Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Tatizo ni umasikini
Umasikini mbaya sana mkuu

Ungangali wa mtoto inategemea na wewe mzazi nyumbani, mtoto akirudi shule mpigishe kazi ndogondogo kama kujifulia nguo mwenyewe kulimalima vinyasi vinavyo zunguka nyumba,sio junia kaangalie katuni

anakomaa,kwasababu hata huko kayumba unako mpeleka ukimdekeza wenzake watamshika makalio
 
Q
Anadhani wazazi wanaouza viwanja kusomesha watoto ni wajinga.

Tuangalie mfano hai kwa Shilole ,aliweka bondi hati ya nyumba kusomesha watoto hii yote hii kutambua umuhimu wa elimu Bora kwa mtoto.

Huko St Kayumba ni bora liende tu.
Watoto wachache sana wawezao kuwaamhia wazazi wao asante kunisomesha Kayumba

Waliosoma Private watoto wengi asilimia kubwa hushukuru sana wazazi wao kwa kuwasomesha private.Sababu wanaona kabisa mzazi Ali sacrifice na alifanya maamuzi sahihi kwa future yake
 
Unamaanisha St Kayumba haifai kwa watoto wadogo ?
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
 
Unasema watoto walisoma Kayumba wanajiamini kuliko wale wa private.

Embu wachukue hao watoto wa Kayumba na hao wa private kila mmoja azungumze mbele ya umati wa watu uone nani anaweza kujieleza mbele za watu na nani hawezi.
 
Mawazo ya kimaskini.
 
Inaonesha umeshikwa sana matako
 
hivi kwanini hamna kiswahili medium sekondari na high school?
 
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
Mkuu kuna watu wanaendaga kusoma udkatari urusi hajui hata neno moja la kirusi. Mwaka wa kwanza anasoma lugha tu na mwaka wa pili ndo anaanza kusoma udkatari kwa kirusi na mwisho wa siku anaondoka na G.P.A ya 4 plus.

Tuliosoma miaka ya tisini asilimia kubwa tumesoma shule za kiswahili na seco tukatusua kama kawa.


Shule za kiswahili watoto wanaanza kufundishwa kiingereza darasa la.tatu. so wana soma kiingereza kwa miaka mitano. Kwa usimamizi bora wa mzazi,miaka mitano inatosha sana kwa mtoto kujua basics za lugha ya kiingereza ambazo ata zi apply akifika sekonndari.

Isitoshe siku hizi mambo mengi sana yamerahisisha usomaji kwa watoto.

Kuna programmes nyingi like Ubongo Kids. Kuna Vitabu, kuna videos kuna taasisi zinahusika na kusimamia maendeleo ya kitaaluma.ya wanafunzi, kuna tuitions etc.

So suala la lugha wala sio ishu kabisa kwa mtoto anaependa kusoma na ambae yupo chini ya usimamizi wa mzazi ambae yupo serious na maendeleo ya kitaaluma ya mtoto wake.
 
walikuwa shule gani kabla hujawaamisha? kama utaweza kujib llakini
 
Sahihi
 
T
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhal
Tafuta hela uache makasiriko.
Maskini mnafarijiana au sio. Waza madogo upate kidogo waza makubwa upate makubwa. Somesheni watoto shule bora ni haki yao ya msingi.

Sitaki povu
Yani mzazi ni mjinga anataka na vizazi vyake vibaki kwenye ujinga.
 
T
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhal
Tafuta hela uache makasiriko.
Maskini mnafarijiana au sio. Waza madogo upate kidogo waza makubwa upate makubwa. Somesheni watoto shule bora ni haki yao ya msingi.

Sitaki povu
Yani mzazi ni mjinga anataka na vizazi vyake vibaki kwenye ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…