sana mkuu ila ndio hivyo, sometimes hawa wapangaji wanatuona wenye nyumba muda wote tuna fedha.
Mimi mwenyewe kuna sehemu nina viapartment nimevipanga kimkakati ili nivibadilishe kuwa lodge hapo baadae
All in all biashara ya nyumba inalipa sana inspite of changamoto ndogondogo.
 
Asante Mkuu

Nafikiri ni suala la kukosa uungwana.

Baba mwenye nyumba Mimi ni muelewa Kwa mtu ambaye anaweza kutoa taarifa ya kuchelewa kutoa hela yake ya Kodi, nipo tayari kumsubiria hata miezi 6 lakini akiwa ametoa taarifa.

Huyo Kijana nimelazimika kubadiri kitasa baada ya kuona simu zangu hapokei, kingine ni tabia yake ya kuingia usiku mnene na kuwahi kutoka saa 11 alfajiri.

Nikajua huyu anataka kunikimbia bila kunilipa Kodi yangu.
 
Mkuu Ile ushauri wa kufungua kampuni kwa ajili ya unafuu wa Kodi umefikia wapi..?
 
Ndio maana ni muhimu sana kuuliza ajira au shughuli ya mtu ambaye unataka kumpangishia
 
Polee sana mkuu.. Biashara yoyote ile haikosi changamoto, ukisema lodge bila shaka wenye lodge wapo uku watatupa uzoefu ..usimamizi wa lodge ni mgumu sana. Alot of variables to handle.

Changamoto ya wapangaji kutolipa kodi inatokana na kutokuwa na mfumo mzuri wa malipo. Usikubali mtu aishi kwenye nyumba yako in advance, yaani aishi atalipa akijiskia.. nyumba umetengeneza kwa gharama sana, pengine umekopa.. upangishe kwa mkopo!
Kodi ni miezi mi 3, 6 au 12, kulingana na ubora na location ya nyumba, ..na mteja analipa mwanzo kabla hajaishi.

Tafuta mwanasheria akutengenezee mkataba na kipindi cha kusainishana awepo.. (sikuiz wako wengi sana mtaani wana mihuri hawana kazi). mkataba uweke wazi grace period, unayotoa kodi inapoisha.

Kuna level ukifika huitaji kujuana na mpangaji kabisa, yeye atapambana na mwanasheria wako.
Hii itakusaidia pia kutunza ubora wa nyumba yako, kuna wapangaji wanachafua sana ukuta, wanavunja vioo, masink chooni.. kwenye mkataba inabidi kipengele cha utunzaji wa mali kiwepo.. vitakavyoharibika nyumba ikiwa chini yake atalipa..

Kuna gharama ambazo utazikwepa na kuziona sio muhimu, zikagharimu investment ya millions of money.
Mfano mzuri, ni Bima ya gari sio muhimu ad litakapopata ajali.
.
 
Marekani kule ukihamia kwenye nyumba ya mtu unaweka deposit ambayo kwa kawaida huwa ni kodi ya mwezi mmoja. Ukiondoka kwenye hiyo apartment ni lazima uiache kama ulivyoikuta. Ukiondoka nyumba ikiwa salama deposit yako unarudishiwa. Vinginevyo itatumika kwenye matengenezo yote ambayo mwenye nyumba itabidi afanye kabla mpangaji mwingine hajaingia. Hii huwa inasaidia wapangaji kutoharibu vitu makusudi mbali na tear and wear za kawaida.

Na ukienda kupanga kwingine lazima useme ulikopanga kwa mara ya mwisho na lazima watawasiliana naye. Akisema kuwa huyo mpangaji ni bomu aisee hupangishwi. Na ikitokea ukabadilishiwa kitasa hiyo inaingia kwenye rekodi moja kwa moja na itakuwia vigumu sana kupata sehemu ya kupanga maana kila mtu atakuwa anakukimbia.

Mifumo kama hii huwa inasaidia. Sisi huku mtu anaharibu nyumba makusudi na hakuna kitu utamfanya!
 
Very right! πŸ‘, hela yake ikiwa rehani atatunza nyumba tu!
 
Mkuu Ile ushauri wa kufungua kampuni kwa ajili ya unafuu wa Kodi umefikia wapi..?
Nipo kwenye Process, nimeshaenda baadhi ya Taasisi za Serikali ikiwemo TRA kwaajili ya kupata miongozo yao.

Hopefully Mwakani panapo Majaaliwa itakuwa tayari.

Bila kutumia mbinu hiyo, TRA hawana utani kwenye Kodi zao πŸ™Œ
 
Ndio maana ni muhimu sana kuuliza ajira au shughuli ya mtu ambaye unataka kumpangishia
Sahihi, nimewahi kupata tukio moja Mwaka Juzi.

Kuna Kijana mmoja alikuja kumpangia nyumba binti mmoja kwenye apartment yangu, alimlipia Kodi ya miezi 8, baadaye akaja kuongeza Kodi ya miezi 4. Jumla miezi 12.

Ilipobaki miezi 3 Kodi yao kuisha, nilifanya kuwakumbusha (Nina kawaida ya kumjulisha Mpangaji kwamba Kodi yao inakaribia kuisha Kila ikibaki miezi 3).

Yule binti amekaa, hadi Kodi ikaisha, nikampa wiki moja awe amenilipa Kodi yangu ama ahame.

Binti hana hela, na kumbe yule Boyfriend yake aliyekuwa anamlipia Kodi ameachana naye πŸ™Œ

Usumbufu ukawa mwingi pamoja na Kiswahili, baada ya wiki 2 nikamtolea Vyombo vyake Kwa nguvu.

Hii ni changamoto za kuwa na Wapangaji Wasumbufu wasio na Kipato cha kueleweka
 
Sio vibaya kujifunza vitu vizuri, nadhani hii idea yako ni nzuri.

Ukipata Mpangaji, unamsainisha Mkataba wa namna hiyo ili kulinda nyumba yako Incase akaiharibu kwa namna moja ama nyingine
 
Very right, japo unaweza kuonekana Mnoko Kwa Wapangaji lakini inasaidia kulinda asset yako.

Kodi zenyewe hazifanani hata na hela uliyotumia kujengea πŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…