Nitaifanyia utafiti hiyo biashara pamoja na Soko lake.Wee utakuwa unaishi ddm
VIP kuhusu apartment mnk Kuna apartment inalipwa 5000 kwa mwezi hspa ddm je hazilipi
Kuhusu breakfast nakubaliana na wewe.Kitu kingine, ongeza nguvu sana kwenye social media na marketing. Uzuri ni kwamba kila kitu ni kipya tumia fursa hiyo kujitangaza. Wabongo wengi wavivu na wanadharau nguvu ya mitandao, au wanawekeza kidogo sana. Mtu katumia 100M+ ukimwambia tia 1M kwenye social media anakataa wakati hela inakuja.
Ukitumia mtandao vizuri na ukawa na consistency utapata wateja wengi na badala ya hesabu ya vyumba vinne kati ya 10 ukajaza zaidi ya hapo. Weka na mfumo wa kujua vyumba vipo wazi au vimejaa, utaratibu wa kufanya booking mapema, hakikisha breakfast haikosi hii sio utani.
Nyumba ya wageni inayotegemea bodaboda na wenyeji wajitutumue ndio waingie haijawahi kuishinda inayotegemea wageni. Sasa wageni watakujua vipi. Imagine hapa nimesearch polyclinic nikapewa hizi options, fikiria mtu anaenda hiyo wilaya akatafuta lodge zilizopo akapewa hiyo kati ya machaguo ya kwanzaView attachment 2884969
Kama una wiwa kubadiri Uwekezaji Fanya Mkuu, Soko la biashara ya nyumba za Kulala Wageni zenye quality and standards ni chache sana.Nimekupata mkuu mawazo yako mazuri sana .
Kuna mada nimeziona kuhusu Airbnb nazo nazisoma Kwa kina kujifunza .
Kuna jamaa nimeona kabadili nyumba zake za kupanga kuwa lodge na anapata wateja . Nyumba zangu nzuri kulipo Kwa huyo mshkaji wangu
NAKAZIASoko la biashara ya nyumba za Kulala Wageni zenye quality and standards ni chache sana.
Nimeona pia Kuna mdau alichangia juu ya kutoa huduma za breakfast, Wi-Fi huduma ya Vinywaji na Chakula pia maana Kuna wateja wakisharudi room huwa hawataki kutoka nje Tena kwaajili ya kutafuta chakula na Vinywaji.Kuhusu breakfast nakubaliana na wewe.
Mwaka Jana nilfikia lodge Fulani Iko mbeya mitaa ya mwanjelwa kama unaelekea isanga.
Iko katikati ya mtaa lakini mazingira wamejitahidi Kuya keep up.
Vyumba safi kabisa, maji ya kutosha. Breakfast Kila siku asubuhi.
Vitanda vizuri sana.
Wahudumu Wana lugha na ushirikiano mzuri.
Ilikuwa kipindi kile wasafi festival inafanyika mbeya.
Ziko room za 20,35 na 45
Japo Mimi nililala room ya 20 nilikuwa nakula breakfast canteen kwao wale 35 hadi 45 wanapeleke hadi room yaani room service.
Nilikaa pale siku 7 ,7Γ20 ni 140k.
Na vyumba vilijaaa. Just imagine.
Tumia Wanawake kwenye hii biashara achana na wanaumeAsante Mkuu
Watanzania wengi sio waaminifu
Baada ya kuichezea Camera saivi analeta hela anayojisikia maana anasema Leo wamelala wateja 7 kumbe wamelala 9
Nimetengeneza mara 3 lakini baada ya muda inaharibika Tena.
Nina hakika ningekuwa nakaa mwenyewe huenda Payback period ingeshuka hadi miaka 2
Maana nahisi napoteza Mapato mengi Kwa Wizi wao Hawa Vijana
Nasikia biashara ya Lodge short time ndio inarudisha hela kuliko watu kulalaπ, ukiwa na mfanyakazi mwaminifu na eneo lako lipo mafichoni kidogo mbona unaulaMwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.
Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.
Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.
Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k
Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k
Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.
Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.
Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.
Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.
Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.
Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.
Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.
Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.
Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;
~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)
Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekezaΓ·Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida
=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years
Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.
VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?
Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700
Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi
Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.
Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700Γ·7,200,000
Miaka 13.2 hivi
Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.
Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).
Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).
Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.
.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.
All in Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Short time itaharibu biashara maana Lodge inakuwa kama danguro tu.Nasikia biashara ya Lodge short time ndio inarudisha hela kuliko watu kulalaπ, ukiwa na mfanyakazi mwaminifu na eneo lako lipo mafichoni kidogo mbona unaula
Ila ndio hivyo tena, mambo ya ulimwengu hayo
Kabisa yaani hasa ikiwa classic na nzuriHongera sana Babu, uzi mzuri wa mwanzo wa mwaka. Ngoja nisabuskraibu, Japo sijui nitapata lini pesa tena.
Lodge wilayani nadhani ni biashara nzuri, kwa sisi tunaosafiri kama team mkifika sehemu mnavamia lodge/hotel yote siku 5-7 lazima tajiri atajirike.
Mimi nafikiria kufungua danguro kama yule jamaa wa RiversideShukrani Mkuu π π
Of course standards na quality ni muhimu sana kwenye hii biasharaNAKAZIA
Hahaa hawa ndio maana wengine wanajengea vitanda vya tofaliShida Kuna Vijana wakiingia na Mademu zao wanavitumia hovyo utasema anataka kuua Binti wa watu humo ndani π
Hawathamini hela mwenzao niliyoweka bado hata haijarudiHahaa hawa ndio maana wengine wanajengea vitanda vya tofali
Kama mwanza huko,niliona aiseh nikashangaa sana!!Hahaa hawa ndio maana wengine wanajengea vitanda vya tofali