Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Ndoa kwa Zama hizi ni taasisi iliyo shindwa kuji tetea😄.
👉Beside mi chalii tu, hata nusu ya 50 bado😄
Uje nikupe Madini ya kwanini uingie kwenye Ndoa

Kama bado hujafika huo umri basi una uelewa Mkubwa wa mambo Mtambuka.

Jitahidi uzae mtoto kwenye huo umri ili upate watoto genius
 
Uje nikupe Madini ya kwanini uingie kwenye Ndoa

Kama bado hujafika huo umri basi una uelewa Mkubwa wa mambo Mtambuka.

Jitahidi uzae mtoto kwenye huo umri ili upate watoto genius
thanks for the appreciation 💪🙏, hii nime rithi kwa mzee wangu Ushimen
👉Ila kuhusu mdoa mhhh, maybe another time mkuu.

Acha tupambanie ugali kwanza mzee, Zama zime badilika mno
 
thanks for the appreciation 💪🙏, hii nime rithi kwa mzee wangu Ushimen
👉Ila kuhusu mdoa mhhh, maybe another time mkuu.

Acha tupambanie ugali kwanza mzee, Zama zime badilika mno
Kila la heri Mkuu

Binafsi I had my first born at 26 japo nilibahatika mapema kupata ajira baada ya Chuo
 
Bar, lodge na hoteli ni kati ya biashara ambazo kwangu naona ugumu kuzifanya ingawa zina faida.
Zipo tofauti na Imani Yako Mkuu?

Ukiwa na mtazamo huo hata biashara ya Madini ndiyo hutaweza kuja kuifanya.

Maana huko bila kujenga urafiki na Waalamu utajikuta miaka na miaka unachimba lakini "hutoboi" kama asemavyo Mzee Bwege
 
Hivi musoma mjini kunafaa kuwekeza biashara ya lodge?. Kwa waliopo huko naomba muongozo.
Musoma kama utajenga Lodge nashauri ukajenge karibu na Ferry wanapofanyia shughuli za Uvuvi.

Kuna Lodge Moja nililala kule Bunda wanakouza uza dagaa wanaita Soko la Tunduma.

Jamaa amejenga karibu kabisa na Ziwa.

Mara nyingi Guest yake inakuwa imejaa maana Wageni wakija kufunga mzigo wa dagaa wanafikia pale kwake
 
Hii biashara ni nzuri ukibahatika kupata location nzuri
Yeah....wakati unachagua site kwaajili ya kujenga zingatia Hilo suala.

Bora ununue Kiwanja gharama kubwa lakini uwe na uhakika wa kufanya biashara
 
Mzee mwenzangu Kudos sana...
Naomba kujua hawa wageni na wachakataji sio kwamba hua wanapendelea gesti zikiwa mpya? Ndani ya miaka mitatu sio kwamba itahitajika uwe ushaifufua upya ili uwe na consistency kwenye mauzo?

Ukitaka kuisukuma uniambie nipate ya udalali hapo
 
Mwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.

Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.

Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.

Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k

Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k

Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.

Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.

Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.

Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.

Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.

Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.

Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.

Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.

Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;

~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)

Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida

=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years

Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.

VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?

Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700

Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi

Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.

Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi

Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.

Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).

Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).

Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.

.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.

All in all Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
👏👏👏👏
 
Babu hongera sana, hiyo biashara nzuri sana..!! Hapo anza kujenga nyingine ukishapaua ingia bank wakupe mkopo wa kumalizia ujenzi utanishukuru..!!
 
Mzee mwenzangu Kudos sana...
Naomba kujua hawa wageni na wachakataji sio kwamba hua wanapendelea gesti zikiwa mpya? Ndani ya miaka mitatu sio kwamba itahitajika uwe ushaifufua upya ili uwe na consistency kwenye mauzo?

Ukitaka kuisukuma uniambie nipate ya udalali hapo
Shukrani Mkuu 🙏🙏

Biashara ya real Estate inahitaji maintenance ya mara Kwa mara, hivyo nitakuwa nafanya ukarabati Kila baada ya miaka 3 japo zile minor repairs za accessories nafanya Kila Mwezi. Mfano Kuna baadhi ya Wateja hawajazoea kutumia bomba la mvua (shower) pamoja na zile bomba za kunawia ukitita.

Kwahiyo mara nyingi vinahitaji kubadirishwa mara Kwa mara

Kuhusu kuuza Sina mpango ila kama utaona Lodge potential mtu anauza nitaomba unijulishe

Wanasema Koo(Clan) zilizokuwa zinakuwa ndiyo zilikuwa zinatawala 🤗

Vivyo hivyo biashara lazima iwe na sifa ya Kukua na kuongezeka
 
Babu hongera sana, hiyo biashara nzuri sana..!! Hapo anza kujenga nyingine ukishapaua ingia bank wakupe mkopo wa kumalizia ujenzi utanishukuru..!!
Shukrani Mjukuu, ngoja tutumie vizuri hela za Kiinua mgongo (Pension) kuwekeza kabla hazijapitiwa na akina Mobero, maana wanasifa ya kinusa hela ilipo😜
 
Back
Top Bottom