Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Wewe ni mwathirika wa mfumo mbovu wa elimu ya Tanzania. Yote uliyoelezea hapa na hizo ''faida'' unazosema umepata zinaonyesha jinsi ulivyoathirika na elimu yetu!
 
Yes uko sahihi, ila hoja yangu ni kwamba hizi shule za English Medium kama umejipanga siyo shule mbaya Sababu nzuri zipo na mbaya zipo pia. Mimi na pendelea zaidi shule binafsi zinazosimamiwa na taasisi za kidini au za Wahindi, za waswahili nyingi ni za hovyo. Shule zetu za serikali ni hovyo mnoo na kwa dunia tunayokwenda Mtoto hataweza pata vitu vya msingi vinavyokwenda na wakati. Chukulia mfano Agha khan Primary School huwezi fananisha na shule yoyote ya msingi ya serikali.
 
" English Medium zawaswahili nyingi ni ovyo" upo sahihi kabisa mkuu. Mbaya zaidi hizo za waswahili ndo zipo nyingi ndo maana ninaziita kayumba zilizo changamka
Wyatt Mathewson
 
Elimu ni nini?
Mpeleke mwanao shule ya Kayumba kama huna hela, ila usimpeleke mwanao Kayumba ili ujenge. Elimu ya msingi ni muhimu sana kama una uwezo mtoto asome shule nzuri. sio kila English Medium ni mbaya, nzuri zipo nyingi tu inategemea na mzazi ulifanya utafiti kabla au ulibabaishwa tu na majengo na mabasi mazuri ya kubebea watoto.
 
Umenikumbusha kuna lecture mmoja pale muhas kasoma st kayumba anaitwa david thomas kasomea mtera dam sec na form 4 2010 alitoka na 1

Kipanga wa st.kayumba anakuwaga kipanga kweli kweli tena wa kujitengeneza mwenyewe na sio wakutengenezwa..

Watu wana jua ukweli ila wanajifanya tu
 

Ukiwa na hela ndo uzitumie kizembe mkuu? Hiyo haipo. Mpeleke Kayumba halafu msimamie vizuri atatoboa tu mkuu.

Umeongea point nzuri sana halafu tena unataka kuharibu.


Umesema English Medium za waswahili nyingi ni ovyo. Ni ubabaishaji mtupu.
 
Takataka
 
Huyo dogo ulitegemea apewe msaada na taasisi alafu wamtelekeze wakati yupo vizuri darasani
Sijakataa mtt kusoma hizo shule mpeleke ukiwa na uwezo na kwasabb ya kupata elimu bora na mazingira mazuri ya kujisomea
 
Hahaha...comment yako noma
 
Shule nzuri ni shule ambayo ina utilize uwezo wa mtoto.

St Kayumba sio good option kwa mtoto unless kipato sio kizuri. Nimesoma st kayumba from p' to o'level kwahiyo najua kitu nachokizungumza hapa so you better pay attention!

Watoto wanao excel shule za kayumba academically mostly wana biological advantage (wamezaliwa na uwezo mkubwa wa akili wa kuhifadhi kumbukumbu vizuri). Na wachache sana wanafaulu kwa jitihada binafsi za wazazi kama kuwapeleka tuition na ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mtoto shuleni (kuangalia kama anafanya homework vizuri n.k). Ila watoto wengi wa Kayumba wapo kwenye hatari kubwa sana ya kuharibikiwa. Nina mifano hai ya kutosha, so you better listen careful.

Anyday of the week, nitapigia kura International/English Medium over Kayumba kwa sababu ya utofauti mkubwa wa mifumo yao ya uendeshaji. Yes you heard me well, SYSTEM!

Mdogo wangu alibahatika kusomeshwa English medium, wakati yupo std 6 nilikua napiga naye story za hapa na pale nikagundua anajua vitu vingi ambavyo laiti angesimamishwa na hawa form four wengi wa kata kwenye debate, kwa kweli ingekua ni aibu.

Sasa shida iko wapi?

Kayumba hakuna ufuatiliaji wa karibu kwa watoto. At least hata English Medium za mchongo wanamrudisha mtoto mpaka nyumbani na wanampitia tena Ahsubuhi. Kila siku mtoto lazima aachiwe homework za kutosha kumpunguzia muda wa kucheza mtaani hovyo (Aliyocheza shuleni inatosha!).

Ila Kayumba mzazi huna uhakika kama mtoto kafika shule, huna uhakika kama mtoto atarudi nyumbani salama, huna uhakika kama muda aliofika nyumbani ndio wenyewe au kuna mahali kapitia, huna uhakika kama hajaachiwa homework au kaachiwa, hujui marafiki zake ni kina nani, hujui kama anahudhuria vipindi vyote au lah... na ikitokea siku umeitwa Shule ujue kabisa kuna kosa kubwa sana kafanya maana haya mengine ya ufaulu walimu sio shida zao, utajua mwenyewe na mtoto wako!
 
Neno langu la faraja kwako ni kwamba

Watu tumesema shule hizohizo ymza kayumba na kata, tukaongea kingereza na kufaulu vizuri tu

Ila kinachohitajika sasa mazingira ya nyumbani hakikisha yawe ya kisomi.

Vitabu vingi, waunganishe maktaba, wajisomee sana.

Waache uswahili wote
 
" English Medium zawaswahili nyingi ni ovyo" upo sahihi kabisa mkuu. Mbaya zaidi hizo za waswahili ndo zipo nyingi ndo maana ninaziita kayumba zilizo changamka
Wyatt Mathewson
Mkuu

Any shule inayofata British GCSE au International Baccalaurette (IB) ndio international school hizo zingine ni shule za Kitanzania za private tu

Nafikiri bado hatujaelewana nini maana ya International School hapa Tanzania

Mna confuse shule ya Tanzanian curriculum ambazo ni private ambazo ni sawa tu na shule za serikali kimuundo

The real international school we are talking about here are IB and GCSE based schools not otherwise

Do not confuse please
 
Nina mtoto anasoma la Kwanza ila ana mwandiko mzuri kuliko darasa la 7 wa Kayumba
Anapiga hesabu za darasa la 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…