cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Naomba kazi kwako, wee tena unataka nikununulie kiko?Hahaha..........ninunulie Kiko kwanza Babu yako nivute [emoji12]
Au ndo unanyima kazi kijanja? Haya bhana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba kazi kwako, wee tena unataka nikununulie kiko?Hahaha..........ninunulie Kiko kwanza Babu yako nivute [emoji12]
Hii ni idea nzuri sana, Kwa njia hii unaweza jikuta unamiliki Lodge/Hotel hata City CenterUzi nzuri Sana ..naomba kuongezea...
Kuhusu wizi tumia technology..nenda jukwaa la IT wakueleze kuhusu vitasa vya card. Na software zake iwe chumba kikipata Tu mgeni unapata notifications hapo hapo...hata kama wa short time.....
Kwingine since wewe ni mpya kwenye biashara nashauri Fanya research ya lodge zilizo kufa au kukosa soko ikiwezekana uzi Kodi upige hela ..
Wengi wanashindwa maintenance Tu...sasa badala ya wewe kutumia hela nyingi kujenga zingine ...jaribu kukodi Kwa mkataba mrefu ..itakusaidia vitu viwili....kwanza utapunguza competition since competition umeinunua...pili utantumia hela ndogo for expansion...
Unaweza amini kkoo kuna hotel inakodishwa Kwa milioni 4 Tu Kwa mwezi wakati ni jengo la ghorofa 8..?
kisa muasisi kafa na watoto wanakula hela yote hawafanyi maintenance..
All in all nakutakia all the best miaka miachache kutoka sasa uwe na lodge hata tano...
Kwa startup business huwa ni ngumu sana kupata investment capital.Babu Hongera Sana Sana kwa hiyo hatua ni wengi tunatamani kufanya kitu Cha hivyo tatizo ni vyanzo
Sure sure mwanzo ni mgumu Sana lakini pia umejitahidi kakaKwa startup business huwa ni ngumu sana kupata investment capital.
Mfano mwenyewe nimetumia miezi 12 kukamilisha Mradi, ambapo ningekuwa na fedha za kutosha ningejenga Chini ya miezi 3 hadi kukamilisha kwake
nina ujuzi juu ya masuala ya umeme na IT.... kwenye hii kero yako ya vijana kuharibu kamera,. muelekeze mtaalamu wako anaekufungia kamera, naamini atakusaidia kwa urahisi tu....kwasasa tuna mini-cameras unazoweza connect na Smart phone yako lakini itakutaka uwe na internet connection muda wote...hivyo unaweza ongeza huduma ya wi-fi kwa wateja wako, hata wa VIP tu kwa kuanza lakini huku ikiendelea kukusaidia na wewe kwenye ulinzi wa mapato yako... kipindi najitafuta nimechimba sana madini huko, kwanzia mawelu,mapapai,soweto,sangambi, isoko mpaka igundu huko...hivyo huko ni nyumbani naamini naweza kuja kukutembelea ndugu... KAZI NJEMA kwakoAsante Mkuu
Watanzania wengi sio waaminifu
Baada ya kuichezea Camera saivi analeta hela anayojisikia maana anasema Leo wamelala wateja 7 kumbe wamelala 9
Nimetengeneza mara 3 lakini baada ya muda inaharibika Tena.
Nina hakika ningekuwa nakaa mwenyewe huenda Payback period ingeshuka hadi miaka 2
Maana nahisi napoteza Mapato mengi Kwa Wizi wao Hawa Vijana
Haya ndiyo mambo tunahitahi humu kwakuwa ni mafunzo kwa sisi wajasiliamali, hongera sanaMwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.
Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.
Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.
Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k
Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k
Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.
Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.
Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.
Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.
Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.
Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.
Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.
Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.
Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;
~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)
Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida
=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years
Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.
VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?
Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700
Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi
Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.
Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi
Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.
Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).
Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).
Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.
.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.
All in Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Benefits zake ni zipi
Hata yule msamaria alipomsaidia mtu aliyejeruhiwa na kuporwa na wanyamg'anyi alimpeleka nyumba ya wageni na kumkabidhi pale na kumlipia cost ambazo angetumia kuuguzwa.Unakumbuka Wazazi wake Yesu walipokwenda ugenini kule kwaajili ya kuhesabiwa na kukosa nyumba za Kulala Wageni hadi kupelekea Walale kwenye Zizi la ng'ombe na Yesu kuzaliwa humo?
Imagine kama hii yangu ingekuwepo nyakati hizo, si wangelala kwangu 🤗
Hilo nimechomekea tu Mkuu.... shukrani sana
Kwa kujazia alichosema Grahams
Mfano mteja kaja kwenye lodge akapigwa shoti bafuni akafa au akapata tatizo lolote ambalo mmiliki atatakiwa kufidia, ukiwa huna kampuni mahakama itatumia mpaka nyumba yako ya kulala ili kufidia! Ila ukiwa na kampuni mali zitazokua kwenye risk ni mali za kampuni tu!
2. Kingine ni kwenye kodi, ukiwa na kampuni unaweza usilipe hata shilingi moja provided unatunza gharama mapato na matumizi yako. Tena mda huu anapofanya matengenezo let say ya kumbi ndio mzuri zaidi, gharama zote za ujenzi wa kumbi anaweza wasilisha kama gharama za kampuni na akiwasilisha gharama za mwaka akapatiwa nafuu ya kodi.. angalia hii mifano
A. Assume ana mapato ya 20mil kwa mwaka, bila kampuni tra wataangalia hii 20m kama pato na kukisia jamaa alipe kiasi gani! Hapa anakua hana nguvu ya kucontrol kiasi cha kodi.
B. Chukulia amesajili kampuni na ana mapato ya 20mil kwa mwaka, alafu ndani ya mwaka huo huo akaanza ujenzi wa kumbi na akatumia let say 15mil! Kama alisajili hii kumbi ni mali kampuni basi hii 15mil itaingia kama expense za kampuni... so tra wakija jamaa kupitia mhasibu wake watasema tumepata 20mil lakini tulikua na matumizi ya 15mil ya ujenzi wa kumbi ambayo ni mali ya kampuni hii.. hapo watatoa 20mil - 15mil = 5mil!
Kwa hiyo hii 5mil ambayo ndio faida ndio itatumika katika ku estimate kodi na sio 20mil nzima! Na hapo ni rahisi maana inajulikana kodi ya kampuni ni 30% ya faida!
NB: mimi sio mtaalam wa kodi au mhasibu nimetumia uzoefu na ujuzi wangu mdogo kuhusu makampuni!
Kwa ziada angalia hii video kutoka BRELA:
View: https://youtu.be/DAlo0hOniE4?si=1gD3vPkiHpq
Wengi tunaishia kwenye mipango kama hv,Sahihi Mkuu
Ila najipanga kufungua biashara ya Starehe kama Liquid Pub ama Bambalaga
Nimeifanyia tathmini hahitaji hela ndefu kidogo ila Mtaji unarudi mapema pia
Ukiwa na nia unaweza kufanikiwa hasa ukitia bidii.Wengi tunaishia kwenye mipango kama hv,
Wenye uthubutu ni wachache!!