Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

mkuu kama itakupendeza nitumie picha dm yangu maana mimi nilikuwa mbioni kujenga lodge baada ya wapangaji kunisumbua sana ila mimi nilitaka kuweka mfumo wa slab ili ikikuwa naongea kwa juu tu
Kujenga Kwa mfumo huo angalia kwanza uimara wa nguzo zako kama wali-design kubeba mzigo huo.

Vinginevyo bomoa uanze upya ama kufanya underpinning ili ku-stablize jengo lako ili kuruhusu hicho unachopanga kufanya.
 
kwa kweli mkuu umenipa moyo sana maana nyumba za kupanga ni usumbufu mkubwa sana na bado itachukua muda mrefu sana kurudisha garama zako
Nina nyumba nimepangisha, kutokana na gharama nilizotumia kujenga nimebaini itachukua miaka 15 Hela yangu kurudi.

Hata hivyo naiacha as naitumia kupata ada za Vijana wangu Kwa uhakika
 
Mkuu hongera.

Lakini pia pole kwa uwizi wa watanzania. Hii nchi hovyo sana na hatutaweza kuendelea kwa kizazi hiki. Labda kutokee muujiza wa wale wenye uzalendo wa kweli kuchukua nchi.

Kuna wakati watu wanalaumu wachina eti kwanini wakipewa tenda kubwa za ujenzi wanaleta vibarua kutoka kwao uchina. Shida ni wizi wa watanzania kuanzia juu hadi chini.

Nchi ya hovyo sana hii. Watu wengi wa hovyo.
Asante Mkuu

Watanzania wengi sio waaminifu

Baada ya kuichezea Camera saivi analeta hela anayojisikia maana anasema Leo wamelala wateja 7 kumbe wamelala 9

Nimetengeneza mara 3 lakini baada ya muda inaharibika Tena.

Nina hakika ningekuwa nakaa mwenyewe huenda Payback period ingeshuka hadi miaka 2

Maana nahisi napoteza Mapato mengi Kwa Wizi wao Hawa Vijana
 
kuhusu uimara nazingatia sana hilo mkuu maana mimi ni mjenzi pia lakini ukiweka mfumo wa slab inarahisisha kuongeza mambo mengine kama mgahawa na mengineo manaa tatizo la mazingira yetu ni maeneo kuwa madogo na ukitaka kiwanja cha jirani atakuuzia bei ya kukomoa
Umesema sahihi Mkuu

Tuendelee kukomaa tu
 
Kwa pesa hiyo ungeanzisha Restaurant ya maana na kupata wapishi wazuri ungepata faida na pesa zako zingerudi haraka na faida kubwa
Mwanzo unakuwa mgumu lakini baada ya muda utaona faida.
Inategemea pia eneo la biashara na mzunguko wa pesa.
Restaurant ukiweza kuiendesha vizuri hukosi laki 3 mpaka 5 kila siku.
Nafanya biashara hiyo Arusha
 
Asante Mkuu, ila Benki zinasumbua sana kwenye kutoa Mikopo Kwa biashara mpya.

Kuna haja Wizara ya Fedha/Benki Kuu wakalegeza masharti kwenye hizo Taasisi za Kibenki

Vinginevyo ndoto za Wajasirimali wengi zinakufa
Hongera sana mkuu suala la benki jaribu kuongea vizuri na meneja Tanzania hakuna kinachoshindikana
 
Hongera sana Babu, uzi mzuri wa mwanzo wa mwaka. Ngoja nisabuskraibu, Japo sijui nitapata lini pesa tena.

Lodge wilayani nadhani ni biashara nzuri, kwa sisi tunaosafiri kama team mkifika sehemu mnavamia lodge/hotel yote siku 5-7 lazima tajiri atajirike.
Asante Mjukuu

Wanasema Mwanzo mgumu ila ukitia nia unaweza kufanikisha japo unaweza kuchukua muda

Kuna Siku nilipata Wageni dizaini hiyo unayosema ya watu 8 na walikaa wiki 1.

Unakuta Kila Siku mzigo unasoma SIM banking 😅
 
Kwa pesa hiyo ungeanzisha Restaurant ya maana na kupata wapishi wazuri ungepata faida na pesa zako zingerudi haraka na faida kubwa
Mwanzo unakuwa mgumu lakini baada ya muda utaona faida.
Inategemea pia eneo la biashara na mzunguko wa pesa.
Restaurant ukiweza kuiendesha vizuri hukosi laki 3 mpaka 5 kila siku.
Nafanya biashara hiyo Arusha
Biashara ya chakula nitaifanya iambatane na Vinywaji.

Nataka nijenge dizaini ya Kitambaa Cheupe ama Bambalaga
 
Mwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.

Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.

Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.

Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k

Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k

Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.

Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.

Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.

Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.

Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.

Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.

Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.

Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.

Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;

~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)

Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida

=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years

Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.

VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?

Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700

Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi

Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.

Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi

Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.

Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).

Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).

Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.

.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.

All in Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Tuwekee na ramani ya hiyo project mkuu!!
 
Back
Top Bottom