Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Wewe ni mwathirika wa mfumo mbovu wa elimu ya Tanzania. Yote uliyoelezea hapa na hizo ''faida'' unazosema umepata zinaonyesha jinsi ulivyoathirika na elimu yetu!
 
Ni kweli mkuu ila Nina watoto wanasoma shule moja jijini 2M per each, Kwa mwaka 4.M yaani mkuu inanisononeshansana kuona wanakaririshwa tu. Nimewaza sans baada ya kusoma Uzi huu.

Kibaya zaidi mkurugenz ameweka burser/mhasibu Hana huruma.

Naendelea kuwaza lkn elim ni Bora kuliko kiwanja. Lkn wapi Sasa tunakwenda.

Mimi n mtumish wa imma. Serikalini ndio kumejaa walimu very professional. Lkn serikali inawakosea san na wao hawafanyi vema. Ila wapo vzr wakiwezeshwa.

Kwa Sasa naona si English Media Wala feza school hakuna lolote.

Huyu accountant ameniingiza kwenye matatizo makubwa mno.
Nakumbuka ilikuwa Januari nikiwa nimeandaa ada kama kawaida kianzio. Si akaikataa bana! Watoto wawili Kila mmoja laki Nne jumla laki nane, alidai Kila mmoja lazima owe 600K. Niliingia mkopo ambao unaniandama hadi sasa....

Mmiliki wa shule nilimuamini nikadamp wanangu lkn alitubadilia, alikataa hata end of Januari nikamilishe aligoma. Iliniuma Sana. Kwa hiyo mleta Uzi huu hili suala ni seriasi sana.
Yes uko sahihi, ila hoja yangu ni kwamba hizi shule za English Medium kama umejipanga siyo shule mbaya Sababu nzuri zipo na mbaya zipo pia. Mimi na pendelea zaidi shule binafsi zinazosimamiwa na taasisi za kidini au za Wahindi, za waswahili nyingi ni za hovyo. Shule zetu za serikali ni hovyo mnoo na kwa dunia tunayokwenda Mtoto hataweza pata vitu vya msingi vinavyokwenda na wakati. Chukulia mfano Agha khan Primary School huwezi fananisha na shule yoyote ya msingi ya serikali.
 
" English Medium zawaswahili nyingi ni ovyo" upo sahihi kabisa mkuu. Mbaya zaidi hizo za waswahili ndo zipo nyingi ndo maana ninaziita kayumba zilizo changamka
Wyatt Mathewson
 
Elimu ni nini?
Mpeleke mwanao shule ya Kayumba kama huna hela, ila usimpeleke mwanao Kayumba ili ujenge. Elimu ya msingi ni muhimu sana kama una uwezo mtoto asome shule nzuri. sio kila English Medium ni mbaya, nzuri zipo nyingi tu inategemea na mzazi ulifanya utafiti kabla au ulibabaishwa tu na majengo na mabasi mazuri ya kubebea watoto.
 
Umenikumbusha kuna lecture mmoja pale muhas kasoma st kayumba anaitwa david thomas kasomea mtera dam sec na form 4 2010 alitoka na 1

Kipanga wa st.kayumba anakuwaga kipanga kweli kweli tena wa kujitengeneza mwenyewe na sio wakutengenezwa..

Watu wana jua ukweli ila wanajifanya tu
 
Mpeleke mwanao shule ya Kayumba kama huna hela, ila usimpeleke mwanao Kayumba ili ujenge. Elimu ya msingi ni muhimu sana kama una uwezo mtoto asome shule nzuri. sio kila English Medium ni mbaya, nzuri zipo nyingi tu inategemea na mzazi ulifanya utafiti kabla au ulibabaishwa tu na majengo na mabasi mazuri ya kubebea watoto.

Ukiwa na hela ndo uzitumie kizembe mkuu? Hiyo haipo. Mpeleke Kayumba halafu msimamie vizuri atatoboa tu mkuu.

Umeongea point nzuri sana halafu tena unataka kuharibu.

Umesema English Medium za waswahili nyingi ni ovyo. Ni ubabaishaji mtupu.
 
1. Mtoto anatembea kilo mita 4 kila siku wenzake wanakaa kwenye gari. ( MKUU HUZIJUI FAIDA ZA KIAFYA ZA KUTEMBEA UMBALI MREFU ? Nenda ka google " Health benefits of walking" kukurahisishia tu ni kwamba hakuna mazoezi yenye afya kwa mwanadamu kama mazoezi ya KUTEMBEA muda mrefu. Moja kati ya FAIDA hizo ni pamoja na kuimarisha Misuli ya moyo ( kwa FAIDA ya wote kwenye mguu wa kushoto kuna misuli ambayo ipo connected na moyo. So unapokuwa unatembea unakuwa unaimarisha misuli ya moyo. Mtoto KUTEMBEA kilo mita nne kila siku kwa miaka saba ni bonge la advantage kwake kiafya. In addition to that kama ni mtoto wa kiume pia inasaidia kuimarisha misuli ya uume" penile muscles " na kustabelize hormones za kiume.

2. Darasa moja kuwa na wanafunzi mia vs darasa moja kuwa na wanafunzi 20:

Mtoto anatakiwa kukaa kwenye darasa la watoto wengi ili aweze kupata challenge kutoka kwa watoto wenzake... isitoshe huo ndio uhalisia wenyewe katika maisha kwa sababu huku mtaani kila sehemu ni watu kibao. So mtoto alie soma kwenye darasa lenye watoto mia anapokuja kwenye maisha halisi, uwepo wa watu wengi kwenye jambo lolote hauwezi kuwa changamoto kwake, mfano siku akienda kwenye interview ambayo shortlisted wapo watu elfu moja na wanao hitajika ni watu kumi, kwake haiwezi kuwa tatizo wala hawezi kuwa shocked kwa sababu alikuwaga anakuwa mtu wa TANO kati ya watoto 230. Kwa mtoto aliesoma kwenye darasa lenye wanafunzi 20 kwake hii itakuwa changamoto.

Kama hiyo haitoshi, chuo kikuu mfano UDSM kozi nyingi huwaga ni watu kuanzia mia 2 na ushee. Kuna kozi kwa mfano Education huwaga zina watu hadi mia 600 na zaidi. Mtoto wa kayumba hii haitamsumbua lakini st.junior hii itamsumbua.

Kingine mtoto akiwa kwenye shule yenye watoto wengi inamsaidia kujuana na watu wengi na hivyo kutengeneza network kubwa ( wanasema ur network is ur networth)

Tofauti na huyo wa darasa moja watoto 15, anakuwa hana network kubwa au atakosa network kabisa kwa sababu shule hizo hufundishwa pia tabia za kizungu kama vile ubinafsi .
Takataka
 
Inawezekana umeishia wapi! Kuna T.O mmoja wa hivi karibuni kutoka Kanda ya Ziwa. Anatoka familia ya kimaskini sana hadi alikuwa anaahirisha masomo akapige vibarua. Baada ya kuwa T.O. form four, akapewa ofa ya kusoma Feza Boys. Sasa hivi kamaliza form six na sio tena yule wa kupiga vibarua! Connections zipo hadi Ulaya Bro!
Huyo dogo ulitegemea apewe msaada na taasisi alafu wamtelekeze wakati yupo vizuri darasani
Sijakataa mtt kusoma hizo shule mpeleke ukiwa na uwezo na kwasabb ya kupata elimu bora na mazingira mazuri ya kujisomea
 
Kuna akina mama nitilie wanaoishi chumba kimoja wanasomesha watoto English medium kwa Vikoba ukimuuliza kwa nini anakwambia mwingine anasema mimi sitaki mwanangu wa kike aje kuolewa kama mimi asiyejua neno hata moja la kingereza msumbufu huyu tulisoma wote kayumba

Nampeleka mwanangu huko English Medium aweza.kutana na mwanaume wa kueleweka waliyesoma wote kuliko.hawa waswahili wa kayumba

Anakwambia wengi huoa au kuolewa na wale walisoma wote kama ulisoma Kayumba uwezekano mkubwa kupata msoma Kayumba mwenzio mkubwa sitaki.Changamoto nimepitia zinatosha.Kayumba wasumbufu uelewa mdogo
Hahaha...comment yako noma
 
Shule nzuri ni shule ambayo ina utilize uwezo wa mtoto.

St Kayumba sio good option kwa mtoto unless kipato sio kizuri. Nimesoma st kayumba from p' to o'level kwahiyo najua kitu nachokizungumza hapa so you better pay attention!

Watoto wanao excel shule za kayumba academically mostly wana biological advantage (wamezaliwa na uwezo mkubwa wa akili wa kuhifadhi kumbukumbu vizuri). Na wachache sana wanafaulu kwa jitihada binafsi za wazazi kama kuwapeleka tuition na ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mtoto shuleni (kuangalia kama anafanya homework vizuri n.k). Ila watoto wengi wa Kayumba wapo kwenye hatari kubwa sana ya kuharibikiwa. Nina mifano hai ya kutosha, so you better listen careful.

Anyday of the week, nitapigia kura International/English Medium over Kayumba kwa sababu ya utofauti mkubwa wa mifumo yao ya uendeshaji. Yes you heard me well, SYSTEM!

Mdogo wangu alibahatika kusomeshwa English medium, wakati yupo std 6 nilikua napiga naye story za hapa na pale nikagundua anajua vitu vingi ambavyo laiti angesimamishwa na hawa form four wengi wa kata kwenye debate, kwa kweli ingekua ni aibu.

Sasa shida iko wapi?

Kayumba hakuna ufuatiliaji wa karibu kwa watoto. At least hata English Medium za mchongo wanamrudisha mtoto mpaka nyumbani na wanampitia tena Ahsubuhi. Kila siku mtoto lazima aachiwe homework za kutosha kumpunguzia muda wa kucheza mtaani hovyo (Aliyocheza shuleni inatosha!).

Ila Kayumba mzazi huna uhakika kama mtoto kafika shule, huna uhakika kama mtoto atarudi nyumbani salama, huna uhakika kama muda aliofika nyumbani ndio wenyewe au kuna mahali kapitia, huna uhakika kama hajaachiwa homework au kaachiwa, hujui marafiki zake ni kina nani, hujui kama anahudhuria vipindi vyote au lah... na ikitokea siku umeitwa Shule ujue kabisa kuna kosa kubwa sana kafanya maana haya mengine ya ufaulu walimu sio shida zao, utajua mwenyewe na mtoto wako!
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Neno langu la faraja kwako ni kwamba

Watu tumesema shule hizohizo ymza kayumba na kata, tukaongea kingereza na kufaulu vizuri tu

Ila kinachohitajika sasa mazingira ya nyumbani hakikisha yawe ya kisomi.

Vitabu vingi, waunganishe maktaba, wajisomee sana.

Waache uswahili wote
 
" English Medium zawaswahili nyingi ni ovyo" upo sahihi kabisa mkuu. Mbaya zaidi hizo za waswahili ndo zipo nyingi ndo maana ninaziita kayumba zilizo changamka
Wyatt Mathewson
Mkuu

Any shule inayofata British GCSE au International Baccalaurette (IB) ndio international school hizo zingine ni shule za Kitanzania za private tu

Nafikiri bado hatujaelewana nini maana ya International School hapa Tanzania

Mna confuse shule ya Tanzanian curriculum ambazo ni private ambazo ni sawa tu na shule za serikali kimuundo

The real international school we are talking about here are IB and GCSE based schools not otherwise

Do not confuse please
 
Nina mtoto anasoma la Kwanza ila ana mwandiko mzuri kuliko darasa la 7 wa Kayumba
Anapiga hesabu za darasa la 4
 
Back
Top Bottom